Kamanda Muliro: Watatu wakamatwa kwa kuharibu Mabasi ya Mwendokasi, wengine wasakwa katika fujo Magomeni

Kamanda Muliro: Watatu wakamatwa kwa kuharibu Mabasi ya Mwendokasi, wengine wasakwa katika fujo Magomeni

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne, amesema mbali na Mabasi ya Mwendokasi na Vituo vinne vya Mabasi hayo kupigwa mawe usiku wa jana, baadhi ya Wananchi hao walifanya fujo katika Vituo viwili vya Polisi ambavyo ni Kituo cha Polisi Magomeni Usalama na Kituo cha Polisi Magomeni Kagera.
View attachment 3482176
Soma: Magomeni: Vurugu zazuka, ofisi ya mabasi ya mwendo kasi yavamiwa na kupelekea kuvunjwa vioo

Kamanda Muliro amenukuliwa akieleza yafuatayo

"Kuna fujo zilitokea pale Gerezani na ikaja ikatokea Magomeni Mapipa, Usalama na Kagera kuna gari ilichelewa pale Gerezani kuna Watu wakafanya fujo pale kwa kulishambulia, baadae kuna gari lilikuja pale Mapipa likapata hitilafu Abiria wakashuka na baadhi ya Abiria wakachukua mawe wakaharibu lile gari kwenye baadhi ya vioo"

"Kazi yetu kuhakikisha usalama unaimarika, mpaka sasa kuna Watu tunawahoji ambao inadaiwa walikuwa sehemu ya vurumai, pia baadhi walifanya fujo maeneo ya Kituo cha Polisi cha Usalama na pale Kagera baadhi ya magari yakaharibiwa vioo vyake na baadhi ya Vituo vikapata madhara ya fujo zile" - Muliro.

"Polisi walifika na kudhibiti hali ile maeneo ya Kagera sababu mabasi yalikuwa yanapandisha Ubungo mpaka Kimara, hali ile ilithibitiwa na kusema kweli pamoja na sababu mbalimbali zilizokuwa zinaelezwa lakini suala la kuharibu miundombinu ya usafiri ni kosa kisheria hata ukitoa sababu mbalimbali, maeneo ya Kagera lile kundi tulilazimika kuhakikisha kwamba wanajua Polisi amefika pale wakatawanyika pale wakakimbilia maeneo Mburahati"

View attachment 3482178
Hongereni vijana kwa kujitoa wahanga kwaajili ya Wengi hata familia za polisi zitafurahia kuingizwa kwa mabus mapya leo...wao na sisi letu moja.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne, amesema mbali na Mabasi ya Mwendokasi na Vituo vinne vya Mabasi hayo kupigwa mawe usiku wa jana, baadhi ya Wananchi hao walifanya fujo katika Vituo viwili vya Polisi ambavyo ni Kituo cha Polisi Magomeni Usalama na Kituo cha Polisi Magomeni Kagera.

Kamanda Muliro amenukuliwa akieleza yafuatayo "Inadaiwa baadhi walifanya fujo kwenye maeneo yale ya Kituo cha Polisi cha Usalama pale na Kagera na kwenye fujo hizo baadhi ya magari yaliharibiwa vioo vyake lakini pia baadhi ya Vituo vile vya eneo lile vilipata madhara ya fujo zile"

"Kwahiyo Polisi walifika na kuweza kudhibiti hali ile pale Maeneo ya Kagera kwasababu Mabasi yalikua yanapandisha kuja Ubungo mpaka kule Kimara, kusema ukweli pamoja na sababu nyingine mbalimbali ambazo zimekuwa zikielezwa lakini swala la kuharibu miundombinu hii ya usafiri ni kosa kisheria kwahiyo hata ukitoa sababu nyingine mbalimbali sisi Wasimamizi wa sheria tunaangalia usalama unaimarika namna gani, kama kuna jambo lolote zipo taratibu zinatakiwa kufuatwa" - Kamanda Muliro
1759389203273.jpg
 
Muliro ni mwendo wa kutoa milio tu, bado Oktoba 29 atatafuta pa kutolea mwangwi...
 
Back
Top Bottom