wasalaam wakuu,kwenye jamii yetu tumeaminishwa kuwa watoto ni Malaika hawana dhambi wala hatia yoyote(hata mimi nakubali hili).sasa mimi nauliza kama kweli watoto ni Malaika kwa nini wana roho mbaya na tabia za ovyo?Mfano unakuta mtoto wa miaka chini ya miwili ni mchoyo na mbinafsi yaani kitu chake hatoi kabisa,watoto wengine wana wivu kama wanawake kwa mfano ulimweka chini na kubeba mwingine yeye anaumia na kuanza kulia(hapa nazungumzia wale wa chini ya miaka miwili,tabia nyingine ni ukorofi,matusi(nimeshuhudia mtoto wa chini ya miaka 2 anatukana),na tabia kubwa ni kiburi na dharau.naomba kujuzwa au shetani anawapa mafunzo ya uovu huko tumboni kwa mama zao tabia hizi nimezifanyia uchunguzi.Nawasilisha
%by Sir Khan.born 2 win%
Ndugu yangu hapa umechanganya madesa tu, ila ukweli ni kuwa watoto hawana roho mbaya hata kidogo. Ni kwamba hayo matendo yao yanayopelekea udhani kuwa wana roho mbaya, yanadhihirisha asili ya mwanadamu namna anavyotakiwa aishi hapa duniani, baada ya kuwa ameumbwa na Mungu. Kuna mambo mawili tu makubwa na ya msingi ambayo kwayo binadamu aliumbwa ili ayafanye. MOJA Ibada kwa ajili ya kumwabudu Mungu aliyeumba na PILI kufurahia maisha yake hapa duniani.
Kinachotokea sasa kwa mtoto kwa mfano umemununulia kitumbua halafu ukajaribu kumuomba akakunyima, ni kwamba kile kitumbua kinamfurahisha, iwe na kwa kukila au kwa kukivuruga kwenye mchanga bila hata kukila, hasa anapokuwa ameshiba tayari. Kwa hiyo kitendo cha mtoto kukunyima wewe kitu,hakunyimi kwa sababu anakuchukia au kwa sababu ni mchoyo, hapana, ila anakunyima kwa sababu kitendo cha wewe kukupa kile alichonacho kitamfanya akose kitu cha kumfurahisha tena, na yeye kusudi lake mojawapo kubwa ambalo kwalo aliumbwa ni aliumbwa ili afurahi. Kwa hiyo akikupa wewe automatically atakuwa amepoteza kitu cha kumfurahisha, na ukizingatia kuwa yeye hajui kuwa na wewe pia ni mhitaji kama alivyo yeye pia.
Ni kama wewe hapo ulipo una gari lako ukaamue kulidumbukiza mtoni liende na maji wakati mto hauhitaji hilo gari lako, haitamaanisha kuwa unaupenda mto huo au unauchukia. Hivyo ndivyo yalivyo mahusiano yetu sisi na watoto hasa hawa ambao hawajajua chochote. Kwa hiyo mtoto anapokunyima kitu, hakunyimi kwa sababu anakuchukia na anapokupatia pia, hakupatii kwa sababu anakupenda hapana, ni matendo ambayo yako automated tu katika maisha yao.
Mimi siyo daktari wa binadamu lakini maoni yangu kwa mfano mtoto anapozaliwa huwa ni lazima alie kama yuko kawaida. Mimi ninavyodhani ni kuwa huwa analia baada ya mwili wake kukukutana na hali ya hewa nyingine nje ambayo hakuwa ameizoea pindi alipokuwa tumboni mwa mama yake. Hali hii huwa inamghasi na ukirudi kweye point yetu kwamba binadamu aliumbwa ili afurahi, hali hiyo huwa inamnyang'anya furaha yake na hivyo kumsababisha alie. kwa sbabu huwa inamnyang'anya furaha yake.
Kwa hiyo Watoto hawana roho mbaya, na ukirudi kwenye imani utafiti wangu mimi umeshanionyesha kuwa siri zote za binadamu wakubwa kwa wadogo, kweye ulimwengu wa roho, zimebebwa na watoto, na ikitokea mtu yeyote asiyekuwa ana dhamira nzuri au ana mambo ya giza na akawa anajaribu kuwatumia ili wazifiche, kadri anavyojitahidi kuwafanya wazifiche, ndivyo kadri anavyowafanya wazidi kuzi-expose kwa kiwango cha juu zaidi ya kile ambacho alitaka wakifiche. Sharti moja linalohitajika hapa ili uweze kuvuna to the maximum kutoka kwa watoto, ni lazima uwe uko na Mungu tu na hauna mchanganyiko wa kitu kingine chochote, na siri watakazokuwa wanakulete ni zote nzuri na mbaya ila zote zimeunganika katika kusudi moja la kukufanya ujilinde na mwovu Ibilisi. Watoto huwa hawaangushi kwa hili na HAYUPO anayeweza kuwafanya wafanye otherwise, ni NATURAL GIFT yao kutoka kwa Mungu na HAYUPO BINADAMU ANAYEWEZA KUIPOKONYA
Mwisho, bunadamu aliumbwa ili afurahi,..., kwa hiyo hakikisha kuwa kila siku unaponyanyua mguu wako kutoka nyumbani kwako, mguu huo siyo wa kwenda kuondoa furaha ya mwingine, ila kuongeza. Pia hakikisha kuwa una Ibada na Mungu mmoja wa kweli, na ni Mungu mmoja tu anayetakiwa kuabudiwa, miungu hawana haki wala hadhi ya kuabudiwa, kwa sababu huwa wanafanya kazi kinyume na Mungu mmoja wa kweli
Natanguliza shukrani zangu!