Ni Sawa na una shida kwahio uuze kitendea kazi chako, no sio sahihi! Hata hivyo "smartphone ya shilingi ngapi" does guarantee kiwango cha shida au kiwango cha kuhitaji msaada. Very soon itakua kama basic need tu kuwa na smartphone. Sasa Mpwa nikiuza smartphone nitawezaje kutafuta kazi, kuperuzi taarifa za kazi na kutuma maombi???
Kwa mtazamo wangu, ingekua Mimi ningekusaidia kwa kadiri Mungu atakavyosaidia bila kuwa judgemental. Maana kama unaanza kuniuliza "simu ya shilingi ngapi", then possibly utaniuliza umevaa nguo za shilingi ngapi, viatu vya bei gani, umekula msosi wa bei gani, unaishi nyumba ya bei gani etc.
Kuwa na shida, stress, depression and the like hadi kufikia hatua ya kajinyonga au kuomba msaada doesn't mean niwe na simu ya being ndogo, niwe rough, nisiwe na makazi mazuri, No, TUNATOFAUTIANA KIWANGO CHA UHITAJI kwahio ukishindwa kunisaidia kwa sababu ya "bei ya simu" nitakushangaa Mpwa.
Miaka kadhaa hapa jukwaani alijitokeza binti mmoja akaanzisha Uzi kuwa "Anauza Uchi ili aweze kuishi mjini na apate ada". Nilimfuata inbox tukaongea kwa kirefu sana na niliweza kumpa nilichompa, nimefurahi siku moja kumuona amekua AGENT anatangaza bidhaa sake kwenye makundi ya WhatsApp.
Sasa tukisema uza simu au lugha yoyote yenye uelekeo wa kuwa judgemental hatutakua tunawasaidia, wengine tunahitaji maneno ya faraja tu.
Hapo vipi Mpwa, nikutakie Siku njema.