Kama watumishi wa Halmashauri wanapewa mikopo isiyo na riba, kwanini watumishi wengine wenye hali ngumu kama walimu wasiwekwe kwenye mpango huo?

Walimu ni watumishi wa serikali ambao inawezekana wanaongoza kwa kuwa na free time. Kilichobaki ni kuigeza hiyo free time kuwa pesa.
Walimu webyewe kutwa kucha KUBET Tu kisha mikeka ina chanika. Mwalimu una BETI? Ukienda bar UNASONGESHA???
 
Walimu na watumishi wa halmashauri ni miongoni mwa wafanyakazi wa serikali wenye hali ngumu sana.

Ila nimejionea watumishi wa halmashauri wakisema kuwa huwa kuna mpango wanapewa mikopo isiyo na riba kabisa.

Hoja yangu kama kuna huo mpango basi serikali iwakumbuke na walimu pia.

Hawa ndugu zetu walimu hawana posho kabisa kama watumishi wengine wa serikali na hawana cha kuiba kazini. Kwa hiyo kwao kula kwa urefu wa kamba haiwezekani.

Serikali iwaonee huruma angalau wawe kwenye huu mpango itawapunguzia kwa sehemu kubwa makali ya maisha maana mikopo ya riba inawatesa sana.

Kwa wanaofahamu zaidi kuhusu mpango huu karibuni kuchangia.

Je, fungu hilo huwa ni kwa halmashauri zote?

Na fungu hilo hutoka wapi?

Na je, linawalenga tu walioko ofisini halmashauri au wafanyakazi wote walio chini ya halmashauri husika?
​
We Bwana mdogo uwezo wako wa kufikiria na kupambanua mambo ni mdogo sana na una ujuaji mwingi wakati huna ujualo.

Hakuna mkopo usio na riba kwa watumishi wa Halmashauri pasipo walimu. Mkopo wa hazina hauchagui kada mkuu, wote wanalipa ukiwa na sifa.

Mi mwalimu nimekopa mkopo wa Hazina usio na riba. Jitahidi kufanya japo utafiti kidogo kabla hujaandika kitu mbele za watu. Unaonesha uchi wa akili yako kijana.
 
Mkopo usiokuwa na riba labda kwa walemavu ,labda ukute wanaweza kupata mikopo yenye riba nafuu kupitia mifuko ya Almashauri..Hata Taasisi za serikali zina Saccos za ndani ,zinawawezesha kupata mikopo mizuri kwa riba nafuu maana hao watumishi ndio wachangiaji wakubwa.

Baadhi ya Taasisi ambazo zina favour ya mikopo ni BOT ,wanaofanya kazi hapo wanaweza kupata mikopo mikubwa kwa riba ndogo ,ikiwa ni sehemu ya kuwapa kipaumbele ...TRA wana saccoss zao mtu anaweza. Kukopa mpaka milion 100 kwa riba nafuuu ,kunq Sumatra Saccos na nyingine.
 
We Bwana mdogo uwezo wako wa kufikiria na kupambanua mambo ni mdogo sana na una ujuaji mwingi wakati huna ujualo.

Hakuna mkopo usio na riba kwa watumishi wa Halmashauri pasipo walimu. Mkopo wa hazina hauchagui kada mkuu, wote wanalipa ukiwa na sifa.

Mi mwalimu nimekopa mkopo wa Hazina usio na riba. Jitahidi kufanya japo utafiti kidogo kabla hujaandika kitu mbele za watu. Unaonesha uchi wa akili yako kijana.
Sijajua nini kimekupanikisha mwalimu mpaka kunitukana? Huo uzi ni sehemu yangu ya utafiti kama umesoma vizuri maswali niliyouliza mwishoni yanaonyesha hilo

Labda niulize kwa nini walimu wengi hawafahamu kuhusu huo mkopo wa hazina?

