Yametimia, Joe Biden keshachagua mgombea mwenza. Nilikuwa nasoma sehemu kwamba Democrats walishauri achague mgombea mwenza mwanamke tena mweusi: Binafsi nilihisi labda wanatania au wameenda mbali sana lakini yametimia. Hapa inamaanisha kwamba huyu babu Joe Biden mwenye miaka zaidi ya 77 akiwa Rais na akifia madarakani basi taifa la Marekani litakuwa na Raisi mwanamke wa kwanza, tena mweusi.
Sasa kama huyu babu Biden ameshauriwa vizuri au vibaya, binafsi sifahamu. Lakini ambacho nina uhakika nacho asilimia 100% ni kwamba watu wakifikiria kwamba endapo huyu babu atashinda na bahati mbaya akafia madarakani basi Kamala Harris ndiyo atakuwa Rais wao, nadhani italeta sana shida.
Japo kimkakati inaweza kuwasaidia kupata kura za weusi na zile za wanawake, lakini nikiangalia kile ambacho alifanywa Hillary Clinton kwasababu ya jinsia yake na kile ambacho alifanywa Raisi Obama kwasababu ya rangi yake nachelea kusema kwamba huyu mama atakuwa na kipindi kigumu sana. Mfumo siyo rafiki kwa mwanamke mweusi, hivyo kama ni chuma cha pua anatakiwa awe chuma cha pua haswaa.
----