CCM hawana mamlaka ya kutoa viti maalum. Hivi ni viti ( bila shaka wanastahili zaidi ya hapo) ambavyo ni stahili ya CHADEMA na vimetokana na kura walizopigiwa. Sio fadhila ya NEC wala CCM. Aidha ruzuku haitoki kwenye mfuko wa CCM bali inatokana na kodi ambazo wananchi wote wanachangia bila kujali itikadi yao. Sio fadhila, ni haki yao na wanastahili kulipwa ili waendeshe shughuli zao. Kusema kuwa wakipokea watageuka kuwa ni chama "ruzuku" ambacho hakijali "principles" ni upuuzi maana wakati hao unaowanyooshea vidole wanafilisiwa, wanapigwa, wanafunguliwa kesi za kutungwa, wanapofungwa, wanapopigwa mabomu, wanapodhalilishwa na vijana wadogo ambao madaraka yamewafanya wakose adabu, wanafukuzwa bungeni, wanapozuiwa kufanya kampeni, wanaponyimwa stahili zao n.k. wewe shujaa na wenzako kama wewe wenye "principles" hamkujitokeza kusimama nao.
Badala yake mnajificha kwenye majukwaa kama haya na kujimwambafai. Mngekuwa mnasimama nao toka mwanzo hali isingefikia hapa. Polisi wangejua kuwa wakimgusa mmoja wao kwa uonevu mngejitokeza kwa wingi, wangeacha kuwabughudhi. Mngesimama kidete kuhakikisha haki inatendeka kwenye vituo vya kupigia kura sio wasimamizi wala NEC ambao wangethubutu kufanya waliofanya.
Wakina Salome Makamba, Pendolino Peneza, Suzan Kiwanga, Nusrat na wengine wengi tu wametupwa ndani au wamenyang'anywa haki yao ya kugombea lakini nyinyi wenye " principles " ambao mko tayari kufia chama mliufyata. Waacheni ambao wameonyesha kwa matendo kuwa ni watetezi wa wananchi na chama chao wapewe nafasi ya kuendelea kufanya. Mkitaka wasifanye hivyo , nyie Great Thinkers, anzeni kuwaonyesha kwa matendo kuwa mko pamoja nao. Kama hamuwezi, nyamazeni.
Amandla...