Kama wewe sio Freemason basi hujui chochote kuhusu Mungu wala ulimwengu

Usilazimishe mambo.

Kwa hiyo tumaini haliwezi kupatikana kutokana na hiyo logic yako ya TRUE au FALSE?
 
Usilazimishe mambo.

Kwa hiyo tumaini haliwezi kupatikana kutokana na hiyo logic yako ya TRUE au FALSE?
Umeielewa sawasawa maana ya hilo neno tumaini..

Nioneshe wapi neno tumaini linasimama kati ya true au fallacy... wapii

Pale katika kauli yako inamaanisha ulikuwa neutral ikijidhihirishia zaidi kwamba wewe kuna nguvu ambazo zimekuzidi uwezo ambazo unazitumainia kwamba zimemfanya jamaa awe salama
 
Hivi umeelewa maana ya neno "Tumanini" mkuu??
Unalazimisha mambo kwa logical non sequitur.

Unachoandika hapa ni sawa na kusema.


1. Wanawake ni watu.
2. John Pombe Magufuli ni mtu.
3. Kwa kuwa wanawake ni watu, na John Pombe Magufuli ni mtu, hivyo...
4. John Pombe Magufuli ni mwanamke.

Unaunganisha mambo ambayo hayana muunganiko.

Unalazimisha tumaini lisiendane na logic.

Unalazimisha mtu anaposema "natumaini sitagongwa na gari, kwa sababu naangalia kwa umakini kulia na kushoto kabla sijavuka barabara" awe hajatumia logic.

Eti kwa sababu ametumaini.

Unafanya kosa la logical non sequitur.

Unalazimisha conclusion ambayo haina uhusiano na premises.
 
Hio mfano wako ulioutoa hauwezi kuwa logically proved, unajua kwann...??
 
"natumaini sitagongwa na gari, kwa sababu naangalia kwa umakini kulia na kushoto kabla sijavuka barabara"

Nioneshe ni kwa jinsi gani hii sentensi inaweza kuchanganuliwa na kuwa logical sentence...?

How..?
 
Turudi tena kwenye definitions, ili tuelewane sawa.

Naomba u define logic.
 
Define logic please.
Logic in oxford dictionaries imetafsiriwa kama ifuatavyo.

"Logic is reasoning conducted or assessed according to strict principles of validity"

"Logic is a method of reasoning that involves a series of statement judgement by following strict principles of validity"

By the way..
Unazifahamu principles of validity za logic??
 
Nimefanya formal truth table analysis ya logic, ambayo inabeba hizo principles za validity, tangu 1995.

Sina hakika kama ulikuwa ushazaliwa mwaka huo, kwa uandishi wako hapa.

Sasa kwa definition yako hiyo uliyotohoa mtandaoni ya logic, tunaweza kutumia logic kupanga mambo ya kesho kwetu?
 
Mkuu mbona unataka kutoka nje ya mada..

Kuzaliwa au kutokuzaliwa kwangu kwenye huo mwaka hakuingiliani na tunachokizungumzia hapa.

Turudi kwenye mada

Hiyo TRUTH TABLE yako ulioitengeneza kutokea kwenye sentensi iliyokuwa na neno "natumani" umeitengeneza vp...?

Naomba uniwekee hapa niione

Ipige hata picha uipost hapa.

Ninachotaka nijue neno "natumani" limewezaje kuingia kwenye "logical sentence"

Na ndio maana nikakuuliza unazifahamu principles za validity of logic vizuri?

Nijibu kwanza
 
Naomba niwekee PRINCIPLES OF VALIDITY OF LOGIC hapa

Niweke hizo principles hapa kwanza ndipo tuendelee maana nisije nikawa naongea na mtu kumbe najichosha tu.
 
Mkuu mbona unataka kutoka nje ya mada..

Sijatoka nje ya mada, nakujibu kwa kituo. Nazama kwa kina kwenye mada.

Kuzaliwa au kutokuzaliwa kwangu kwenye huo mwaka hakuingiliani na tunachokizungumzia hapa.

Umeuliza kama najua principles za validity ni nini, nimekujibu kwamba sio tu nazijua, bali pia, kwa uandishi wako hapa wa logical non sequitur za kusema wanawake ni watu, Magufuli ni mtu, hivyo Magufuli ni mwanamke, inaonekana kama huo mwaka 1995 nilipoanza kuchunguza logic kwa truth table, wewe ulikuwa hujazaliwa.

Hujakanusha.Unalalama tu.

Turudi kwenye mada

Mimi sijatoka kwenye mada. Rudi wewe.

Hiyo TRUTH TABLE yako ulioitengeneza kutokea kwenye sentensi iliyokuwa na neno "natumani" umeitengeneza vp...?

Kwa probability, unaelewa kwamba unaweza kutumia logic kwa probability?

Naomba uniwekee hapa niione

Ipige hata picha uipost hapa.

Ninachotaka nijue neno "natumani" limewezaje kuingia kwenye "logical sentence"

Na ndio maana nikakuuliza unazifahamu principles za validity of logic vizuri?

Nijibu kwanza

1. The probability of Member A being sick is 1%
2. The probability of Member A being not sick is 99%
3.It is logical to assume Member A is not sick.

Unachotaka kulazimisha hapa, kwamba logic ni lazima iende na certainty ya TRUE or FALSE, na haiwezi kutumika kwenye probabilistic reasoning, maana yake ni kwamba, hatuwezi kutumia logic katika kupanga mambo ya kesho.

Kwa sababu hakuna anayejua kwa hakika kama tutaiona kesho kwa uhakka wa TRUE or FALSE.

Ndiyo maana nimekuuliza swali ambalo mpaka sasa umekwepa kujibu.

Nimekuuliza, unaweza kutumia logic kupanga mambo ya kesho?

Hujajibu.

Kwa sababu unajua ukikubali kwamba unaweza, utakuwa umekubali kwamba unaweza kutumia logic katika jambo linaloenda kwa probability ambalo halina uhakika wa TRUE or FALSE.

Pata shule ya bure hapa kuhusu probabilistic logic and truth preservation.


 
Mkuu nini maana ya Probability...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…