kwanini unasema mungu hayupo?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ambaye ameumba ulimwengu huu uliojaa mabaya, hayupo, ni dhana tu, tena dhana potofu inayoweza kuoeshwa kimantiki kwamba inajipinga yenyewe. Ina contradiction.
Kusema Mungu huyo yupo ni sawa sawa na kusema kuna "pembe tatu yenye pembe sita" katika Euclidean plane geometry.
Yani ni kitu ambacho definition yake yenyewe ina mambo mawili yanayojipinga, kwa hiyo hakiwezi kuwepo kiuhalisi.
Mungu huyo anajipinga kama "pembetatu yenye pembe sita"
Angekuwepo, utakatifu wake, ujuzi wake, upendo wake na uwezo wake mkuu, usingeruhusu ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya mengi kama huu uweze kutokea.
Kama unakubali Mungu huyo yupo, imekuwaje akaruhusu ulimwengu huu uweze kuwepo ilhali una uwezekano wa kuwa na mabaya mengi sana?
Jibu la shetani halitoshi, kwa sababu shetani alikuja baadaye, naongelea uumbaji wa ulimwengu kabla shetani hajakuwepo. Ukisema mabaya yamesababishwa na wanadamu kula tunda bustani ya Edeni, nitakwambia kabla ya binadamu kula tunda Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hawawezi kula tunda, kwa nini hakuumba huo?
Mungu huyo hayupo. Ni hadithi tu.