Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Hiyo ya utayari wa kuchangia chama ni uongo. Mtajitahidi hapo mwanzo lakini ikiaikainen miezi miwili mtaacha kuchangia kwa kusingizia hamna imani na chama cha wachaga. Hamna nia njema na Chadema.

Amandla...
Walivyotolewa kwa michango gerezani wewe uliombwa hata mia??
 
Kwa nini mnakazania sana wakubali kupewa viti vya chee? Hamtaki kuwa wenyewe huko mjengoni maana mtakosa wa kumsimanga na vijembe vyenu? Yaani kina kona mnalazimisha eti wasikatae hivyo viti vya kupewa why??? Nendeni wenyewe...
 
Kususa kama chama itakuwa anguko kuwepo hata wachache bungeni sauti yao itakuwa muhimu japo watakuwa hawana meno sana,kutokupeleka kabisa wanajizika wenyewe kisiasa
Kwani walivyoiba kura hawakujua kuwa kunahitaji sauti ya upinzani mulisema hawapeleki mae.deleo sehemu waliyochagua upinzani kwa hiyo hao wanaenda kuwatetea nani
 
Ni sawa na kuacha kula nyama ya nguruwe kwakua ni haramu ilhali unapikia mafuta ya nguwe vyakula vyako vyote.
Nadhani unajuwa kuwa wanahitaji ruzuku na michango ya wabunge ili wajiendeshe kama chama. Katika miaka mitano iliyopita walipata Tsh21b kwa njia hiyo na inevyoonekana ni kuwa miaka mitano ijayo hawatafikia hata milioni 60 kwa kumtumia mbunge mmoja tu, wanahitaji wabunge zaidi wa kuteuliwa wambao ndio huchangia zaidi.
 
Mbowe aache kujichaguwa viti maalum atakula wapi. Hivyo viti vitasaidia kuipa ruzuku CHADEMA, ama sivyo watapata zero ruzuku.
 
No

Big no mkuu. Waachane nao tu. Mwakani hata Sisomi habari yeyote ya bunge. Ctaki kumjua hata spika wa bunge. Naomba akipatikan msiniambie mimi... Shit ana
😂😂

Ngoja tuone.
 
Lipumba anasemaje!?? Mwenye viti vinne!?
 
Thubutu. Mbowe aache kuwateua ndugu zake awateue hao.
 
Una hoja ya msingi mkuu.. Ila sidhani kama itatekelezeka.

Ni vigumu sana kuacha hela. Kumbuka CDM hawana chanzo kingine chochote cha mapato zaidi ya Ruzuku.

Ila wakifanya hivyo litakuwa ni somo kubwa kwa Dictator Uchwara.
 
Kama Watanzania hawataki kuandama maana yake hawaikubali hiyo agenda ya CHADEMA. Hakuna wafuasi. Demokrasia maana yake wengi wape, kama Watanzania hawataki kwa nini uwaingize mabeberu? Kumbuka mtu anayekusaidia kwa masharti si mtu mzuri. Hakuna kitu kibaya kama misaada ya masharti. Ndiyo maana TZ imeamuwa kutegemea zaidi pesa za ndani kwenye maendeleo kuliko misaada anbayo mwisho wake ni manyanyaso. Hao wakubwa wanalijuwa hili na wameisha msoma Magufuli, kwa hiyio ni waangalifu saana kwenye hili.
 
Chadema, kujiimarisha na kujiporomosha vyote viko mikononi mwenu.

Bora kufa kishujaa kuliko kuishi ukiwa unamuabudu, unasujudu, na kumsifu nyapara jiwe
Mkuu chama kilichokufanya sio Chadema bali ni CCM.Dola imeamua kupora ushindi wa Chadema baada ya CCM kukosa ushawishi!
 
pesa pesa.....Yuda Iskalioti alimuuza Yesu kwa vipande thelathini vya pesa...subiri muone! mleta mada mwenye kaandika kinjaa zaidi...between the line anataka "wote wakose, maana kwenye wachache hawezi kuwemo...amekata tamaa! "
Hivi mtu akikuibia pesa zako ,akatumia hizo pesa kujenga nyumba .Akikukaribishe ukaishi kwenye nyumba hiyo kisa umekosa makazi utakubali?
 
Kamanda kwanini Lema,Mbowe et al hawakugoma kuapishwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2015?
 
Nafasi hii CDM na ACT wanayopewa kufanya maridhio wanatakiwa wautumie vizuri kutokubali kugawiwa TU vyeo kama posho kwa waliyo fanyika... Hakika hapa itadhihilisha upinzani tz Ni wasaka tonge kama ccm tu.

Badala yake waandae list ya demands kushikiza ccm na serikali kuitekeleza ili kufika maridhio na muafaka wa kitaifa wenye manufaaa ya muda mrefu kwa zaidi mtu mmoja mmoja au ya chama kimoja kimoja. Pia kukomsha haya yaliyotokea kwenye uchaguzi huu..

Demand list
1- kuvunjwa kwa NEC hii mara moja, ifanyiwe reforms ya muundo kuifanya iwe huru.

2- Polisi tz, ifanyiwe mabadiriko makubwa ya kufunga isiweze kutumika kisiasa kunufaisha chama chochote.

