Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Wajitafakari, je wao ni chama cha siasa au kikundi cha wanaharakati?

Chama cha siasa lengo lake ni kupata fursa ya kuunda serikali. Kwahiyo kuwa Bungeni ni muhimu sana katika kufikia lengo hilo. Chama cha siasa au mwanasiasa hutegemewa kuwa flexible kutegemeana na hali halisi ya wakati husika ili aweze kutimiza lengo lake.

Kikundi cha uanaharakati kinakuwa na agenda moja au chache kinachozipigania. Hakiwezi kukubali kubadilisha msimamo kwenye masuala yoyote yanayoingiliana na agenda hiyo.

Kwahiyo mwanasiasa hujifunza mazingira yalivyo na kutafuta mafanikio bila kulazimika kubadili mazingira. Mwanaharakati hutumia nguvu na maarifa yake yote kubadili mazingira ili agenda yake itimie.

Kama Chadema ni chama cha siasa, hakiwezi kususia Bunge.
Siasa nje ya bunge huwa zinagoma kufanyika?
 
Ujinga ndio utafanya wasimangwe.

Ile tabia ya kutoa hoja kwa ukali na hisia kubwa hadi mtu anapoteza hekma ya maneno,ndicho kinacholeta shida.

Pia tabia za kutoka bungeni,inaweza kuwa ni haki yao na wanaitekeleza kujitenga na matumizi mabaya ya madaraka ya bunge kutunga sheria kandamizi,ila wanajua jinsi ccm wanavyonufaika na ujinga wa watanzania katika hili?
Wanajua kuwa kuna wananchi wengi hawajawahi kuwaelewa hicho wanachokifanya simply tu sababu ya ujinga mwingi uliopo kwa wananchi wetu?

Mara zote hoja ya ukweli,ukiiongea kistaarabu,ukashauri kiungwana,haiwezi kufutika katika masikio ya unayemshauri.
Hata wananchi wanaelewa sana hoja za namna hii kwa kuwa zina kwenda sambamba na tabia na utamaduni waliozoea watanzania wa kuamini amani ni upole hata katika kutoa hoja.Ukifoka hata kama unaongea ukweli mtupu haueleweki.


Mwisho waachane na hoja za kizushi zinazotokea kwa sababu ya uvumi tu au zilizoasisiwa na wana ccm wenyewe ili kufitiniana halafu wapinzani mnazidandia.Mfano hoja ya Lowasa kuwa ni fisadi iliasisiwa na wana ccm wenyewe kwa ajili ya vita ya uwaziri mkuu.Wakaleta hoja kwa upinzani,nao wajajimilikisha hoja hiyo ila baadae wakalazimika kula matapishi yao
 
Chadema iwapo itapeleka wabunge bungeni baada ya ujinga wote huu uliotokea maana yake imeiunga mkono CCM katika udhalimu wake, nayo itakuwa haina uhalali wowote mbele ya umma kudai reforms zozote za msingi katika nchi
Kwakweli wakishindwa kuliona hili, basi watakuwa wamejimaliza kisiasa.
 
Nawaambia angali mapema kabisa kuwa, mkiwa tayari kupeleka wabunge katika Bunge hili, basi pia muwe tayari na masimango kama vile bila huruma ya Raisi au Spika,wengine msingekuwa humu ndani, tumewabeba, hamna shukurani na kauli zingine za aina hiyo pale mtapopishana nao mitazamo ndani ya hilo Bunge.
Hujui hata utaratibu
Majina yanatakiwa kufika time,mapema zaidi kabla uchaguzi
Itakachofanya tume no kupiga mahesabu kutokana kura mlizopata,kwa mfano hesabu zikisema mnapata wabunge watano,tume itachukua wa Kwanza Hadi wa tano kwenye listi mliowatumia,itawateua
Kazi itakua kwenu kuwafukuza chama
Kumbuka huwezi kumpoka ubunge kirahisi mwanachama wako
Tulieni tu mjijenge sio lazima mbowe na lema wawe wabunge
 
Kuna mnyukano huko wa hatari kina Matiko, Mdee, Bulaya, Magelesi and the likes wameunda women wing kushinikiza kamati kuu kuwaruhusu wateuliwe na kushiriki bingeni kama viti maalum, vinginevo wakiwahama wasilalamike.
We ulisikia wapi.
 
