Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Hiyo ya utayari wa kuchangia chama ni uongo. Mtajitahidi hapo mwanzo lakini ikiaikainen miezi miwili mtaacha kuchangia kwa kusingizia hamna imani na chama cha wachaga. Hamna nia njema na Chadema.

Amandla...
Walivyotolewa kwa michango gerezani wewe uliombwa hata mia??
 
CCM hawana mamlaka ya kutoa viti maalum. Hivi ni viti ( bila shaka wanastahili zaidi ya hapo) ambavyo ni stahili ya CHADEMA na vimetokana na kura walizopigiwa. Sio fadhila ya NEC wala CCM. Aidha ruzuku haitoki kwenye mfuko wa CCM bali inatokana na kodi ambazo wananchi wote wanachangia bila kujali itikadi yao. Sio fadhila, ni haki yao na wanastahili kulipwa ili waendeshe shughuli zao. Kusema kuwa wakipokea watageuka kuwa ni chama "ruzuku" ambacho hakijali "principles" ni upuuzi maana wakati hao unaowanyooshea vidole wanafilisiwa, wanapigwa, wanafunguliwa kesi za kutungwa, wanapofungwa, wanapopigwa mabomu, wanapodhalilishwa na vijana wadogo ambao madaraka yamewafanya wakose adabu, wanafukuzwa bungeni, wanapozuiwa kufanya kampeni, wanaponyimwa stahili zao n.k. wewe shujaa na wenzako kama wewe wenye "principles" hamkujitokeza kusimama nao.

Badala yake mnajificha kwenye majukwaa kama haya na kujimwambafai. Mngekuwa mnasimama nao toka mwanzo hali isingefikia hapa. Polisi wangejua kuwa wakimgusa mmoja wao kwa uonevu mngejitokeza kwa wingi, wangeacha kuwabughudhi. Mngesimama kidete kuhakikisha haki inatendeka kwenye vituo vya kupigia kura sio wasimamizi wala NEC ambao wangethubutu kufanya waliofanya.

Wakina Salome Makamba, Pendolino Peneza, Suzan Kiwanga, Nusrat na wengine wengi tu wametupwa ndani au wamenyang'anywa haki yao ya kugombea lakini nyinyi wenye " principles " ambao mko tayari kufia chama mliufyata. Waacheni ambao wameonyesha kwa matendo kuwa ni watetezi wa wananchi na chama chao wapewe nafasi ya kuendelea kufanya. Mkitaka wasifanye hivyo , nyie Great Thinkers, anzeni kuwaonyesha kwa matendo kuwa mko pamoja nao. Kama hamuwezi, nyamazeni.

Amandla...
Kwa nini mnakazania sana wakubali kupewa viti vya chee? Hamtaki kuwa wenyewe huko mjengoni maana mtakosa wa kumsimanga na vijembe vyenu? Yaani kina kona mnalazimisha eti wasikatae hivyo viti vya kupewa why??? Nendeni wenyewe...
 
Kususa kama chama itakuwa anguko kuwepo hata wachache bungeni sauti yao itakuwa muhimu japo watakuwa hawana meno sana,kutokupeleka kabisa wanajizika wenyewe kisiasa
Kwani walivyoiba kura hawakujua kuwa kunahitaji sauti ya upinzani mulisema hawapeleki mae.deleo sehemu waliyochagua upinzani kwa hiyo hao wanaenda kuwatetea nani
 
Ni sawa na kuacha kula nyama ya nguruwe kwakua ni haramu ilhali unapikia mafuta ya nguwe vyakula vyako vyote.
Nadhani unajuwa kuwa wanahitaji ruzuku na michango ya wabunge ili wajiendeshe kama chama. Katika miaka mitano iliyopita walipata Tsh21b kwa njia hiyo na inevyoonekana ni kuwa miaka mitano ijayo hawatafikia hata milioni 60 kwa kumtumia mbunge mmoja tu, wanahitaji wabunge zaidi wa kuteuliwa wambao ndio huchangia zaidi.
 