3- Matokeo ya Rais tz yarusiwe kupigwa mahakamani

4- Kufanyia marekebisho katiba haraka kunguza mamlaka ya Rais kuteua majaji ili kuongeza Uhuru wa mahakama

5- Kupanga muda wa kumalizia mchato wa katiba mpya toka pale kwa rasimu ya Warioba... NB mvhakato undelea Bila kuhodhiwa na wanasiasa Kama ilivyokuwa Hadi kupelekea ukakwama,

6- Ongezeaeni au kuboeesha haya.


Kukubali kupata viti kadhaa vya hisani bungeni itakuwa ni kujisaliti kwa msimo wenu kuwa mna hubiri mabadiriko/reforms. Hakuna kipindi kizuri Cha kushinikiza ajenda/demand za upinzani Kama hiki ambacho mmeitwa mezani kujadiri kufikia mwafaka wa maridhiano,

OTHERWISE kupata nafasi kadhaaa bungeni kwa ajili ya mshahara,posho na ruzuku ndio huwa lengo lenu japo mnajificha kwenye kutetea watz kwa kutaka reforms.

Msidanganyike na kutudanganya kuwa mkubali hiyo offer eti wakapatikane watu wa kupush ajenda ya kutata reforms mle bungeni, wote tunajua maamuzi ya kungeni huwa yanafikiwa kwa kupiga kura (zikipingwa kwa ushabiki wa vyama, CCM vs vingine) Tangu kuanzishwa kwa vyama vingi tz hakuna jambo ambalo serikali ya ccm itakipeka bungeni likakwama au likapita kwa sababu kulikuwa na wabunge kadhaa wa upinzani, and vice versa (yaani upinzani tz tangu kuanzishwa kwako haijawahi kushinikiza Jambo lolote ile kubwa ambalo ccm wanilipinga/hawakubalini nalo likafanikiwa kupita bungeni)..
 
Kwa sasa kususa ndio solution muafaka,ni njia ya kuionesha dunia kwa vitendo kwamba hujatendewa haki na hujaridhika.Tena nawashauri wawe consistent wasirudi nyuma katika hili.Hao wanaotamani huo ubunge wa kuteuliwa wafutwe uanachama ili wawe huru kuunga juhudi ambayo kimsingi ni haki yao.Ila kupokea ofa za namna hiyo kichwa kichwa kuna gharama kubwa kisiasa.Chama hakitaaminika tena na wananchi.Hata hivyo misukosuko hii ndio itatoa picha halisi kwamba upinzani tulio nao upo kwa ajili ya nani kati ya tumbo na Maendeleo ya wananchi.Itafahamika tu.
 
Unawadanganya viongozi wako na unawaingiza chaka kabisa.Mwaka huu kulikuwa na wagombea urais 13 ccm inao uwezo wa kupata wabunge wa upinzani bila hata chadema na ACT kuwemo.Zanzibar Seif alususa lakini serikali haikusimama na ilikubalika kimataifa.
Na CHADEMA nao wasuse ili serikali iendelee kusimama hatimaye tuzidi kukubalika kimataifa.Wasusie kila aina ya ulaghai ili tukubalike zaidi na zaidi kimataifa.
 
N

Yie ndo.mnashiriki kukiua hicho chama, endeleeni kutoa ushauri usio kuwa na maana.
Chama chenu kitabaki kama cha Dovutwa hapa tanzania.
Hapo wasusie tu hamna namna.Ndo watajijengea heshima zaidi kwa wananchi.Kama Chama hakijafa 2015-2020 naamini hakifi katu hasa hasa kama wakisusa.Wakikubali ofa hizo batili ndo CHADEMA kitakuwa kama Dovutwa.
 
Wasuse tu hamna namna.Ijulikane wazi nchi hii ni ya Chama kimoja vingine geresha tu.Labda wabaki akina Lipumba na Mzee wa ubwabwa na vyama vingine vya kuzugia.Kwenye chaguzi hususani kipindi cha kampeni CCM wawe wanafanya kampeni kiulaini wasiwe wanakutana na fyoko fyoko yoyote.Kifupi siasa halisi ifanywe na CCM peke yao wengine tujikite kwenye hapa kazi tu.Bajeti ya uchaguzi ipunguzwe iongezwe kwenye miradi muhimu zaidi ya Maendeleo.Naamini CCM ikikabidhiwa rasmi hati miliki ya siasa za nchi hii Tz itageuka ulaya maana wao pekee ndo wenye nia ya kutuletea wananchi maendeleo,vyama halisi vya upinzani tumeambiwa watauza nchi kwa mabeberu.Nasisitiza CHADEMA na ACT sio tu wasusie ofa batili bali na chaguzi zote ili wawapishe CCM watuletee maendeleo bila bughudha na kelele za akina Msigwa,Lema,Halima,Sugu,Zito,Heche,Mbowe n.k
 
Si kweli kwamba uhai wa Chama cha upinzani ni fedha tu,kumbuka upinzani ni roho isiyokufa kamwe.Hata dunia nzima tukifa,upinzani utaendelea kuishi daima.Hata hivyo CHADEMA kikifa kwa namna unavyojaribu kutuaminisha nadhani itakuwa vizuri sana kwa sababu tumeambiwa watauza nchi kwa mabeberu,zaidi sana wanakwamisha maendeleo.Je,upo tayari kuona Tz yetu ikiuzwa kwa mabeberu?
 
Kwa hapa kwetu jambo la maana kabisa ni kususa au kujitoa kabisa ibaki CCM peke yake ambayo haiuzi nchi kwa mabeberu,wengine tupige kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…