Umekuwa unarudia rudia maneno. Mfano kama nikisema ivi "dhana ya Mungu yupo ni kweli kwa sababu kuna mbingu na ardhi, mbingu na ardhi zinathibitisja uwepo wa Mungu, kwa sababu kama hakuna mungu basi hakuna mbingu, dhana hii inathibitishwa kuwa kweli kuwa mungu yupo" ni kama umezunguka tu lakini bado hujafafanua. Kwenye Polygon unaweza kupata pembe tatu ukichora mistari yako ndani ya polygon.kwenye hio pembe sita unaweza ukaweka mistari na ukapata pembe tatu kwenye sita, kwa sababu kwenye idadi ya sita, 3 imo ndani.
Ambacho sijafafanua ni kipi?
Unaelewakwamba sijasemakwamba kwenye polygon huwezi kupata pembe tatu, nimesema hakuna pembe tatu ambayohapohapo nipembe tatu na pembe sita?
Unaelewa tofauti?
Unatumia hoja dhaifu ya kulaumu kwanini Mungu anaachia maovu na maasi yanatokea duniani. Wakati yote haya ni matendo ya binaadamu,
Kwanza unaelewa kwamba silaumu, nakosoa kutokuwepo kwa logical consistency?
Unaelewa hilo?
Pili, unasema yote hayo ni matendo ya binadamu, Mungu alipokuwa anaumba ulimwengu, kabla binadamu hajaumbwa, alishindwa kuumba ulimwengu ambao binadamu hana matendo hayo na hawezi kuwa na matendo hayo?
Hujajibu swali hili, nimeshaliuliza kwakujua utakujana point hii. Hujajibu.
na Mungu tayari ameshatangaza malipo yake nini kwa waovu na wema.
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kwaio binaadam ana freewill and not controlled,
Wewe leo una free will ya kurudi mwaka 1982?
binaadamj anacontrol his own destiny, ameshapambanuliwa lipi baya na lipi zuri..
Mnajichanganya, mara mnasema binadamu hajikomboi mwenyewe, ila kwa neema ya Mungu tu anakombolewa, mara mnasema binadamu ana uchaguzi mwenyewe.
Kipi ni kweli hapa? Ana freewill na ana contraol destiny au anapata kumjuaMungu na kwenda peponikwa neema ya Mungu tu?
Lakini wakati wewe unatumia hoja ya maovu ya dunia na kusema ndio maana Mungu hayupo,
Ambayo hujaijibu.
basi mazuri yanayotokea duniani ni ushahidi wa kuwa Mungu yupo, kwa sababu yanaendana na sifa zake.
Kama mazuri ni ushahidi kwamba Mungu yupo, maovu ni ushahidi kwamba hayupo?
Unaweza kuthibitisha kwamba mazuri haya hayatokani na kingine chochote zaidi ya huyo Mungu?
Mimi naweza kusema angekuwepo, asingeweza kuruhusu mabaya yawepo, na mabaya yapo, kwa hiyo hayupo.
Wewe unaweza kuniambia imekuwaje Mungu huyoawepo halafu aumbe ulimwengu unaoruhusu mabaya, wakatialikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya?