Kama wewe ni mwanaume na hakuna sehemu unaweza ukaaminika ukapewa milioni 1 hadi 3, jitafakari

Kama wewe ni mwanaume na hakuna sehemu unaweza ukaaminika ukapewa milioni 1 hadi 3, jitafakari

Sioni kama ni dhihaka, anachoongelea ni cha kutafakarisha. Mfano unapata msiba, hakuna hata wa kukupa rambirambi, taswira inayojitokeza ni kuwa, huna mahusiano mazuri na watu, ama mahusiano yenu ni ya kinafiki.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Kuwa na mahusiano mazuri na watu ni kitu kingine na kuwa na uhakika wa kupata milioni mbili ukiwa na shida ni kitu kingine.

Unaweza kuwa na mahusiano mazuri na 'pangu pakavu' wenzio ambao nao wanahemea kama wewe, unadhani unaweza ipata milioni toka kwao?

Kuna dhihaka kubwa sana hapo ila imejaribu kuwaficha wanaopokea mambo bila ya kutafakari kwa kina, tulia utaiona.

Kwa hiyo unataka tuelewe kuwa, ukiwa na kitu huna haja ya kuwa na mahusiano mazuri na watu?

Ova
 
Kuna rafiki yangu nilimtafutia kazi mahali, vigezo vyote alikidhi, ila tatizo lilikuja barua ya mdhamini hana, mpaka leo hii ninapozungumza amekosa kazi kwa ajili ya mdhamini, tuishi vizuri na watu.
Sasa kwanini hukumdhamini wewe kama ni jamaa yako?
 
Hata wewe unaandika hivi sababu unahisi utasaidiwa....subiri matatizo yakufike, huwa hawapokei simu hao
 
Kuna kipindi huwa tunapata matatizo ya ghafla, eidha msiba, maradhi etc. Kipindi kibaya siku zote huja ukiwa hauna kitu yaani mweupe kabisa mfukoni na unakuta kuna uhitaji wa pesa.

Sasa kama wewe ni mwanaume haswa na hakuna sehemu unaweza ukaaminika ukaazimwa chochote iwe kazini, marafiki, ndugu au mtaani kwako jitafakari aiseeeh.

Kuna rafiki yangu nilimtafutia kazi mahali, vigezo vyote alikidhi, ila tatizo lilikuja barua ya mdhamini hana, mpaka leo hii ninapozungumza amekosa kazi kwa ajili ya mdhamini, tuishi vizuri na watu.
Ama ukiweza kumuunganisha kazi, ulishandwaje kuwa mdhamini wake?
Maana umesema ni rafiki yako
 
Back
Top Bottom