Kwa sababu mimi nimewasikia tu watumishi wa halmashauri wakizungumzia kuuhusu
 
Walimu na watumishi wa halmashauri ni miongoni mwa wafanyakazi wa serikali wenye hali ngumu sana.

Ila nimejionea watumishi wa halmashauri wakisema kuwa huwa kuna mpango wanapewa mikopo isiyo na riba (mkopo wa hazina)

Hoja yangu kama kuna huo mpango basi serikali iwakumbuke na walimu pia.

Hawa ndugu zetu walimu hawana posho kabisa kama watumishi wengine wa serikali na hawana cha kuiba kazini. Kwa hiyo kwao kula kwa urefu wa kamba haiwezekani.

Serikali iwaonee huruma angalau wawe kwenye huu mpango itawapunguzia kwa sehemu kubwa makali ya maisha maana mikopo ya riba inawatesa sana.

Kwa wanaofahamu zaidi kuhusu mpango huu karibuni kuchangia.

Je, fungu hilo huwa ni kwa halmashauri zote?

Na fungu hilo hutoka wapi?

Na je, linawalenga tu walioko ofisini halmashauri au wafanyakazi wote walio chini ya halmashauri husika?
​
Mbona walimu wanapewa mikopo ya hazina!?? Haina riba !!! Wanaita mikopo ya vyombo vya usafiri
MImi ni mwalimu na wala sijawahi kubet na wala sijui hata hatua za kubet zilivyo.
Watz wanashida Sana vichwan huongea vitu wasivyovijua kabisa aiseee!! Nafikiri lishe duni na elimu duni ni tatizo
 
Acha kupotosha hata walimu nao ni watumishi wa halmashauri na mikopo hiyo inawahusu pia
Sijajua ni kwa nini walimu hawachangamkii hiii fursa wanakimbilia kausha damu?

Na kipi mwalimu afanye ili anufaike na mkopo wa hazina?
​
 
Nilichogundua kwenye huu uzi walimu hawana ushirikiano na hawapendani

Nimeona baadhi ya walimu wakisema kuwa kwenye huu mkopo wa hazina, mkopo usio na riba hata walimu wanaweza kuwa wafaidika kwa ssbabu ni wafanyakazi walio chini ya halmashauri

Cha ajabu hawataki kufunguka wenzao wafanye nini ili nao wafaidike na mikopo hii isiyo na riba

Inasikitisha sana, hii kada ndio maana inadharuliwa sana

Mpwayungu Village anachosemaga kuhusu walimu ni sahihi sana
​
 
Walimu na watumishi wa halmashauri ni miongoni mwa wafanyakazi wa serikali wenye hali ngumu sana.

Ila nimejionea watumishi wa halmashauri wakisema kuwa huwa kuna mpango wanapewa mikopo isiyo na riba (mkopo wa hazina)

Hoja yangu kama kuna huo mpango basi serikali iwakumbuke na walimu pia.

Hawa ndugu zetu walimu hawana posho kabisa kama watumishi wengine wa serikali na hawana cha kuiba kazini. Kwa hiyo kwao kula kwa urefu wa kamba haiwezekani.

Serikali iwaonee huruma angalau wawe kwenye huu mpango itawapunguzia kwa sehemu kubwa makali ya maisha maana mikopo ya riba inawatesa sana.

Kwa wanaofahamu zaidi kuhusu mpango huu karibuni kuchangia.

Je, fungu hilo huwa ni kwa halmashauri zote?

Na fungu hilo hutoka wapi?

Na je, linawalenga tu walioko ofisini halmashauri au wafanyakazi wote walio chini ya halmashauri husika?
​
Jamani mtawauwa walimu na mikopo maana wao wasisikie fursa mpya ya mikopo
 
Walimu ni watumishi ambao wakitumia free time vizuri na mazingira yao wanaweza kutengeneza pesa ya kutosha tu.
Tatizo mtaji, mwalimu ws level ya degree anaanza na mshahara take home 620k-670k​
 
Back
Top Bottom