Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Nimesoma mahali kuhusu Kamanda Tundu Lissu kuandika barua mbili kwa IGP kuomba kuhakikishiwa usalama wake ndipo arejee nyumbani Tanzania.
..Nimesikiliza mahojiano kati ya Mh.Tundu Lissu na kituo cha habari cha Clouds.

..Watangazaji walimuuliza Tundu Lissu atarejea lini, na jibu alilowapa ni kwamba anasubiri IGP Sirro amkubalie maombi yake ya kupewa ulinzi mara atakaporejea nchini.

..Na Mh.Lissu amedai kwamba IGP ameandikiwa barua mbili kuhusu suala hilo lakini hajajibu hata moja.

cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Mag3, Erythrocyte , Richard, Stuxnet , tindo, Salary Slip , Mzee Mwanakijiji
Mkuu Joka Kuu, asante kwa taarifa hii ya Lissu kuandika barua kwa IGP, kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake kwanza ndipo arejee home, nyumbani Tanzania.

Hatua hii ni nzuri na muhimu sana ili angalau Lissu na dereva wake warejee nyumbani ili sasa ndio vyombo vyetu vya uchunguzi vianze kazi uchunguzi ya kuwabaini wasiojulikana, waliomshambulia Lissu, maana tangu ameshambuliwa vyombo vya uchunguzi vilishindwa kufanya uchunguzi wowote hadi wamhoji Lissu na dereva wake!, this means if they both would have perished in that event, ingekuwa case closed!.

Jeshi letu la polisi ni jeshi lenye utu sana, baada tuu ya shambulio, polisi waliarifiwa within minutes, na kutoka eneo la tukio na kituo cha polisi ni just 10 minutes drive kutoka kituo cha polisi hadi kwenye crime scene, lakini polisi hawakuwa na haraka kufuatia eneo hilo kuwa ni secured area, hivyo walifika baada ya masaa 2, wakakuta Lissu ameisha kimbizwa Dodoma hospital na hawakukuta mtu mwingine yoyote aliyeshuhudia, wala hakuna hata na mlio wa risasi uliosikika!.

Licha ya shahidi muhimu wa tukio hilo, dereva wa Lissu kutojeruhiwa na alikuwa available siku nzima, ila polisi wetu walingia utu na ubinaadamu wa kutochukua maelezo yeke ili kumpa nafasi ya kutosha shahidi huyo pekee, kupumzika na kupumzisha mawazo, watamchukia maelezo wakati wowote kwani maelezo yana haraka gani ? Hadi kuchukuliwa mapema huku watu wana photographic memory hata baada ya miaka 3, watakumbuka every details hata tiny details!.

Lissu na dereva wake walipokuwa Nairobi ambapo ni karibu, jeshi letu la polisi liliingia utu wa kutowahoji ili kusubiria wapone. Walipokwenda Belgium kufuatia kule ni ulaya, na rais Magufuli hapendi safari zisizo za muhimu, kwa vile uchunguzi huo sio muhimu kivile na hauna haraka, jeshi letu la polisi lilingia tena huruma kuwaacha hadi wapone na kurejea nyumbani Tanzania ndipo liwahoji na uchunguzi ndipo uanze.

Hivyo sasa wanasubiriwa kwa hamu Tundu Lissu na dereva wake warejee nyumbani nchini Tanzania ndipo uchunguzi wa tukio la shambulio lile uanze!.

To be honest, baada ya mimi kuangalia ile hard talk ya BBC, nilisema hivi
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela! - JamiiForums

Hivyo Kamanda Tundu Lissu, "East, West, home is best" , karibu sana nyumbani, huna haja ya kusubiri majibu ya IGP Kamanda Sirro kukuhakikishia ulinzi na usalama wako, Yule YEYE aliyekulinda na kukuepusha na kifo licha ya kupigwa risasi 16, ni mlinzi mzuri kuliko vijana wa Siro!.

Kuhusu wale wasiojulikana waliokushambulia, according to postulates and proof ya theories mbalimbali kuwahusu wasiojulikana hao, japo malengo yao kwako, yalikuwa ni malengo fulani ambayo hayakutimia, hivyo unawasiwasi ukirejea, watakamilisha, nakuhakikishia kuwa hata ukirejea sasa bila hakikisho la IGP Sirro, wale wasiojulikana wako, hawawezi tena kuikamilisha ile kazi kwasababu kazi nyingine ni za only one try, iki fail, ndio basi tena, ni kama uchawi, mchawi ukiisha mshtukia, hakulogi tena and by now watakuwa wanashughulikiwa na kitu kinachoitwa karma, mmoja baada ya mwingine!.