Wakihalalisha haramu kuwa halali basi wajue CCM itarudia michezo hii tena na tena na wananchi watawaona kuwa ni chama cha ruzuku tu hakipo tayari kutetea principle zao!

Chadema hawawezi kudai eti bora waende bungeni na hivyo eti kwa uchache wao huo wakatetee wananchi!! , wakawatetee kwa nani?, yaani wakawateteee wananchi kwa serikali hii hii ya CCM iliyowapora uchaguzi waziwazi?

Chadema hawawezi kutangaza kutoutambua uchaguzi hakafu wakatoka hapo eti wanataka wanufaike na uchaguzi huo wasioutambua!

Kamati kuu isimame imara, ikikubali kuhalalisha ujinga basi nayo itakuwa jinga na haitokuwa na maana iwepo!

Na wawe makini na watu wa dini watakaotumwa kwao kuwalainisha ili walainike na pia wawe makini na ID za mitandaoni zitakazokuwa zikitumika kuwapa ushauri wa kukubaliana na haramu ile.

Chadema isimamie msemo wae wa Sasa basi, ili tuanze chapter mpya ya kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya!
Mbowe aache kujichaguwa viti maalum atakula wapi. Hivyo viti vitasaidia kuipa ruzuku CHADEMA, ama sivyo watapata zero ruzuku.
 
No

Big no mkuu. Waachane nao tu. Mwakani hata Sisomi habari yeyote ya bunge. Ctaki kumjua hata spika wa bunge. Naomba akipatikan msiniambie mimi... Shit ana
😂😂

Ngoja tuone.
 
Ng'ombe atachijwa alivyolala na msimu huu hakuna kuachia kitu.. Walioshinda waende bungeni na idadi ya viti maalumu itakayopatikana waende bungeni. Ruge Mdee, Matiko ,Bulaya, Mwaifunga, Mwakagenda, Pareso, Aliyegombea Singida mjini na Dodoma mjini wote wateuliwe.
Thubutu. Mbowe aache kuwateua ndugu zake awateue hao.
 
Kama wanataka tuwaone wajinga wa kutupa wakubali viti maalum .Watakuwa wamefanya ujinga wa hali ya juu sana , Yaani wasithubutu kufanya hivyo basi sisi wananchi tutakuwa hatuna imani nao tena , unaenda kukaa meza moja na muuaji , mporaji , dhulumati ? Aliyekupora ushindi hadharani .Watumieakili .Na mimi niliwaambia vyama vyote humu mwaka jana , wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wasishiriki uchaguzi huo maana watakuwa wanahalalisha uchaguzi haramu kuwa halali , niliandika thread tano ,unaweza kureview hawakusikia .Sasa ndio kama wana akili watajifunza kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya .Wawaache CCM waweke viti vyao maalum mbonawdna watu wengi tu .Kuna Alhad Musa Salim na kamati yake ya amani , kadinari Pengo , Wagombea uchwara wa urais ambao hawskupata kura hata mia , kina Queen Sendiga , Wana wake zao , watoto wao wawape hao .
Una hoja ya msingi mkuu.. Ila sidhani kama itatekelezeka.

Ni vigumu sana kuacha hela. Kumbuka CDM hawana chanzo kingine chochote cha mapato zaidi ya Ruzuku.

Ila wakifanya hivyo litakuwa ni somo kubwa kwa Dictator Uchwara.
 
CHADEMA sasa wakae nje ya Bunge kabisa. Wadai Tume huru kwa kupitia nchi wahisani kwa vile Watanzania hawako tayari kuandamana kwa sasa. Misaada ikatwe mpaka Tume huru itakapoundwa. Hatuwezi kabisa kujitegemea.

Kama hilo haliwezekani, waunde vikundi vya kigaidi (underground). Wawatungue wasimamizi wa uchaguzi, viongozi wa CCM, Msajili nk. Heshima itarudi.
Kama Watanzania hawataki kuandama maana yake hawaikubali hiyo agenda ya CHADEMA. Hakuna wafuasi. Demokrasia maana yake wengi wape, kama Watanzania hawataki kwa nini uwaingize mabeberu? Kumbuka mtu anayekusaidia kwa masharti si mtu mzuri. Hakuna kitu kibaya kama misaada ya masharti. Ndiyo maana TZ imeamuwa kutegemea zaidi pesa za ndani kwenye maendeleo kuliko misaada anbayo mwisho wake ni manyanyaso. Hao wakubwa wanalijuwa hili na wameisha msoma Magufuli, kwa hiyio ni waangalifu saana kwenye hili.
 
