Tokea katika mkutano ulioshirikisha wadau wengine wa uchaguzi Dar, kamanda Sirro amenukuliwa akisema vyama kulinda kura ni kosa la jinai.
Kwa mujibu wa kamanda huyu kazi ya kulinda kura ni kazi ya polisi peke yao.
Kwa nini kamanda Sirro haoni umuhimu wa wenye mali yaani yenye kura zao kujiridhisha kuwa ziko salama?
Kwa nini kamanda Sirro haoni kuwa vitimbi vya polisi dhidi ya vyama vya upinzani vinawafanya kutoaminika?
Rejea vitimbi vya polisi wa Mbeya dhidi ya Sugu. Rejea matamshi ya bashiri kuhusiana na matumizi ya vyombo vya dola ili kubakia madarakani.
Kamanda Sirro kwanini haoni umuhimu wa utaratibu wa wazi kwa vyama kujiridhisha kuhusiana usalama wa kura, ni kigezo muhimu kuonyesha kuwa haki imetendendeka kwa mustakabala mzuri wa amani yetu sote?
Ni kweli kuwa kamanda Sirro anategemea kwa dhati kabisa kuwa polisi wake katika mazingira haya watatenda haki?
Muda bado, vyama vya upinzani vitatatikiwa kuhitaji tume huru na maelewano baina ya polisi na nyama upinzani ni lazima uwe bayana ili kuepusha watu kuleta vurugu.
Unaishi sehemu gani isiyo kuwa na utaratibu? Kama uwakilishi usingekuwa na umuhimu basi hata bunge lisingekuwa na maana kwani tungeenda watanzania wote Dodoma ili kutunga na kupitisha sheria.
Unadhani Watanzania wote tukienda kulinda kura humo ndani kura zinapohesabiwa kutatosha.
Mwambie Sirro aache kujidhalilisha. Kama vile ambavyo hakuna sheria inayosema polisi ndio watalinda kura basi mwaka huu wananchi tutalinda kura zetu zote.
Na hii ndo hoja kuu kwa mwaka huu. Wananchi tutalinda kura zetu!!! Full stop
hata wale wawakilishi wa vyama hawatakiwi au?
kamanda Sirro kumbuka kuwa; wapinzani hawawezi kuwa na imani nanyi kwani mmetumika mara nyingi sana kukandamiza upinzani.
Nazani inaruhusiwa kukaa kama mita mia mbili kukizingira kitua cha kura polisi wasije wakatoka na kukimbia na masanduku ya kura kama walivyofanya Pemba.
Polisi wangekuwa na rekodi nzuri wangeaminiwa kwenye hilo suala, tatizo polisi wetu nao wameonekana ni wapenzi na mashabiki wa CCM, sasa nani atawaamini wakisema watalinda kura kwenye uchaguzi unaohusisha wapinzani?!
Zaidi Sirro anaetoa matamko yanayoonekana kukipendelea chama tawala kila wakati ataaminiwa vipi kwenye hili?
Ni wajibu wake kuviaminisha vyama vya upinzani kwamba polisi watakuwa fair kutenda haki sawa kwa vyama vyote, lakini sio kwa kauli tu, anatakiwa kuonesha kwa vitendo, akianza kwa kubadili aina za kauli zake anazozitoa kila wakati zinazoonekana kukipendelea chama tawala.
Mwambie Sirro aache kujidhalilisha. Kama vile ambavyo hakuna sheria inayosema polisi ndio watalinda kura basi mwaka huu wananchi tutalinda kura zetu zote.
Na hii ndo hoja kuu kwa mwaka huu. Wananchi tutalinda kura zetu!!! Full stop
Unaishi sehemu gani isiyo kuwa na utaratibu?? Kama uwakilishi usingekuwa na umuhimu basi hata bunge lisingekuwa na maana kwani tungeenda watanzania wote dodoma ili kutunga na kupitisha sheria.
Unadhani watanzania wote tukienda kulinda kura humo ndani kura zinapohesabiwa kutatosha.