Kamati Kuu ya CCM yaielekeza Serikali kuchukua hatua kuhusu maoni ya TOZO

Huyu kijana yupo mtupu kichwani.
 

Badala ya kuelekeza pekee wametoa maoni pesa itoke wapi ya hiyo miradi kama sio tozo. Raisi akikopa tutalalamika, wakiongeza kodi tutalalamika, wasikoweka uwekezaji kwenye kilimo tutalalamika hii inaonyesha Watanzania hawajui watakalo. Tumezoea kutokuwekeza na misaada ya wenzetu ambao huko kwao wanalipa tozo
 

Drama Kings & Queens kama kawaida.

Waliopanga hiyo tozo wapumzishwe kwa sababu ubunifu wao tayari umeshapunguza imani ya wananchi kwa serikali kwa kiwango kikubwa.

Kushughulikia tozo pekee huku akili zile zile zilizoileta bado zipo mamlakani ni kuwatukana na kuwadharau wananchi
 
MALALAMIKO ya utitiri wa kodi hususani za miamala ya simu na ya kibenki, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa iliyokutana jana Septemba 7,2022, imetoa maelekezo sita kwa serikali ikiwemo kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu utozaji wake wa Kodi.

Pia imetakiwa kuzingatia Ilani kuwapatia nafuu wananchi wa kipato cha chini hususani wa vijijini, kubana matumizi, kuongeza wigo wa kodi, kubuni vyanzo na mfumo rafiki kwa kila mwananchi na kusikiliza maoni na ushauri.

Akizungumza leo Septemba 8,2020 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka kwenye ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam, amesema maelekezo hayo yaliyotolewa kwa serikali yamezingatia ibara ya 20 (b) ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.

“Naomba kuinukuu, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa gharama nafuu kwa kupanua wigo wa matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kifedha, ili kuongeza huduma jumuishi za fedha nchini, kuchochea uwekezaji wa ndani na kukidhi mahitaji halisi ya wananchi hususan wa kipato cha chini na waishio vijijini.” Amesema Shaka.

Maelekezo hayo ya Kamati Kuu yamekuja ikiwa tozo za miamala ya simu ilianza kupigiwa kelele tangu ilipoanza kutumika mwaka jana, tozo kwenye miamala ya kibenki imeibua upya hisia za malalamiko kuhusu mzigo wa tozo kwa wananchi.

Shaka amesema licha ya miradi mbalimbali ya maendeleo kutekelezwa kwa fedha za tozo na kuwawekea wananchi mazingira mazuri ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025, lakini serikali haina budi kuwapunguzia wananchi makali ya maisha kwa kupunguza utitiri wa tozo hususani za kieletroniki na kuweka kodi rafiki.

“Serikali imeweza kufanya mambo makubwa katika kipindi kifupi kwa mfano; ujenzi wa vituo vya afya 234 na shule mpya za sekondari 214 na maeneo mengine kadhaa, ambayo yanagusa maisha ya Watanzania ya kila siku.

“Hata hivyo baada ya kutafakari na kujadiliana na kubishana vikali, serikali haina budi kufuata maelekezo na siku si nyingi mtapata taarifa ya hatua zilizochukuliwa baada ya maelekezo haya,” amesema na kuongeza kuwa CCM itakua kali na kufuatilia mienendo na uwajibikaji wa wateule wa Rais.

“Wasaidizi wa Rais washuke chini kwenda kusikiliza kero za wananchi, tumefanya ziara mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza, kuna changamoto lukuku ambazo si lazima Rais ndio ashuke chini kuzishughulikia, wakijipanga vizuri changamoto hizo zinatatuliwa,” amesema.
 
Mkono wa kulia unatengeneza tatizo (kwa kuweka tozo) halafu mkono wa kushoto unatoa maelekezo kutatua tatizo (kupunguza tozo).

Boring tune from the very same old party
 
Kamati Kuu inapoiagiza Serikali huwa inamtoa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania ana inamjumlisha? Kama anajumlishwa yeye si ndiyo mwenyekiti wa hiyo Kamati Kuu? Kwa maana nyingine anajiagiza kuhusu tozo aliyoipitisha mwenyewe iwe tozo.
 
Kitendo Cha chama changu ccm kuchuchukuwa tozo ktk mafuta na hyo hyo tozo wakapeleka Kutoa ruzuku hakika nimeona Kuna nati aziko sawa kwa viongoz wetu mafuta yamesababisha maisha kuwa magumu na upatikanaji wa chakula kuwa mgumu na Bei kuwa juu yote hayo Ni kutokana Bei za wese mshindwe ccm na kulegea

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo Serikali za kiafrika hizo.

Linatengenezwa tatizo, chawa wanalipamba huku walio wengi wanapumlia mashine halafu unajitia kusikia kilio cha wengi, unalitatua.

Chawa wanaibuka tena kuipongeza serikali kwa usikivu.

Ndiyo maisha yetu hayo.
Hasa Steve yule chawa wa kulipwa.
 
Wamelitengeneza wenyewe kwa mbwembwe kisha eti wanalishangaa! Na mimi ninawashangaa!
 
Niliwahi kuuliza uwezo wa huyu mwenyekiti kupambanua mambo nikaambiwa nawachukia wanawake.
Mwigulu ana makusudi yake dhidi ya huyu mama asiyeelewa kinachoendelea.
😂 changa likiiva litapasuka na Mtu.

🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…