Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Kutenda KOSA si KOSA, KOSA ni kurudia KOSA
 
Jamvini (this thread)hapa kuna sala nyingi tu.
Makutano ya watu katika sala ni kanisa.
"YEYE" Kwa kutamkwa katika kanisa yamfanya muumba kufurahi. Furaha yake yabariki.
Na uhakika barua ni sala ya maombi na kama vile Paskali alivyoelezea hapo juu, basi sala hizi zimefika, kweli zimefika.
Aluta continua
 
Mmhh mungu wangu , wasiojulikana bado wanaendelea na kazi, hawajachukuliwa hatua zozote, sasa uombe ulinzi kwa aliyeshindwa kukulinda siku ile na aliyeshindwa kuwakamata wasiojulikana si utakuwa unatafuta balaa jingine. Usije ukakuta Kaka yako mkubwa huyu ana unasaba na walioshindwa
 
Jamani tusimlaumu IGP kwa kutojibu barua. Mazingira ya suala hili yanafahamika. Kwa nini IGP ajitie kitanzi kwa suala ambalo hajui mwanzo au mwisho wake? Tusubiri hadi 2026 ndo suala hili linaweza kupiga hatua. Nadhani mmenielewa.
 
Paskali unajivunjia heshima kwa bandiko lako uchwara namna hii. Waliotaka kuua Lissu wanajulikana, Pompeo pia alisaidia kumtaja hadharani na akaenda mbali zaidi kwa kumpiga STOP ya kuingia Marekani.
Kwanini unajivunjia heshima yako kwa KUBUMBA BUMBA ushahidi wako wa hovyo? Unafanya haya kwa faida ya nani mpuuzi?
 
Siandiki chochote bora nifute fute gari.
Eti kituo cha polisi ni dakika kumi tuu kufika eneo la tukio lakini walitumia masaa 2 kuwasili
 
Amen
Mtetezi yu hai
Ni yule Jana Leo na Milele
 
Kipenga cha urais kimepulizwa Chadema, kumekucha!

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Tundu Lisu: Nitagombea urais
TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maaendeleo (Chadema)-Bara, amesema atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Amesema, ataandika barua ya kuomba ridhaa ya chama chake kugombea kiti cha urais kwenye uchaguzi huo na kwamba, wakiona inafaa na kumpitisha, yupo tayari kupeperusha bendera ya chama hicho
Akizungumza na Mwanahalisi Online leo Jumatano tarehe 3 Juni 2020, lililotaka kujua kama anao mpango wa kugombea urais ndani ya chama chake.
“Nilikuwa nasubiri baraza za chama, nitaandika barua ya kuomba ridhaa ya chama changu nigombee urais,” amesema Lissu
Mapema leo Jumatano, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ametangaza kufunguliwa kwa milango kwa wanachama wa chama hicho, wanaotaka kuwania urais kuandika barua kwa katibu mkuu.
Mnyika amesema, milango hiyo imefunguliwa kuanzia leo hadi tarehe 15 Juni 2020 kisha baada ya hapo, watakaokuwa wamejitokeza watapelekwa kamati kuu ya chama hicho kwa hatua zaidi za ndani.
Baada ya tangazo hilo la Mnyika, MwanaHALISI ONLINE limezungumza na Lissu kwa simu akiwa nchini Ubelgiji ambaye amesema, “kama mwanachama mtiifu wa Chadema, nilikuwa nasubiri uongozi wa chama unaohusika, utoe baraka zake kwa wanachama kuanza mchakato wa uchaguzi.”

Mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki amesema, “kwa vile hizo baraka zimekwisha kutolewa na kwa vile nimekuwa natajwa tajwa na najitaja taja, basi nitafanya kitu ambacho nimekuwa nakisemasema.”

Lissu ambaye amewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesema, “nitamwandikia barua rasmi katibu mkuu wa chama ili kutoa tangazo rasmi kwake.”
“Na vilevile, nitazungumza na umma wa Watanzania na wengine wanaotutakia mema baada ya kuwa nimetangaza nia rasmi na kwa uchache, maswala muhimu ninayoyaona katika uchaguzi huu kwenda mbele,” amesema.

