Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

Jamani eeh,

Hivi CCM ikipitisha mgombea ambaye ana utata wa Uraia, hamwoni kwamba atapingwa na vyama vingine... are guys thinking really?
 
Ndugu wawili wanapogombana, wewe chukua jembe ukalime. Watakapopatana watakukuta wewe tayari unavuna wakati wao hawana cha kuvuna, ndipo watatambua ujinga wao.
Ahlan wasahlan Kichuguu hapo umenena. JF imevamiwa na wanasisiem, wananung'unika ile mbaya, oh huyu mbona kakatwa ah mbona yule kabaki. Wanamageuzi wamebaki roho kwatuuuuuuuuuu!
Waacheni bwanaaaaaa wakimaliza kutaja majina yao, tutachagua hata maruhani. yangu macho
 
Mmmhhh hii ndio sia bwana ukimalizia utajua mwenyewe
kwa kweli naanza kwa kukupa pole kijana najua umewekeza sana na vijisenti vingi vikiwepo vya mzee wetu rostam lakini yawezekana mungu akukupenda zaidi,,,pole sana mengi yataongelewa ila jifikirie sana yale mambo uliokuwa ukikwaruzana na riziwani na beno
wengi walisoma mbele na wabaya wako uko nao hapo hapo walijua mcheezo unaoenda kuchezwa ingawa ulijisahau na kuamini mzee wako rostam ndio mwisho wa matatizo bila kujua kuna nweeeeeeeeeeeeeeeccccccccccccc,,,nakupa pole ukitaka kuishi maisha ya amani ccm funga mdomo angalia kama una akili zako timamu wote wasioongea bungeni ndio waliorudishwa ,..kuna wenye miaka 20 hata kumwambia spika habari zako kwenye kipaza sauti ndio wanendelea kupeta siasa ni mchezo wa kichaa ....najua hapo mbele utaangalia chama chenye msaada ila usikurupuke kukimbia ccm watakumaliza tena kwa 24hrs airport...ukimalizana na swala la uraia washa moto utakavyo
 
Hussein Bashe siyo RAIA - hayo mengine ni mengineyo!

Uraia wake umekuwa ukijadiliwa kwenye "circles" nyingi na hata ule mkutano wa Iringa - but it seems yeye alimtegemea sana Rostum kuliko ukweli wenyewe!
 
Ina maana Bashe hizi fununu alizinasa na bado akamtgemeaa zaidii RA??? Kumbe aliyepeleka malalamiko ya uraia wa Bashe ni mgombea wa nzega Kupitia Kwa Rizwan Jakaya Kikwete. Nasikia file lilimfikiaa muungwana wakiwa faragha na Riz na mkuu akamhakikishia mwanae ujumbe umefika na huyo Bashe CCM ataisikiaaa......
 
Ridhwani Kikwete hasa baada ya uchaguzi wa makamo mwenyekiti wa UVCCM Taifa ambapo bwana Bashe alishiriki na Swahiba wa Ridhwani Bwana Beno Malisa..!!

Je CCM inatufunza nini? na Tunakwenda wapi..?


Napenda toa tangulizo kwa Ridhwani Kikwete
kama aliwekwa kwenye kampeni za baba yake kuja kuichafua siasa asije akategemea chochote 2015 hiyo imekula kwake ni bora asingeliingia kwani anajipalia mkaaa mapema na wakati huo in 2015 asije tegemea kutakuwa na mtu au watu wa kumbeba democrasia na siasa za kipindi hicho itakuwa tofauti kabisa,

kaenda mwanza akambeba Masha na akashirikiana na watu wa maswa kumng'oa Shibuda sasa kama ameisha anzisaha uhasa nadni ya UVCCM inakula kwake mazima anajichimbia kaburi muda si mrefu.

Na tatizo kubwa humu ndani ya siasa za CCM ni kuwa watu waliomo humo au wafuasi wengi wa CCM wanasumbuliwa na njaaa njaaaa za vijisenti vya hapa na pale wansea utaniachaje kila ukienda na kutoka utaniachaje njaaaa zitatumaliza humo CCM nawambieni na hicho ndicho chanzo cha kufikia mahali mbunge atakuambia mtanifanya nini kwa si nilinunua ubunge maana kila akija nadi sera zake au kuwa na vikao vidogo vidogo na wajumbe kadhaa wa CCM wanajua kuna kuganga njaaa na kweli wanapewa kumbe ndiko kununua uongozi, sasa sielewi Ridhwani anataka nini? nikuweka misingi bor ya siasa safi au kuchafua kabisa na kuweka tabaka la watu fulani baba aweze kuongoza vyema??
 


