Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ahlan wasahlan Kichuguu hapo umenena. JF imevamiwa na wanasisiem, wananung'unika ile mbaya, oh huyu mbona kakatwa ah mbona yule kabaki. Wanamageuzi wamebaki roho kwatuuuuuuuuuu!Ndugu wawili wanapogombana, wewe chukua jembe ukalime. Watakapopatana watakukuta wewe tayari unavuna wakati wao hawana cha kuvuna, ndipo watatambua ujinga wao.
..Lakini tukirudi nyuma huyu bwana bashe ,NI MJUMBE WA BARAZA KUU UMOJA WA VIJANA TAIFA (UVCCM),NI MJUMBE MKUTANO MKUU WA CCM MKOA TABORA,AMEWAHI KUGOMBEA NAFASI YA NEC UVCCM TAIFA na AMEWAHI KUGOMBEA MAKAMO MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA. ILa kwa mbali kuna fununu kwamba huyu Bwana Bashe hana mahusiano mazuri na mtoto wa MH.Rais
Ridhwani Kikwete hasa baada ya uchaguzi wa makamo mwenyekiti wa UVCCM Taifa ambapo bwana Bashe alishiriki na Swahiba wa Ridhwani Bwana Beno Malisa..!!
Je CCM inatufunza nini? na Tunakwenda wapi..?
Napenda toa tangulizo kwa Ridhwani Kikwete
kama aliwekwa kwenye kampeni za baba yake kuja kuichafua siasa asije akategemea chochote 2015 hiyo imekula kwake ni bora asingeliingia kwani anajipalia mkaaa mapema na wakati huo in 2015 asije tegemea kutakuwa na mtu au watu wa kumbeba democrasia na siasa za kipindi hicho itakuwa tofauti kabisa,
kaenda mwanza akambeba Masha na akashirikiana na watu wa maswa kumng'oa Shibuda sasa kama ameisha anzisaha uhasa nadni ya UVCCM inakula kwake mazima anajichimbia kaburi muda si mrefu.
Na tatizo kubwa humu ndani ya siasa za CCM ni kuwa watu waliomo humo au wafuasi wengi wa CCM wanasumbuliwa na njaaa njaaaa za vijisenti vya hapa na pale wansea utaniachaje kila ukienda na kutoka utaniachaje njaaaa zitatumaliza humo CCM nawambieni na hicho ndicho chanzo cha kufikia mahali mbunge atakuambia mtanifanya nini kwa si nilinunua ubunge maana kila akija nadi sera zake au kuwa na vikao vidogo vidogo na wajumbe kadhaa wa CCM wanajua kuna kuganga njaaa na kweli wanapewa kumbe ndiko kununua uongozi, sasa sielewi Ridhwani anataka nini? nikuweka misingi bor ya siasa safi au kuchafua kabisa na kuweka tabaka la watu fulani baba aweze kuongoza vyema??
Nadhani sheria zingine inatakiwa ziwe za kimataifa, Mtu kazaliwa Tanzania, leo unakuja kumwambia si raia wa hii nchi~sasa sijui yeye ni raia wa sayari gani, Mars?. Ni bora hawa CCM wangemtengenezea zengwe lingine lakini kwa hili la uraia mmhh...It doesn't make any sense to me!.
,,,duu huyu dogo wamemuonea....nasikia chilligati ametangaza kuwa atavuliwa vyeo vyake vyote ....na hataweza hata kupiga kura ...nadhani wamembana ili asiweze hata kugombea kupitia chama kingine...unless aweze kuchalange hili suala mahakamani kabla ya uteuzi.....ni wazi safari yake kisiasa imefikia ukingoni......the like of balozi bandora,yule mwenyekiti wa ccm kagera -anatoli,jenerali ulimwengu,na yule mama wa uwt[forget the name].unless otherwise....huyu bashe alikuwa kwenye bifu kali sana na Rizwani....na katika siku za karibuni alikuwa anaonekana kupata nguvu sana!!!
Wakuu hili suala la Bashe tuliangalie kwa mapana zaidi hivi nchi hii ni ya kifalme? ina maana ukikosana na mtoto wa rais mambo yako yanaharibika? nimesikia hata Ridhwan akienda mikoani wakuu wa mikoa na wilaya wanamnyenyekea.Ukichanganya na mama Salma kupokea taarifa kutoka kwa watumishi wa serikali katika ziara zake tusipoangalia taratibu tutaanzisha utawala wa kiimla TAFAKARI CHUKUA HATUA OCTOBER 2010!