Katika kusisitiza hilo, Lissu amesema, “Nafikiri nitafanya hivyo ndani ya muda huu ambao umetolewa na chama wa kufanya hivyo na kwa vyovyote vile sitawachelewesha.”

Akijibu swali aliloulizwa na MwanaHALISI ONLINE anarejea lini nchini, Lissu amesema, “suala la kurejea nchi linashughurikiwa na wakati mwafaka utakapofika wananchi watapata taarifa.”
Amesema, sheria za Tanzania hazijazungumzia mtu akiwa nje ya nchi hiyo kwa kipindi fulani hatoweza kugombea hivyo hana wasiwasi na hilo.
“Kama nitakuwa mgombea urais kwa niaba ya chama lazima nitakuja Tanzania,” amesema
Lissu amekuwa nje ya Tanzania tangu tarehe 7 Septemba 2017, aliposafirishwa kwenda Hospitali ya Nairobi, Kenya kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 nje ya makazi yake Area D jijini Dodoma.

Mwanasiasa huyo alifikwa na mkasa huo, akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge lililokuwa likiendelea jijini humo.

Alipata matibabu Nairobi hadi tarehe 6 Januari 2018 alipohamishiwa Ubelgiji aliko mpaka sasa kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, Lissu amekwisha kusema, amepona na anachosubiri ni kuhakikishiwa mazingira salama ya maisha yake ili yasije kujitokeza kama yaliyomkuta awali.
Source: Mwanahalisi online.
My Take
Tunamsubiria huyu mwamba arejee.
P.
 
Bwana Paskali nataka kukuhakikishia kuwa
kwa mwandishi kama wewe unapaswa kutumia kalamu yako kuelemisha jamii,badala ya kutia jamii hofu.
Mkuu Nanyaro, karibu mitaa hii, au na hapa ni kuwatia watu hofu?.
P.
 
Elections 2020 - Please CHADEMA, mtapata mnachokitafuta
Naunga mkono hoja kuhusu ndio the best man wa kum challenge rais Magufuli kwasababu Lissu ni zaidi ya Magufuli katika... kama nilivyoeleza hapa
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

However, I'd like to differ kwenye Lissu kumshinda Magufuli!. Lissu will only challenge but not to win but just to challenge na sio kumwangusha Magufuli kwasababu...

Ila hili wimbi la watia nia wa Chadema hadi Mbowe, tells me kuwa Lissu ni Just a Pacemaker and not a contender kwasababu ana mlolongo wa kesi za jinai, hivyo hii hoja yangu kumhusu Lissu na kurejea kwake, kwangu is still valid
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!
Usikute wanamngoja kwa hamu!, Lissu anajua!, Chadema wanajua,... wanamsubiri arudi, watasubiri sana!.

Hivyo bandiko hili litaendelea kusimama mpaka siku Lissu ame touch down

P
 
Mkuu Ngongo, kwanza naunga mkono hoja ya presidential candidature ya Tundu Lissu kwasababu ni presidential material, hata mimi nilishauri
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Ila baada ya kuanza kufunguka funguka huko Ughaibuni, niliingia mashaka kama atarejea home
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Tundu Lissu akatoa conditions to be met kabla ya kurejea, na mimi nikashauri
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Na alipoamua kugombea kutokea Ughaibuni nika comment
Elections 2020 - Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Na mwisho nikawatajia mgombea urais wa Chadema, sio Lissu!.

Elections 2020 - Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge...

P
 
Wanabodi, mimi nilidhani Lissu hatarejea
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

I wish him all the best.
Paskali
 

Kuna watu nimewaambia wafungue macho: inawezekana kabisa migogoro, malumbano, minyukano n.k ikiwamo fujo katika medani za kisiasa zikaepukwa pale walio pande zote za sheria wanapotii na kufanya mambo yao in a civilised manner. A balanced approach from the enforcer as well as from the enforcee. Tuheshimiane na kulindana. Hakuna aliye juu ya sheria zinazoongoza nchi. Tutimize wajibu wetu kiweledi na responsibly. Rogue elements sio wengi.
Sipendi nchi yangu pendwa itumbukie kwenye jamhuri ya midizi.

Thx uncle P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…