Yana mwisho.
 

Kweli hata mie hapa nashindwa kuelewa, kama mtu kazaliwa Tanzania yeye ni raia wa wapi? Tunajua wazi kuwa Tanzania bado haijaruhusu Dual Citizenship, kama kazaliwa Tanzania na ana cheti cha kuzaliwa kilichothibitihwa na mamlaka husika then mnatakiwa kumwomba samahani huyo Bashe.

Najua yuko karibu na RA but I don't care kwenye hii issue ya URAIA. Kama kazaliwa Tanzania Bashe ana haki ya kimsingi kabisa kuwa Mtanzania.
 

Wakuu hili suala la Bashe tuliangalie kwa mapana zaidi hivi nchi hii ni ya kifalme? ina maana ukikosana na mtoto wa rais mambo yako yanaharibika? nimesikia hata Ridhwan akienda mikoani wakuu wa mikoa na wilaya wanamnyenyekea.Ukichanganya na mama Salma kupokea taarifa kutoka kwa watumishi wa serikali katika ziara zake tusipoangalia taratibu tutaanzisha utawala wa kiimla TAFAKARI CHUKUA HATUA OCTOBER 2010!
 

Hilo nalo neno dada hata Royal family ilianza hivi hivi itafata watu kufukuzwa kazi kwa barua za kutoka kwa Mama Salma n a Riz.
 
wanasema "waache wafu, wawazike wafu wao".. na msemo wangu ni kuwa "ukikuta samaki wanakaangana, wewe jiandae kula"
 
 
Jana ametoa vithibitisho kuwa aliukana Usomalia toka 2008 na kuwa hakuitwa kujitetea na hana taarifa rasmi kuwa katolewa.....yeye kayasikia kwenye magazeti tu....kazi ipo
 
Jamni nisaidieni hapa..Mnasema huyo dogo alikuwaga na mavyeo mengi,sasa hakuwahi ata kutoka nje? ata kwenda kwenye vikao vya vyama vingine kama vile ANC.Kama ni hivyo alikuwa anatumia documents gani
 

Mkuu
Kwanini akosane na mtoto wa rais? Huoni huo ni utovu mkubwa wa nidhamu? Mtoto wa rais ni mtu mkubwa sana. Kwa usalama wa taifa lolote inafaa aheshimiwe. Kila anachotaka kufanya hairuhusiwi kumpinga. Wana JF tusipokuwa makini itafikia mahali watu watatulisha maneno ya uchonganishi kiasi siku ukimkuta mke wako akanavinjari na mtoto wa rais uanze kumkasirikia. Hii itakuwa ni mbaya sana kwa mustakabadhi wa taifa letu. Mtoto wa rais popote duani anaruhusiwa kufanya lolote bila kuhojiwa na wala watu kukasirika. Mfano mzuri ni Libya au Iraq kabla ya USA kuingia. Hizo ndio heshima wanazotakiwa kupewa watoto wa marais. Nashukuru kuona Watanzania na sisi tumeanza kuamka kwani nimesikia hata uchaguzi wa Yanga alikuwepo. Hii inatupa matumaini kwni tunaanza konyesha heshima anayostahili kupewa.
 
Jadili.

Leo tumepewa assignment na lecturer wetu, na swali la kwanza akatuuliza kauli ya Makamba aliyoitoa jana. Naomba hints zenu tafadhali.
 

Kumbe!
 
Kuna habari kuwa Hussein Bashe ataongea na waandishi leo..! Je kasema nini...? Vilevile mliopo kwenye press conference hiyo mnaweza kumuuliza kuhusu ripoti hizi mbili zinazotatanisha..

1. Akihojiwa na BBC swahili alisema kuwa yeye ni raia kwakua mama yake ni mtanzania (si msomali) na baba yake ndie msomali kwahivyo amerithi uraia wa mzazi mmoja wapo (mama yake) ambaye ni mtanzania na hana haja ya kuukana uraia wa baba.

2. Gazeti la leo la Mwananchi linadai alishaukana uraia wa Somalia kwenye mahakama ya kivukoni.

Lipi kweli kati ya haya mawili?
 
Sasa huyu anaongea nini tena wakati sisiem hawamtaki .Uhamiaji wameshasema
kuwa yeye ni raia ila makamba amesema uhamiaji hawajui kitu.Ukibishana na
mjinga na wewe utakuwa mjinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…