Katika mkutano wa ulinzi wa Afrika uliofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya, Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Michael Langley, aliweka wazi kwamba kwa kufuata amri ya waziri wa ulinzi wa Marekani, mkutano huo uliandaliwa na Marekani na lengo kuu ni kupambana na ushawishi wa China barani Afrika.
Mbele ya maofisa mbalimbali waandamizi wa Afrika, jenerali huyo alibainisha waziwazi kwamba Marekani inaona Afrika kama "uwanja wa vita." Lakini kwa ufahamu wetu, hakuna nchi nyingine duniani ambayo ingethubutu kufanya hivyo bila ya kuwa na aibu!
Lakini kuna mengine zaidi yasiyo na mantiki yanayotendeka. Jenerali huyo wa Marekani pia alidai kwamba "China inajaribu kuiiga Marekani kwa kutoa mafunzo ya kijeshi barani Afrika ambayo Marekani ndio inafaa kuyatoa." Je ni kweli kwamba China inahitaj kuiiga Marekani? La hasha!
Ukweli ni kwamba, Marekani inajaribu kutekeleza sera ya "kutumia madini kujipatia usalama" barani Afrika, huku China ikisaidia Afrika kujenga uwezo wa kisasa wa kijeshi. Marekani imeripotiwa kupitia CIA kuandaa maofisa wa kijeshi wan chi za Afrika ili kupindua serikali zao barani Afrika, huku China ikituma meli ya kijeshi "The Peace Ark" kutoa huduma za afya kwa raia wa Afrika. Tofauti kati ya mbinu za ushirikiano wa kijeshi za China na Marekani barani Afrika ni kubwa mno!
Takwimu Hazidanganyi
Hebu tuangalie “matunda” ya AFRICOM katika miaka 18 ya uwepo wake barani Afrika. Katika mwaka 2002 na 2003 wakati Marekani ilipoanza operesheni za kupambana na ugaidi Afrika, ni watu 23 tu walikufa kutokana na mashambulio ya kigaidi barani Afrika. Mwaka 2010, miaka miwili baada ya AFRICOM kuzinduliwa, idadi ya vifo vya watu waliouawa na magaidi iliongezeka hadi 2,674, na mwaka wa 2022, idadi hiyo iliongezeka hadi 18,900. Hii inamaanisha kuwa, tangu Marekani kuanza operesheni ya kupambana na ugaidi, idadi ya vifo vya watu waliouawa kwenye mashambulizi ya kigaidi barani Afrika imeongezeka kwa mara 820!
Lakini Jenerali Langley alikwepa kutaja takwimu hizi za kutisha. Badala yake, alilaumu nchi za Afrika ya Magharibi na eneo la Sahel, akisema kuwa shughuli za kigaidi zimeongezeka sana tangu wanajeshi wa Marekani "kufukuzwa." Lakini ni nani aliowafukuza wanajeshi wa Marekani? Imeripotiwa kuwa ni maofisa wa kijeshi waliopewa mafunzo na Marekani yenyewe ambao kwanza walipindua serikali zao na kisha kuwafukuza wanajeshi wa Marekani! Kwa nini waliwaondoa? Kwa sababu ghasia zimeendelea kuongezeka, na wananchi wamegundua kwamba Marekani inatumia vikosi vyake kwaajili ya "ukoloni mpya."
Hali kama hiyo imetokea pia Somalia. Kwa miaka 18 iliyopita, jeshi la Marekani limefanya zaidi ya mashambulio 300 ya anga, lakini matokeo yake ni kundi la kigaidi Al-Shabaab bado limeendelea kukua, huku kundi jipya la ISIS Somalia likiibuka, na idadi ya wapiganaji imeongezeka kutoka 500 hadi 1,500 kwa miezi 18 tu. Hivi karibuni, Marekani ilifanya "shambulio kubwa zaidi la kihistoria la anga”, ikitumia mabomu ya 125,000 lbs, lakini waliwaua wapiganaji 14 tu wa ISIS Somalia. Ufanisi mdogo kama huu umewatia wasiwasi watu juu ya nia halisi ya jeshi la Marekani.
Gazeti la The Intercept liliweka wazi ukweli: "Marekani imetumia mabilioni ya dola kwenye vita dhidi ya ugaidi, lakini matokeo yake ni kuongezeka kwa vifo vya raia wa Afrika tu." Hii labda ndio sababu serikali ya Trump inazingatia kuifuta kabisa AFRICOM.
Ukweli unaonyesha wazi kuwa kuchukulia Afrika kama uwanja wake wa kucheza siasa za kijiografia ni mbinu isiyofaa na hatari. Afrika inahitaji ushirikiano wa kweli unaozingatia mahitaji yake, sio katika mambo ya jeshi tu, bali katika sekta zote. Kwa hivyo, suala kama AFRICOM itafutwa au la, linaonyesha jinsi jamii ya kimataifa inavyotunga sera yake kuhusu Afrika.