Chadema, kujiimarisha na kujiporomosha vyote viko mikononi mwenu.

Bora kufa kishujaa kuliko kuishi ukiwa unamuabudu, unasujudu, na kumsifu nyapara jiwe
Mkuu chama kilichokufanya sio Chadema bali ni CCM.Dola imeamua kupora ushindi wa Chadema baada ya CCM kukosa ushawishi!
 
pesa pesa.....Yuda Iskalioti alimuuza Yesu kwa vipande thelathini vya pesa...subiri muone! mleta mada mwenye kaandika kinjaa zaidi...between the line anataka "wote wakose, maana kwenye wachache hawezi kuwemo...amekata tamaa! "
Hivi mtu akikuibia pesa zako ,akatumia hizo pesa kujenga nyumba .Akikukaribishe ukaishi kwenye nyumba hiyo kisa umekosa makazi utakubali?
 
Kamanda kwanini Lema,Mbowe et al hawakugoma kuapishwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2015?
Sishauri viti maalum waende bungeni, huyo dada aliyechaguliwa aende maana ameshaonyesha hajali sana yaliyotokea kwenye uchaguzi huu, bali anajali zaidi ubunge wake. Ili asipewe airtime negative, aachwe aende. Kusikika sio lazima bungeni, mbona Lisu hakuwa bungeni zaidi ya miaka mitatu, na bado karudi na mvuto hadi imebidi uchaguzi unajisiwe? Hawa cdm hata sasa hawakupata mvuto huu kupitia bunge hili maana halikuwa live, na walitangazwa zaidi kwa mambo negative kuliko positive. Siamini kama bunge hili ndio linaweza kuwajenga cdm zaidi ya kuhalalisha uhayawani.
 
Nafasi hii CDM na ACT wanayopewa kufanya maridhio wanatakiwa wautumie vizuri kutokubali kugawiwa TU vyeo kama posho kwa waliyo fanyika... Hakika hapa itadhihilisha upinzani tz Ni wasaka tonge kama ccm tu.

Badala yake waandae list ya demands kushikiza ccm na serikali kuitekeleza ili kufika maridhio na muafaka wa kitaifa wenye manufaaa ya muda mrefu kwa zaidi mtu mmoja mmoja au ya chama kimoja kimoja. Pia kukomsha haya yaliyotokea kwenye uchaguzi huu..

Demand list
1- kuvunjwa kwa NEC hii mara moja, ifanyiwe reforms ya muundo kuifanya iwe huru.

2- Polisi tz, ifanyiwe mabadiriko makubwa ya kufunga isiweze kutumika kisiasa kunufaisha chama chochote.

3- Matokeo ya Rais tz yarusiwe kupigwa mahakamani

4- Kufanyia marekebisho katiba haraka kunguza mamlaka ya Rais kuteua majaji ili kuongeza Uhuru wa mahakama

5- Kupanga muda wa kumalizia mchato wa katiba mpya toka pale kwa rasimu ya Warioba... NB mvhakato undelea Bila kuhodhiwa na wanasiasa Kama ilivyokuwa Hadi kupelekea ukakwama,

6- Ongezeaeni au kuboeesha haya.


Kukubali kupata viti kadhaa vya hisani bungeni itakuwa ni kujisaliti kwa msimo wenu kuwa mna hubiri mabadiriko/reforms. Hakuna kipindi kizuri Cha kushinikiza ajenda/demand za upinzani Kama hiki ambacho mmeitwa mezani kujadiri kufikia mwafaka wa maridhiano,

OTHERWISE kupata nafasi kadhaaa bungeni kwa ajili ya mshahara,posho na ruzuku ndio huwa lengo lenu japo mnajificha kwenye kutetea watz kwa kutaka reforms.

