Kama wewe sio Freemason basi hujui chochote kuhusu Mungu wala ulimwengu

"Mteja unaempigia hapatikani kwa sasa..Tafadhali jaribu tena baadae"
 
Huyo mtu akifa na kichwa chake kisifanye kazi, kutakuwa na maiti ya mtu mmoja au wawili?
Hahaahha Hata wawe Mia! Swali langu ni rahisi Mno! Sijataka Kujua Hesabu hapa!
Any way Tuachane na Hayo "Niambie Galaxy, Dunia na Maisha ni nini”

NB Kama Utasema chanzo cha maisha ni hisabati Nitajie huyo Aliyeifanya hiyo hisabati na Kufanya Galaxy, Cosmic na Maisha Kuwepo katika Nyanja hizi.
 
Kwanini tuachane na hayo wakati hayo yanakupa jibu kukufumbua macho kuhusu haya?

Unakubali square root ya 2 ni 10?

Unaweza kuiandika kwa kikamilifu square root ya 2 katika decimal point notation?

Unaelewa uhusiano wa habari hii na swali ulilouliza?
 
Kiranga Acha Ubabaishaji! Nimekuuliza Swali "Nani" Au "Nini" Unachotakiwa Ni kunijibu Tu kuwa Ni Kipi! Kama tuliumbwa na hesabu Sema "Hesabu"! Kama Na Tulizuka Tu Sema "Tulizuka" Kama tuliumbwa Na mbuzi Sema "Mbuzi" Usianze Kuingia Kwenye Vichaka na Kutafuta mbinu za kulikwepa swali kijanja!

"Sema hapa Dunia Inakusikia Kiranga"
 
Nikikuuliza rangi ya wimbo wa taifa wa Tanzania ni rangi gani, utaweza kunijibu ni rangi gani?
 
Nikikuuliza rangi ya wimbo wa taifa wa Tanzania ni rangi gani, utaweza kunijibu ni rangi gani?
Sawa Ukiniuliza hivyo "nitajibu Swali" sitakuuliza swali! Nitasema hivi, Wimbo wa taifa Hauna rangi yoyote bali Una Maneno yenye maana na Melody ndani yake!

So Hata Wewe hapa Hutakiwi Kuniuliza swali Unatakiwa Kujibu "labda" Binadamu Hatukuumbwa wala Kuzuka Bali "Tulitengenezwa". Na kama Tulitengenezwa Umtaje Aliyefanya hiyo kazi.

Ninachotaka Ni ujibu Swali Sio Uniulize Tena Swali, Kama ambavyo mimi nimekujibu kwenye hilo Swali lako.
 
mkuu LIKUD nadhan research uloifanya unazo data za kutosha naona ni bora uiweke kwa ufafanuzi mzuri mkuu iyo robo page kwa reseach yako sioni kama umeitendea aki
 
Katika Socratic method unaweza kujibu swali kwa swali.

Tatizo sijui kama ushawahi hata kuisikia Socratic method. Kwa jinsi unavyoandika unaonekana hujawahi kuisikia.

Hata Yesu alipoulizwa na watu kama walipe kodi kwa Kaizari au wasilipe, alitoa sarafu na kuwaonesha watu na kuwauliza, sarafu hii ina picha ya nani?

Alijibu swali kwa swali, lakini swali alilotumia kujibu swali lilitoa mwanga mzuri sana.

Watu walipojibu sarafu ina picha ya Kaisari, akasema, mpeni Kaisari vya Kaisari.

Akawa kaonesha kwamba ni sawa kumlipa kodi Kaisari kwa sababu hata fedha ina sura yake.

Sasa wewe ungekuwa katika mkutano huo, kwa kukataa swali kujibiwa kwa swali, ungeweza kukataa hilo jibu na kusema "jibu swali".

Wakati huelewi kwamba swali linaweza kuwa jibu zuri sana la swali lingine.
 
Utawezaje Kuanza Kujifanya Unamzungumzia Yesu hapa?, Ambae alikuja Kueneza habari ambazo wewe unazipinga! Unataka Kuniambia Kuwa umekosa Jibu Umeamua Kumkimbilia Bwana Yesu akuokoe kwa kuanza kufanya niamini Maisha na Mafunzo yake!

Mimi Yesu Simuamini!

Turudi Kwenye maada Na Uhalisia wa Sasa, Dawa Ya Deni ni kulipa na Dawa ya swali Ni Jibu.

Nipe Jibu la swali Nililokuuliza, Mimi Yesu, sijui na watoza Kodi "Siwajui!"

Nijibu Tumeumbwa/ Tumetengenezwa/Tumezuka/ Kutokana Na Nini?

Maana Sioni Sababu Mzee Kila Siku Unakuwa Unawasumbua Watu hapa Kumbe We Mwenyewe Hujui Lolote! Nipo Mbele Yako Kutaka Kujua mwanzo wa Cosmic na Life Ni nini, kwa wwwe unavyojua.
 
Yesu anaweza kutumiwa kuelezea falsafa. Na mtu ambaye haamini Mungu yupo wala haamini Yesu ni Mungu lakini anakubali mafundishobfulani ya Yesu yalikuwa mazuri. Kama mtu. Kama mwanafalsafa.

Falsafa za upendo alizofundisha Yesu sina tatizo nazo.

Nimeongelea mwanafalsafa mwingine, Socrates. Hujamtaja. Nina shaka kama ushawahi hata kumsikia.

