Uchaguzi 2020 Kamanda Sirro: Vyama kulinda kura ni kosa la jinai

Uchaguzi 2020 Kamanda Sirro: Vyama kulinda kura ni kosa la jinai

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tokea katika mkutano ulioshirikisha wadau wengine wa uchaguzi Dar, kamanda Sirro amenukuliwa akisema vyama kulinda kura ni kosa la jinai.

Kwa mujibu wa kamanda huyu kazi ya kulinda kura ni kazi ya polisi peke yao.

Kwa nini kamanda Sirro haoni umuhimu wa wenye mali yaani yenye kura zao kujiridhisha kuwa ziko salama?

Kwa nini kamanda Sirro haoni kuwa vitimbi vya polisi dhidi ya vyama vya upinzani vinawafanya kutoaminika?

Rejea vitimbi vya polisi wa Mbeya dhidi ya Sugu. Rejea matamshi ya bashiri kuhusiana na matumizi ya vyombo vya dola ili kubakia madarakani.

Kamanda Sirro kwanini haoni umuhimu wa utaratibu wa wazi kwa vyama kujiridhisha kuhusiana usalama wa kura, ni kigezo muhimu kuonyesha kuwa haki imetendendeka kwa mustakabala mzuri wa amani yetu sote?

Ni kweli kuwa kamanda Sirro anategemea kwa dhati kabisa kuwa polisi wake katika mazingira haya watatenda haki?

IMG_20200820_093436_378.jpg

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Nawasilisha.
 
Tokea katika mkutano ulioshirikisha wadau wengine wa uchaguzi Dar, kamanda Sirro amenukuliwa akisema vyama kulinda kura ni kosa la jinai.

Kwa mujibu wa kamanda huyu kazi ya kulinda kura ni kazi ya polisi peke yao.
Muda bado, vyama vya upinzani vitatatikiwa kuhitaji tume huru na maelewano baina ya polisi na nyama upinzani ni lazima uwe bayana ili kuepusha watu kuleta vurugu.

Sent from my SM-A605FN using JamiiForums mobile app
 
Unaishi sehemu gani isiyo kuwa na utaratibu? Kama uwakilishi usingekuwa na umuhimu basi hata bunge lisingekuwa na maana kwani tungeenda watanzania wote Dodoma ili kutunga na kupitisha sheria.

Unadhani Watanzania wote tukienda kulinda kura humo ndani kura zinapohesabiwa kutatosha.

Kuwa mpinzani sio tiketi ya kujitoa ufahamu
 
Tokea katika mkutano ulioshirikisha wadau wengine wa uchaguzi Dar, kamanda Sirro amenukuliwa akisema vyama kulinda kura ni kosa la jinai.

Kwa mujibu wa kamanda huyu kazi ya kulinda kura ni kazi ya polisi peke yao...
Mwambie Sirro aache kujidhalilisha. Kama vile ambavyo hakuna sheria inayosema polisi ndio watalinda kura basi mwaka huu wananchi tutalinda kura zetu zote.

Na hii ndo hoja kuu kwa mwaka huu. Wananchi tutalinda kura zetu!!! Full stop
 
Tupe utaratibu unaoruhusu vyama kulinda kura.
 
Polisi wangekuwa na rekodi nzuri wangeaminiwa kwenye hilo suala, tatizo polisi wetu nao wameonekana ni wapenzi na mashabiki wa CCM, sasa nani atawaamini wakisema watalinda kura kwenye uchaguzi unaohusisha wapinzani?!

Zaidi Sirro anaetoa matamko yanayoonekana kukipendelea chama tawala kila wakati ataaminiwa vipi kwenye hili?

Ni wajibu wake kuviaminisha vyama vya upinzani kwamba polisi watakuwa fair kutenda haki sawa kwa vyama vyote, lakini sio kwa kauli tu, anatakiwa kuonesha kwa vitendo, akianza kwa kubadili aina za kauli zake anazozitoa kila wakati zinazoonekana kukipendelea chama tawala.
 
Mwambie Sirro aache kujidhalilisha. Kama vile ambavyo hakuna sheria inayosema polisi ndio watalinda kura basi mwaka huu wananchi tutalinda kura zetu zote.
Na hii ndo hoja kuu kwa mwaka huu. Wananchi tutalinda kura zetu!!! Full stop

Sheria ya kukaa mita 200 bado ipo
 
Hao polisi hatukuwachagua sisi wananchi kuwa walinzi wa kura zetu.

Unatoa mfano wa wabunge na polisi.

Jiulize lini wewe ulipiga kura kumchagua polisi awe mlinzi wa kura zako?

Ni sawa kufananisha usiku na mchana.

Sisi tutalinda kura zetu wenyewe na kama yeye IGP anasema ni jinai basi mahakama itaamua.Yeye sio mahakama.
Unaishi sehemu gani isiyo kuwa na utaratibu?? Kama uwakilishi usingekuwa na umuhimu basi hata bunge lisingekuwa na maana kwani tungeenda watanzania wote dodoma ili kutunga na kupitisha sheria.

Unadhani watanzania wote tukienda kulinda kura humo ndani kura zinapohesabiwa kutatosha.

Kuwa mpinzani sio tiketi ya kujitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom