Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne, amesema mbali na Mabasi ya Mwendokasi na Vituo vinne vya Mabasi hayo kupigwa mawe usiku wa jana, baadhi ya Wananchi hao walifanya fujo katika Vituo viwili vya Polisi ambavyo ni Kituo cha Polisi Magomeni Usalama na Kituo cha Polisi Magomeni Kagera.
Soma: Magomeni: Vurugu zazuka, ofisi ya mabasi ya mwendo kasi yavamiwa na kupelekea kuvunjwa vioo
Kamanda Muliro amenukuliwa akieleza yafuatayo
"Kuna fujo zilitokea pale Gerezani na ikaja ikatokea Magomeni Mapipa, Usalama na Kagera kuna gari ilichelewa pale Gerezani kuna Watu wakafanya fujo pale kwa kulishambulia, baadae kuna gari lilikuja pale Mapipa likapata hitilafu Abiria wakashuka na baadhi ya Abiria wakachukua mawe wakaharibu lile gari kwenye baadhi ya vioo"
"Kazi yetu kuhakikisha usalama unaimarika, mpaka sasa kuna Watu tunawahoji ambao inadaiwa walikuwa sehemu ya vurumai, pia baadhi walifanya fujo maeneo ya Kituo cha Polisi cha Usalama na pale Kagera baadhi ya magari yakaharibiwa vioo vyake na baadhi ya Vituo vikapata madhara ya fujo zile" - Muliro.
"Polisi walifika na kudhibiti hali ile maeneo ya Kagera sababu mabasi yalikuwa yanapandisha Ubungo mpaka Kimara, hali ile ilithibitiwa na kusema kweli pamoja na sababu mbalimbali zilizokuwa zinaelezwa lakini suala la kuharibu miundombinu ya usafiri ni kosa kisheria hata ukitoa sababu mbalimbali, maeneo ya Kagera lile kundi tulilazimika kuhakikisha kwamba wanajua Polisi amefika pale wakatawanyika pale wakakimbilia maeneo Mburahati"