Msidanganyike na kutudanganya kuwa mkubali hiyo offer eti wakapatikane watu wa kupush ajenda ya kutata reforms mle bungeni, wote tunajua maamuzi ya kungeni huwa yanafikiwa kwa kupiga kura (zikipingwa kwa ushabiki wa vyama, CCM vs vingine) Tangu kuanzishwa kwa vyama vingi tz hakuna jambo ambalo serikali ya ccm itakipeka bungeni likakwama au likapita kwa sababu kulikuwa na wabunge kadhaa wa upinzani, and vice versa (yaani upinzani tz tangu kuanzishwa kwako haijawahi kushinikiza Jambo lolote ile kubwa ambalo ccm wanilipinga/hawakubalini nalo likafanikiwa kupita bungeni)..
 
Kususa sio solution nzuri hata kidogo mbona enzi za dr slaa walikuwa few na impact's yake ilionekana, ccm si yakususiwa hapo wakija na propaganda mfu na akili hizi za watanzania wapinzani kuja kuaminiwa itachukua mda mrefu. Waache ujinga wa kususa waende bungeni waje na new strategy.
Kwa sasa kususa ndio solution muafaka,ni njia ya kuionesha dunia kwa vitendo kwamba hujatendewa haki na hujaridhika.Tena nawashauri wawe consistent wasirudi nyuma katika hili.Hao wanaotamani huo ubunge wa kuteuliwa wafutwe uanachama ili wawe huru kuunga juhudi ambayo kimsingi ni haki yao.Ila kupokea ofa za namna hiyo kichwa kichwa kuna gharama kubwa kisiasa.Chama hakitaaminika tena na wananchi.Hata hivyo misukosuko hii ndio itatoa picha halisi kwamba upinzani tulio nao upo kwa ajili ya nani kati ya tumbo na Maendeleo ya wananchi.Itafahamika tu.
 
Unawadanganya viongozi wako na unawaingiza chaka kabisa.Mwaka huu kulikuwa na wagombea urais 13 ccm inao uwezo wa kupata wabunge wa upinzani bila hata chadema na ACT kuwemo.Zanzibar Seif alususa lakini serikali haikusimama na ilikubalika kimataifa.
Na CHADEMA nao wasuse ili serikali iendelee kusimama hatimaye tuzidi kukubalika kimataifa.Wasusie kila aina ya ulaghai ili tukubalike zaidi na zaidi kimataifa.
 
N

Yie ndo.mnashiriki kukiua hicho chama, endeleeni kutoa ushauri usio kuwa na maana.
Chama chenu kitabaki kama cha Dovutwa hapa tanzania.
Hapo wasusie tu hamna namna.Ndo watajijengea heshima zaidi kwa wananchi.Kama Chama hakijafa 2015-2020 naamini hakifi katu hasa hasa kama wakisusa.Wakikubali ofa hizo batili ndo CHADEMA kitakuwa kama Dovutwa.
 
Kwa wale wanaosema wasiingie bungeni wangetoa ushauri wa nini wafanye wakiwa nje ya bunge. Waeleze chama kitajiendesha vipi wakiwa nje ya bunge. Waeleze chama kitawapiganiaje waliotiwa ndani kwa kukitetea chama.
Lissu ndio huyo anahamia Ubelgiji ambako bila shaka ataendeleza juhudi zake za uharakati.
Kutegemea kuwa nchi za magharibi zitaiwekea serikali vikwazo na kushinikiza mabadiliko wakati nyie wenyewe mmejifungia ndani ni ndoto za alinacha.
Hao wakina dada wanaotaka kuingia bungeni ni wapiganaji na mpaka sasa hivi wajitolea sana kwenye harakati za kutetea maslahi ya wananchi. Hawa wakiwa bungeni wana ujasiri wa kuikosoa serikali pale inapokosea na hivyo kuwafungua macho raia wasio na uelewa. Wasipokuwepo, serikali itajifanyia inavyotaka wakijua hamna wa kuwaonyesha raia athari za maamuzi yao. Msijidanganye kuwa mtaweza kuwaelimisha kwa kupitia social media.
Mkiwakataza ndio mwanzo wa kuwa insignificant.