Indume Yene;
Kwa sheria za TZ na baadhi ya nchi za Ulaya ,hata kama umezaliwa kwenye nchi hizo lkn wazazi wako wote 2 sio raia itakupasa ukifikisha umri wa miaka 18 uende mahakamani kuapa ili upate uraia wako;Tanzania kwa Afrika na Belgium kwa Ulaya ni mfano tu wa baadhi ya nchi nyingi duniani zinavyofanya hivyo!
CCM wanadai Bashe alizaliwa na wazazi toka Somalia waliofika Tabora;wanadai kuwa wazazi wake walipata uraia wa TZ miaka 10 baada ya Bashe kuzaliwa;kama ni kweli ilikuwa hivyo kisheria ilimpasa Bashe kuomba uraia wa TZ alipofikisha miaka 18 kwani ingawaje yeye alizaliwa TZ lkn wakati anazaliwa wazazi wake HAWAKUWA RAIA WA TZ!
Lkn nimemsikia Bashe mwenyewe akiongea wazi kuwa Mama yake ni MTZ mzawa wa Tabora na anashangaa kuambiwa yeye sio raia!Sheria ya TZ inasema wazi kabisa kuwa"kama mmoja wa Mzazi wako ni mzawa,na wewe mtoto umezaliwa TZ ;automatically bila kuomba uraia ukifikisha miaka 18 unakuwa RAIA halali wa TZ kwa kuurithi toka kwa mmoja wa wazazi wako aliye mzawa"!
Kama anayosema Bashe kuhusu uraia wa Mama yake ni kweli basi CCM wanapaswa wamuombe radhi kwani atakuwa ana sifa za kuwa Raia halali wa TZ akirithi toka kwa mama yake;lkn kama wazazi wake walimzaa wakiwa sio raia ingawaje alizaliwa TZ Bashe anakosa sifa za kuwa Raia wa nchi hii hasa kama alipofikisha miaka 18 hakuuomba mahakamani,na anapaswa kupewa muda aombe upya uraia wake,akikaidi bila kufanya hivyo anapaswa kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kuishi nchini kinyume na sheria!
Sheria na mazoea ni vitu 2 tofauti,na tutakuwa na uwezo mkubwa wa kuongelea suala hili kisheria kama tutapata ukweli wa mambo hasa kama ni kweli wazazi wa BASHE WOTE 2 HAWAKUWA RAIA wakati wanamzaa Bashe au kama Mama yake ni Raia wa TZ hivyo hakuwa na haja yeyote kisheria ya Bashe kuomba uraia wake!
Wakuu hili suala la Bashe tuliangalie kwa mapana zaidi hivi nchi hii ni ya kifalme? ina maana ukikosana na mtoto wa rais mambo yako yanaharibika? nimesikia hata Ridhwan akienda mikoani wakuu wa mikoa na wilaya wanamnyenyekea.Ukichanganya na mama Salma kupokea taarifa kutoka kwa watumishi wa serikali katika ziara zake tusipoangalia taratibu tutaanzisha utawala wa kiimla TAFAKARI CHUKUA HATUA OCTOBER 2010!
Mkuu
Kwanini akosane na mtoto wa rais? Huoni huo ni utovu mkubwa wa nidhamu? Mtoto wa rais ni mtu mkubwa sana. Kwa usalama wa taifa lolote inafaa aheshimiwe. Kila anachotaka kufanya hairuhusiwi kumpinga. Wana JF tusipokuwa makini itafikia mahali watu watatulisha maneno ya uchonganishi kiasi siku ukimkuta mke wako akanavinjari na mtoto wa rais uanze kumkasirikia. Hii itakuwa ni mbaya sana kwa mustakabadhi wa taifa letu. Mtoto wa rais popote duani anaruhusiwa kufanya lolote bila kuhojiwa na wala watu kukasirika. Mfano mzuri ni Libya au Iraq kabla ya USA kuingia. Hizo ndio heshima wanazotakiwa kupewa watoto wa marais. Nashukuru kuona Watanzania na sisi tumeanza kuamka kwani nimesikia hata uchaguzi wa Yanga alikuwepo. Hii inatupa matumaini kwni tunaanza konyesha heshima anayostahili kupewa.