Hitimisho
Kwa maoni yangu, namshauri Kamanda Tundu Lissu, kama ni kurejea tuu nyumbani, arejee tu nyumbani Tanzania wala asisubiri jibu la barua zake kwa IGP Sirro kuhusu kumhakikishia ulinzi na usalama wake, kwasababu kwanza just his survival tuu alone, muujiza beyond human beings ability and capabilities, it's a miracle from The Devine intervention hivyo Aliyemlinda na shambulio lile baya la kutisha na kusikitisha hadi kubakia hai mpaka leo, Yupo!, Aliyemsimamia matibabu akatibiwa hadi akapona Yupo!, Aliyeyafanya yote hayo ni YEYE Mwenye Uweza, awezaye yote! Namhakikishia Lissu arejee tuu nyumbani, issues za ulinzi wake na usalama wake, amwachie yule YEYE Awezaye yote!, Ataendelea kumlinda. Na usikute yote hayo Lissu aliyopitia na anayopitia, ni mapito tuu ili YEYE kuonyesha Uweza Wake kwa watu wa mataifa, na hata katika ukombozi wa Ulimwengu huu, ni kwa Kupigwa Kwake, sisi tuliponywa, hivyo at this juncture, Tundu Lissu hatakiwi tena kuendelea kutegemea uwezo wa binaadam katika ulinzi wa uhai na usalama wake, amtegemee YEYE. Tundu Lissu Atamke maneno haya, "NAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU"

Welcome Back Home, Kamanda Mdogo wangu Lissu (mimi ni kaka yake kule shuleni Ilboru)

Mwacheni Mungu Atwe Mungu
Welcome back home Kaka Mdogo Tundu Lissu.
Mimi Kaka yako Mkubwa
Karibu Nyumbani.
Paskali.
 
Kwa usalama wake, Lissu ni bora arudi baada ya Bwana yule kuondoka ofisini.

Lissu tafuta kazi huko Ulaya uwezi kuishi huko kwa muda mrefu ila usifikirie kurudi home kwa sasa.

Afrika tuna miungu watu wanaoweza kufanya maamuzi ya hovyo na bado wakabaki salama na sana sana watekelezaji wa maamuzi hayo ndio wanaoweza kuja kuingia matatani ila sio wato maamuzi unless vyama vyao vinatoka madarakani ndio na wao wanaweza kushughulikiwa.
 
Pascoo huyu ni mbunge wangu aisee usitake mje mmalize
Chamsingi siro ampe ulinzi waa askari wa 2 kwa siku

Hivi kwani kujibu barua ni vigumu au kuhakisha ulinzi ni vigumu?
Jukumu la polisi wakiongozwa na IGP ni kulinda RAIA na Mali zao
Je siro ameshindwa kazi yake?
Au pale hamna anaejua kuandika barua?
Au hawana hela ya kutuma barua kwenda Belgium?
 
Pascal Mayalla,
Una lengo zuri na wazo lako, LAKINI Usimdanganye/kumpa ujasiri mwenzako usio na SCIENTIFIC BACK UP. kUNA MSEMO, Mungu nisaidie na wewe ukijisaidia. Kama wewe unavyojisaidia kwa kuchukua tahadhali ya kutoandika ya kupinga serikali baada ya MUNGU kukunusuru na "kifungo" cha Ndugai! Hujamwachia Mungu, unajilinda kwa tahadhali kadha wa kadha!
 
Usimdanganye ! Arudi wamdungue tena ? Kumbuka hata yule Lazaro aliyefufuliwa na Yesu Kristo alikufa tena. Zaidi sana hata Mtoto Yesu Kristo alikaa uhamishoni Misri mpaka yule Herode aliyetaka kumuua alipofariki. Abaki huko huko kama anamudu gharama za maisha ya huko.
 
Hatua hii ni nzuri na muhimu ili angalau sasa Liasu na dereva wake warejee ili vyombo vyetu vya uchunguzi ndipo vianze kazi ya kuwabaini wasiojulikana
nilipofika hapa wakati nasoma hili bandiko nikajua moja kwa moja wewe upo na waliotaka kumuua lissu, na unawatetea, wewe ni mnafiki mkubwa sana hapa tanzania, huu uandishi kwa kinafiki hauna ishu nyakati hizi, hivi kwanini corona haijakuchukua!?
 
Hatua hii ni nzuri na muhimu ili angalau sasa Liasu na dereva wake warejee ili vyombo vyetu vya uchunguzi ndipo vianze kazi ya kuwabaini wasiojulikana, waliomshambulia Lissu, maana tangu ameshambuliwa vyombo vya uchunguzi vilishindwa kufanya uchaguzi wowote hadi wamhoji Lissu na dereva wake.
Thanks God, Tundu Lissu na Dereva wake walinusurika kwenye zahama ile tofauti na matarajio ya maharamia wale katili kutoka kwenye system!

So, it's interesting to know according to this government, endapo Tundu Lissu na Dereva wake wangekufa, uchunguzi usingefanyika tena!
 
Uungwana kwanza wangelimjibu barua ,hata kama sivo anavyotaka yeye Lissu, akishapata jawabu tena ataamua mwenyewe. Nafkiri Paskali unajua utaratibu wa Kuandikiwa barua hasa ya maombi.

Anaweza kuamua kurudi likitokea la kutokea hao Polisi watasema sisi hatukumjibu barua kafuata nini ilikua tunajaribu kuangalia usalama wake ukoje ili tumjibu yeye kajileta ,nafikiri ilo ndo unalolitaka litokee . Paskali inaonekana na wewe kiukweli humtakii Mtanzania mwenzetu mema
 
Back
Top Bottom