Kama wewe ni mwanaume na hakuna sehemu unaweza ukaaminika ukapewa milioni 1 hadi 3, jitafakari

Kuwa na mahusiano mazuri na watu ni kitu kingine na kuwa na uhakika wa kupata milioni mbili ukiwa na shida ni kitu kingine.

Unaweza kuwa na mahusiano mazuri na 'pangu pakavu' wenzio ambao nao wanahemea kama wewe, unadhani unaweza ipata milioni toka kwao?

Kuna dhihaka kubwa sana hapo ila imejaribu kuwaficha wanaopokea mambo bila ya kutafakari kwa kina, tulia utaiona.

Kwa hiyo unataka tuelewe kuwa, ukiwa na kitu huna haja ya kuwa na mahusiano mazuri na watu?

Ova
 
Kuna rafiki yangu nilimtafutia kazi mahali, vigezo vyote alikidhi, ila tatizo lilikuja barua ya mdhamini hana, mpaka leo hii ninapozungumza amekosa kazi kwa ajili ya mdhamini, tuishi vizuri na watu.
Sasa kwanini hukumdhamini wewe kama ni jamaa yako?
 
Hata wewe unaandika hivi sababu unahisi utasaidiwa....subiri matatizo yakufike, huwa hawapokei simu hao
 
Kumkopesha mtu Dunia ya sasa ni kutafta pressure bure
 
Ama ukiweza kumuunganisha kazi, ulishandwaje kuwa mdhamini wake?
Maana umesema ni rafiki yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…