Heshima kwako Njowepo,
Wapo watu wengi sana waliowahi kudanganya uraia wa Tanzania na kufaidi matunda ya uraia kama watanzania wengine.Juzi juzi nadhani maeneo ya Kibaha wamegunduliwa waalimu wawili wa kiganda waliokuwa na vyeti vya kuzaliwa na kadi za kupigia kura za Tanzania.System ya uraia Tanzania iko hovyo sana kiasi kwamba inakuwa ni rais mgeni kukaa Tanzania na kudai yeye ni raia.
Serekali ya Tanzania inatakiwa kumfukuza Bashe nchini kwa kosa la kuishi na kufanyakazi Tanzania bila kufuata taratibu na sheria za nchi.Kwakuwa Somalia sasa hivi hakukaliki Bwana bashe anatakiwa kupelekwa kwenye kambi za wakimbizi ili shirika la wakimbizi UNCHR limuhudumie kama linavyofanya kwa wakimbizi wengine.
Ushindi wa Bashe unatokana na mtandao wa wasomali [watekaji wa meli] waliozagaa Tanzania ambao wanamkakati wa kupachika watu wao kwenye nafasi za kisiasa ili kulinda maslahi yao.Tayari wasomali wamefanikiwa kufanya hivyo nchini kenya kiasi kwamba kundi la Al shabab kutokea Kenya limeweza kufanya ugaidi Uganda bila kipingamizi.Tayari wasomali wanamiliki vituo vingi vya mafuta na mahoteli nchini Tanzania kwa maneno mengine wamefanikiwa kukamata uchumi kilichobaki kwao ni madaraka.Baadhi ya watu bila kujua wanashangaa ushindi mkubwa wa Bashe dhidi ya mpiganaji Seleli lakini wanshindwa kujua nguvu ya fedha iliyotumika tena mbele ya TAKUKURU.Umoja wa wasomali kwa kutumia nguvu ya fedha wameweza kuwazuia UWT / TAKUKURU kufanya kazi yao,bila shaka Muungwana alipewa taarifa yote ndio maana kaamua kumwondoa Bashe.