Jibubla swali lako ni kwamba, hata nikisema sijui kama tumeumbwa au tumetokeaje, hilo halinifanyi nikose kujua kwamba Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ambaye kaumba ulimwengu huu uliojaa maovu, hayupo.

Kama vile ambavyo, sihitaji kujua square root ya 2 kwa ukamilifu ni nini ili kujua kwamba haiwezi kuwa 10.

Kwa sababu gani?

Majibu yote haya, hilo la Mungu huyo kuwapo na la square root ya 2 kuwa 10, yana contradiction, cintradiction inayoonesha uongo.

Kwa hiyo sijui tumetokeaje, lakini kutokujua huko hakunizuii kujua kwamba huyo Mungu ni jibu la uongo. Kwa sababu ana contradiction. Dhana ya kuwepo kwake ina cintradiction.

Jibu la huyo Mungu kuwapo ni sawa na ntu aseme square root ya 2 ni 10, au aseme kuna pembe tatu yenye pembe sita katika Euclidean plqne geometry.
 
Sawa Kwa hiyo jibu ni kuwa "Hujui"
 
Sawa Kwa hiyo jibu ni kuwa "Hujui"
Lakini kutokujua huko hakunifanyi nikipewa jibu la uongo kama vile Mungu nisilitambue kwamba hili ni jibu la uongo.

Sijawahi kudai kwamba najua chanzo cha maisha au ulimwengu umeanzaje.

Ukisoma sana Quantum Physics hata habari ya mambokuwa na mwanzo imehojiwa na kuonekana haina maana katika level fulani ya spacetime continuum.

Kwa hiyo ukifika kwenye basic fabric of space and time swali hili linakosa maana.

Siku zote huwa nasema habari za kuwepo Mungu huyu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote, uwezo wote, aliyeumba ulimwengu ni za uongo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake ina contradictions kubwa sana.
 
Kabla ya Simu kuwapo Duniani, Mtaalam aliyeivumbua Alienda kwa watu wengi sana Kuwaambia kuhusu wazo lake Na alionekana Ni Mwehu! (Chizi).

Huku wengi Wakiweka wazi kuwa Wazo Lake lilikuwa Na Contradiction kubwa sana! lakini Kuna Baadhi Wachache walioamini, (Imani ya Kuamini usichokiona) Na Baadae Ile imani ikaja Kuwa kweli Miongoni mwa Walioamini na wasioamini!

Tukija Kwenye Suala la Mungu Changamoto ni kama ile ile ya kipindi za Uvumbuzi Wa Vyombo Mbali mbali Vya Kilectroniki Karne ya 19, 20, na 21!
Ambavyo Vingi Havikudhaniwa Kabisa kama Vitakuja Kuwapo!

Kifupi, Anayesema Jambo Lipo, Ana nafasi kubwa ya Ushindi Kuliko yule anayesema Halipo!

Bila kuwa na Imani ya Kuhisi jambo Lipo Dunia mpaka Sasa ingekuwa Ni Bush! Watu wangekuwa Hawana Chochote zaidi Walivyo Kiasili (Uchi)

Sikuhisi Vibaya Kwa kumpinga Mungu, Ni dhana Yako Uliyonayo Kichwani unayohisi ni Sahihi, Ila Si Vyema Kwenda Mbele ya Watu Na Kuanza kuwapinga Huku ukijaribu Kuwatoa Kwenye Imani yao, Ili hali wewe mwenyewe Hujui Lolote kuhusu Unaloongelea! Ni Vyema Kuwaacha Wandelee Kumuamini Huenda yupo! akaja Kuwa Msaada kwao Hao wanaoamini, Lakini Pia na wewe!

Maana Waliokuwa wanapinga Kuwa Haiwezekani Kukawa na Kitu kinachopaa angani (Ndege) Siku Zilivyokuja kubuniwa, wenye Imani na Wale Ambao walikuwa wanapinga Kuwa Haiwezekani walizipanda!

Umekiri wazi Kuwa Hata wewe Hujui. Basi Acha Kubishana Na Hao Wanaohisi Yupo Maana Huenda Kweli Yupo hata kama Sifa zake zina Tofauti Kidogo na wanavyoamini.
(Kwa sababu Imani Lazima iwe Na Changamoto kidogo Vichwani Mwa Watu)
 

Tofauti yako wewe na hao waliosema simu inawezekana kuwepo wakaambiwa dhana yao ina contradiction, ni kwamba, wenzako wameweza kuthibitisha simu inawezekana kuwepo, kwa vitendo.

Wewe hujaweza kuthibitisha Mungu yupo, hata kwa nadharia.

Thibitisha Mungu yupo.
 
pharao kuna uwezekano mkubwa sana Kiranga akawa anaamini uwepo wa Mungu katika maisha yake halisi isipokua tu na yeye anakutana na ma atheists huko ambao wanampiga maswali asiyoweza kuyajibu kwa sababu ya ufahamu wake mdogo kuhusu Mungu.

So anahitaji msaada. MPE darasa mkuu.
 
Ukianzana "kuna uwezekano"unaweza kuendeleza chochote hapo.

Tuambie kitu chenye uhakika zaidi ya "kuna uwezekano".
 
Ukianzana "kuna uwezekano"unaweza kuendeleza chochote hapo.

Tuambie kitu chenye uhakika zaidi ya "kuna uwezekano".
Jibu maswali ya pharao tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…