Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,548
- 28,817
Walimu na watumishi wa halmashauri ni miongoni mwa wafanyakazi wa serikali wenye hali ngumu sana.
Ila nimejionea watumishi wa halmashauri wakisema kuwa huwa kuna mpango wanapewa mikopo isiyo na riba (mkopo wa hazina)
Hoja yangu kama kuna huo mpango basi serikali iwakumbuke na walimu pia.
Hawa ndugu zetu walimu hawana posho kabisa kama watumishi wengine wa serikali na hawana cha kuiba kazini. Kwa hiyo kwao kula kwa urefu wa kamba haiwezekani.
Serikali iwaonee huruma angalau wawe kwenye huu mpango itawapunguzia kwa sehemu kubwa makali ya maisha maana mikopo ya riba inawatesa sana.
Kwa wanaofahamu zaidi kuhusu mpango huu karibuni kuchangia.
Je, fungu hilo huwa ni kwa halmashauri zote?
Na fungu hilo hutoka wapi?
Na je, linawalenga tu walioko ofisini halmashauri au wafanyakazi wote walio chini ya halmashauri husika?