Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

Huyu anajitafutia matatizo zaidi. Angetumia busara kama angefunga safari akaongea na Jenerali Umlimwengu kwanza. Hawa jamaa ndo anawapatia visu vya kumchunia! Ngonja tukae sawa kuangalia jinsi ngoma inavyozidi kuonaga.
 
Ukimsikiliza huyu jamaa utaona kuwa maamuzi ya CCM ni Mizengwe. Kwa kweli sasa ninaanza ku-feel sympathy kwa huyu jamaa. Sikiliza Mahojiano ya BBC: Hussein Bashe na John Chiligati - wavuti utaona kuwa Chiligati naona kawa mpole na ile kauli ya kurudisha kadi na nyadhifa zote hakuitoa.

Huwezi sema wazazi wake walihamia miaka ya sitini sitini bila kuwa na straight facts ni mwaka gani na ilikuwa vipi. Inaonekana uhamiaji kama wameulizwa kweli basi hawana mafaili ya miaka ya sitini. Bashe anasema mama yake ni mzaliwa wa Tabora baba yake ndiyo muhamiaji. CCM inachotakiwa kufanya ni kumfungulia mashitaka Bashe ili akathibitishe uraia wake Mahakamani, na si kumhukumu kwa kumnyang'anya nafasi zake. Aachiwe agombee ubunge wakati kesi ipo mahakamani na mahakama ikithibitisha otherwise anapoteza nafasi yake. Vinginevyo huu ulikuwa ni mkakati wa kuhakikisha Kingwangala anagombea na si Bashe.

Otherwise Bashe kuna vyama vingi tu vya siasa Hamia huko. Nina hakika wewe ndiyo chaguo la wana Nzega.
 
Sasa huyu anaongea nini tena wakati sisiem hawamtaki .Uhamiaji wameshasema
kuwa yeye ni raia ila makamba amesema uhamiaji hawajui kitu.Ukibishana na
mjinga na wewe utakuwa mjinga.

Nimeviona ktk T Daima ya leo vivuli vya hati za Bashe vya kuukana uraia wa Somalia. Makamba could be right, at least this time, kwani inaonekana kama vile hati hizi ni feki tu. Jamaa yangu mmoja ambaye ni very conversant ktk masuala ya Uhamiaji na uraia kaniambia hii ni feki moja kwa moja. Nafikiri hapa kuna bomu jingine litakalolipuka -- dhidi ya utawala wa CCM -- kwamba kuna milungula iliotembea kupata hati hii pamoja na ile barua ya Uhamiaji.

Tusubiri.
 
Unauthibitisho kuwa ni feki? au na wewe unapiga ramli kwa ccm??
 
Hussein Bashe siyo RAIA - hayo mengine ni mengineyo!

Uraia wake umekuwa ukijadiliwa kwenye "circles" nyingi na hata ule mkutano wa Iringa - but it seems yeye alimtegemea sana Rostum kuliko ukweli wenyewe!

Halafu huyu Bashe ana mahusu na Rostam -- ndiye alimleta hapa nchini. Itakumbukwa kuwa Rostam aliondoka hapa nchini katikati ya miaka ya 70 kwenda Iran na kurejea mwisho wa miaka ya themanini. Kule aliishi ktk mji mmoja uitwao Godda ambako kuna jamaa zake. Na Bashe anasema alizaliwa kabla ya baba yake kupata uraia wa Tz mwaka 1987. Miaka hii ni coincidence?

Also Note: Does Godda -- a town in Iran -- ring a bell? Kagoda??????
 
Unauthibitisho kuwa ni feki? au na wewe unapiga ramli kwa ccm??

Just do the waiting act -- my friend! Something big is brewing from those docs -- they are fake through and through -- post-dated and obtained corruptly.
 
Mheshimiwa Makamba amekosea kuingilia kazi zisizokuwa zake, yeye ni nani katika serikali mpaka akatae nyaraka za serikali? madaraka yamemlevya:A S 8:
 
“Wasipowasikia Musa (yaani, Vitabu vya kwanza vitano vya Biblia alivyoandika) na manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu” (Luka. 16:31).

Huyo ndio Luteni Usu Mstaafu YUSUFU MAKAMBA
 
Kuna habari kuwa Hussein Bashe ataongea na waandishi leo..! Je kasema nini...? Vilevile mliopo kwenye press conference hiyo mnaweza kumuuliza kuhusu ripoti hizi mbili zinazotatanisha..

1. Akihojiwa na BBC swahili alisema kuwa yeye ni raia kwakua mama yake ni mtanzania (si msomali) na baba yake ndie msomali kwahivyo amerithi uraia wa mzazi mmoja wapo (mama yake) ambaye ni mtanzania na hana haja ya kuukana uraia wa baba.

2. Gazeti la leo la Mwananchi linadai alishaukana uraia wa Somalia kwenye mahakama ya kivukoni.

Lipi kweli kati ya haya mawili?

acheni fitina jamani BBC ipi umesikia tofauti na sisi mbona hatujasikia
 
Basi kama uraia wake ni feki CCM nao ni feki, Uhamiaji, Feki, ShUle zote alizosoma ni FEKI kama zakwao kila kitu nchii hii nifeki lini tutapata ORIJINO KHA! :mad2::mad2::mad2::mad2::mad2:
 
Tanzania Daima la leo , limetoa nakala ya Kiapo cha kukana Uraia wa Somalia, na kukubaliwa na Naibu kamishna Uhamiaji.
Katika yooote, ccm wanakaribia kufa, njia ileile ya vyama vingine vizee barani Afrika.
 
Mwenye kujua SHERIA naomba anijuze: Mfano nimezaliwa Tanzania maisha yangu yote ni hapo hapo TZ kuanzia kielimu hadi kikazi nikaowa TZ na mwenzi wangu ni mtu wa TZ nikizaa watoto watakuwa ni raia wa wapi? nami ni raia wa wapi ikiwa baba yangu ni MGHANA mama yangu ni Mtanzania??
Nitafuata uraia wa kuzaliwa au wa Baba au wa Mama??
 
Mkuu utaumiza kichwa bure. Bashe ni mtanzania kama Rostam Azizi au zaidi ya Rostam Azizi na au kama wewe ulivyo mtanzania. Tatizo la hawa akina bashe ni utegemezi kutaka kubebwa bebwa na either wakubwa au watoto wa wakubwa. inapotokea unamkosea hata mtoto wa mkubwa, system yote inakuangukia.
 
sawa sawa tu hata simuonei huruma angekuwa mtu mwingine ndiyo
yeye alivyokuwa anatamba na hela za rushwa nzega na takururururu hawakufika alijiona mjanja sana
angalau seleli yuko happy kidogo

fisadi hufisadiwa
 
Mkuu utaumiza kichwa bure. Bashe ni mtanzania kama Rostam Azizi au zaidi ya Rostam Azizi na au kama wewe ulivyo mtanzania. Tatizo la hawa akina bashe ni utegemezi kutaka kubebwa bebwa na either wakubwa au watoto wa wakubwa. inapotokea unamkosea hata mtoto wa mkubwa, system yote inakuangukia.

Mkuu hilo nalo neno, maana habari ndio hiyo
 
There is possibility that he querreled with those who were called god fathers and they want to show their influence within the party and within the governing system.
 
Dark City,

Huyu anajimaliza tena vibaya, hata ulimwengu, Balozi Badora walipiga kelele hivi hivi vitu vilipowekwa hadharani walifayata. CCM hawawezi kukurupuka kiasi hicho, na kama hivyo vyeti ni feki basi wanamfunga.
 
Back
Top Bottom