Ni uduni tu wa fikra na imani chafu za kishirikina ndiyo vimekupeleka kwenye conclusion za namna hiyo.
Mtegemee Mungu kwa kila jambo, fanya kazi kwa bidii, utayaona mafanikio.
Watu wa Njombe, wanajituma sana kwenye kazi, na hawana maneno mengi.
Marehemu Makweta aliwahi kusema kuwa alipoenda kwenye jumba la makumbusho ya makoloni ya Ujerumani, alikutana na waraka mmoja toka Tanganyika kwenda kwa watawala wa Ujerumani, ukisema kuwa, Itapita miaka mingi mpaka Tanganyika kuhitaji matrekta kwa sababu kazi zinazofanywa na matrekta, zinaweza kufanywa na watu wa kutoka maeneo ya Iringa, Ruvuma na Kigoma.
Tena wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA, ukienda kuomba kazi, swali la kwanza lilikuwa, unatoka wapi? Ukisema Tanga au Dodoma au Mtwara, unaambiwa kazi hakuna. Ukisema unatoka Njombe au Kigoma, unaambiwa, kimbia haraka uuangane na wenzako, uanze kazi. Yote hiyo ikidhihirisha kuwa watu wa maeneo hayo, kiasili ni wachapa kazi hasa.
Sasa hivi, kutokana na bidii yao, wamefanikiwa kumiliki biashara nyingi Kariakoo na hata Dodoma. Halafu, wengi wao siyo chawa wa wanasiasa, wanategemea zaidi bidii yao ya kazi.