Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa huyu anaongea nini tena wakati sisiem hawamtaki .Uhamiaji wameshasema
kuwa yeye ni raia ila makamba amesema uhamiaji hawajui kitu.Ukibishana na
mjinga na wewe utakuwa mjinga.
Nimeviona ktk T Daima ya leo vivuli vya hati za Bashe vya kuukana uraia wa Somalia. Makamba could be right, at least this time, kwani inaonekana kama vile hati hizi ni feki tu. Jamaa yangu mmoja ambaye ni very conversant ktk masuala ya Uhamiaji na uraia kaniambia hii ni feki moja kwa moja. Nafikiri hapa kuna bomu jingine litakalolipuka -- dhidi ya utawala wa CCM -- kwamba kuna milungula iliotembea kupata hati hii pamoja na ile barua ya Uhamiaji.
Tusubiri.
Hussein Bashe siyo RAIA - hayo mengine ni mengineyo!
Uraia wake umekuwa ukijadiliwa kwenye "circles" nyingi na hata ule mkutano wa Iringa - but it seems yeye alimtegemea sana Rostum kuliko ukweli wenyewe!
Unauthibitisho kuwa ni feki? au na wewe unapiga ramli kwa ccm??
Kuna habari kuwa Hussein Bashe ataongea na waandishi leo..! Je kasema nini...? Vilevile mliopo kwenye press conference hiyo mnaweza kumuuliza kuhusu ripoti hizi mbili zinazotatanisha..
1. Akihojiwa na BBC swahili alisema kuwa yeye ni raia kwakua mama yake ni mtanzania (si msomali) na baba yake ndie msomali kwahivyo amerithi uraia wa mzazi mmoja wapo (mama yake) ambaye ni mtanzania na hana haja ya kuukana uraia wa baba.
2. Gazeti la leo la Mwananchi linadai alishaukana uraia wa Somalia kwenye mahakama ya kivukoni.
Lipi kweli kati ya haya mawili?
acheni fitina jamani BBC ipi umesikia tofauti na sisi mbona hatujasikia
acheni fitina jamani BBC ipi umesikia tofauti na sisi mbona hatujasikia
Acha kubisha vitu usivyokua na uhakika navyo......Jamaa alihojiwa na BBC swahili......
Mwenye kujua SHERIA naomba anijuze: Mfano nimezaliwa Tanzania maisha yangu yote ni hapo hapo TZ kuanzia kielimu hadi kikazi nikaowa TZ na mwenzi wangu ni mtu wa TZ nikizaa watoto watakuwa ni raia wa wapi? nami ni raia wa wapi ikiwa baba yangu ni MGHANA mama yangu ni Mtanzania??
Nitafuata uraia wa kuzaliwa au wa Baba au wa Mama??
Mkuu utaumiza kichwa bure. Bashe ni mtanzania kama Rostam Azizi au zaidi ya Rostam Azizi na au kama wewe ulivyo mtanzania. Tatizo la hawa akina bashe ni utegemezi kutaka kubebwa bebwa na either wakubwa au watoto wa wakubwa. inapotokea unamkosea hata mtoto wa mkubwa, system yote inakuangukia.