wasalaam wakuu,kwenye jamii yetu tumeaminishwa kuwa watoto ni Malaika hawana dhambi wala hatia yoyote(hata mimi nakubali hili).sasa mimi nauliza kama kweli watoto ni Malaika kwa nini wana roho mbaya na tabia za ovyo?Mfano unakuta mtoto wa miaka chini ya miwili ni mchoyo na mbinafsi yaani kitu chake hatoi kabisa,watoto wengine wana wivu kama wanawake kwa mfano ulimweka chini na kubeba mwingine yeye anaumia na kuanza kulia(hapa nazungumzia wale wa chini ya miaka miwili,tabia nyingine ni ukorofi,matusi(nimeshuhudia mtoto wa chini ya miaka 2 anatukana),na tabia kubwa ni kiburi na dharau.naomba kujuzwa au shetani anawapa mafunzo ya uovu huko tumboni kwa mama zao tabia hizi nimezifanyia uchunguzi.Nawasilisha
%by Sir Khan.born 2 win%