Amandla...
Wasuse tu hamna namna.Ijulikane wazi nchi hii ni ya Chama kimoja vingine geresha tu.Labda wabaki akina Lipumba na Mzee wa ubwabwa na vyama vingine vya kuzugia.Kwenye chaguzi hususani kipindi cha kampeni CCM wawe wanafanya kampeni kiulaini wasiwe wanakutana na fyoko fyoko yoyote.Kifupi siasa halisi ifanywe na CCM peke yao wengine tujikite kwenye hapa kazi tu.Bajeti ya uchaguzi ipunguzwe iongezwe kwenye miradi muhimu zaidi ya Maendeleo.Naamini CCM ikikabidhiwa rasmi hati miliki ya siasa za nchi hii Tz itageuka ulaya maana wao pekee ndo wenye nia ya kutuletea wananchi maendeleo,vyama halisi vya upinzani tumeambiwa watauza nchi kwa mabeberu.Nasisitiza CHADEMA na ACT sio tu wasusie ofa batili bali na chaguzi zote ili wawapishe CCM watuletee maendeleo bila bughudha na kelele za akina Msigwa,Lema,Halima,Sugu,Zito,Heche,Mbowe n.k
 
Sasa hizo harakati za kutafuta kuishika dola zinafanyika kwa maneno..Zina itaji watu na vifaa..kufikisha chadema huko sumbawanga vijijini...Sasa hao watu watazunguka hii Tanzania kwa miguu..ili uweze kujenga chama unaitaji fedha..hizo fedha watazitoa wapi..Kama wangekuwa na wafadhili wawape kuanzia milioni Mia mbili kila mwezi sawa...lakini ndugu yangu naona kususia ndio kukiuachama na sio kukijenga..narudia afadhali kushiba kwa masingo kuliko kufa kwa njaa ukijifanya mgumu..cuf wanalijua hili vizuri
Narudia chedema akili za kuambiwa changanyeni na za kwenu...wanaowaambia msusie hawawatakii mema..wanataka mpotee jumla
Si kweli kwamba uhai wa Chama cha upinzani ni fedha tu,kumbuka upinzani ni roho isiyokufa kamwe.Hata dunia nzima tukifa,upinzani utaendelea kuishi daima.Hata hivyo CHADEMA kikifa kwa namna unavyojaribu kutuaminisha nadhani itakuwa vizuri sana kwa sababu tumeambiwa watauza nchi kwa mabeberu,zaidi sana wanakwamisha maendeleo.Je,upo tayari kuona Tz yetu ikiuzwa kwa mabeberu?
 
Marekani kuna kitu kinaitwa gerrymandering. Chama kilichopo madarakani kwenye majimbo wakati wa kuhesabu watu, kina mamlaka ya kuweka mipaka ya majimbo ya uchaguzi. Republicans wametumia haki hiyo kuweka mipaka ambayo inawawezesha kushinda hata kama wanapata kura pungufu kuliko Democrats. Kila walipoweza, wameweka vikwazo ambavyo vimewalenga wasio weupe na vijana kupiga kura. Kwenye uchaguzi wa gavana wa jimbo la Georgia mwaka 2018 Secretary of State wake ( aliyekuwa pia mgombeaji) aliondoa majina ya wapiga kura zaidi ya 300000 kwenye orodha ya wapiga kura wengi wao wakiwa weusi. Baada ya kufanya haya na mengine mengi ya kuwadhulumu haki zao wapiga kura wa Georgia alishinda kwa takriban kura 50000. Democrats wa Georgia hawakususa kuingia bungeni kwa sababu wameibiwa! La hasha, waliingia bungeni wakati wale ambao walikuwa nje ya bunge walifanya kampeni kubwa ya kuandikisha wapiga kura wapya. Hao ndio waliompa Biden ushindi Georgia.

Amandla...
Kwa hapa kwetu jambo la maana kabisa ni kususa au kujitoa kabisa ibaki CCM peke yake ambayo haiuzi nchi kwa mabeberu,wengine tupige kazi.
 
Back
Top Bottom