Kama Watanzania hawataki kuandama maana yake hawaikubali hiyo agenda ya CHADEMA. Hakuna wafuasi. Demokrasia maana yake wengi wape, kama Watanzania hawataki kwa nini uwaingize mabeberu? Kumbuka mtu anayekusaidia kwa masharti si mtu mzuri. Hakuna kitu kibaya kama misaada ya masharti. Ndiyo maana TZ imeamuwa kutegemea zaidi pesa za ndani kwenye maendeleo kuliko misaada anbayo mwisho wake ni manyanyaso. Hao wakubwa wanalijuwa hili na wameisha msoma Magufuli, kwa hiyio ni waangalifu saana kwenye hili.
Ingekuwa viongozi wa Chadema na ACT Wazalendo hawajakamatwa usiku wa kuamkia maandamano , jeshi la polisi limeahidi kulinda haki yao ya kuandamana na wanajeshi wamebaki kambini halafu watu wasiandamane ndio tungeweza kusema kweli wamekataliwa.

Amandla...
 
Zile 330 + million kila mwezi ( X 60 ) kwa miaka mitano matokeo yake ni kupanga tu hapa chini .... .. .

View attachment 1621784
Why ujauliza chopa imelipwa vipi kufanya kazi ya kampen?

Why ujauliza Yale magari yananunuliwa na pesa zipi?

Nyie ccm office mpya ya chama mliojenga kwa ruzuku zenu iko wapi?
 
Kama mnufaika wa ruzuku ni mwenyekit na kazi Hana mpaka miaka mitano tusubir muda tu utaongea lazima wabunge wa vit maalum wateuliwe Sasa nyie makamanda kuwen Makin Sana na uzi zenu isije kua aibu apo baadae

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kama mnufaika wa ruzuku ni mwenyekit na kazi Hana mpaka miaka mitano tusubir muda tu utaongea lazima wabunge wa vit maalum wateuliwe Sasa nyie makamanda kuwen Makin Sana na uzi zenu isije kua aibu apo baadae

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Kama unadhani Mbowe kipato chake kinatokana na ruzuku basi haumjui.

Amandla...
 
Kitu cha muhimu kuliko vyote ni kuwashirikisha ACT-Wazalendo katika maamuzi yao. Pamoja na kwamba ninashauri wachukue ruzuku na viti maalum ( ambazo sio fadhila bali ni haki yao) ni lazima waelewe machungu ya wenzao waliyoyapata pia. Chadema wanawahitaji ACT-Wazalendo ili kuweza kushinda huu mpambano.

Amandla...
 
CCM hawana mamlaka ya kutoa viti maalum. Hivi ni viti ( bila shaka wanastahili zaidi ya hapo) ambavyo ni stahili ya CHADEMA na vimetokana na kura walizopigiwa. Sio fadhila ya NEC wala CCM. Aidha ruzuku haitoki kwenye mfuko wa CCM bali inatokana na kodi ambazo wananchi wote wanachangia bila kujali itikadi yao. Sio fadhila, ni haki yao na wanastahili kulipwa ili waendeshe shughuli zao. Kusema kuwa wakipokea watageuka kuwa ni chama "ruzuku" ambacho hakijali "principles" ni upuuzi maana wakati hao unaowanyooshea vidole wanafilisiwa, wanapigwa, wanafunguliwa kesi za kutungwa, wanapofungwa, wanapopigwa mabomu, wanapodhalilishwa na vijana wadogo ambao madaraka yamewafanya wakose adabu, wanafukuzwa bungeni, wanapozuiwa kufanya kampeni, wanaponyimwa stahili zao n.k. wewe shujaa na wenzako kama wewe wenye "principles" hamkujitokeza kusimama nao.

Badala yake mnajificha kwenye majukwaa kama haya na kujimwambafai. Mngekuwa mnasimama nao toka mwanzo hali isingefikia hapa. Polisi wangejua kuwa wakimgusa mmoja wao kwa uonevu mngejitokeza kwa wingi, wangeacha kuwabughudhi. Mngesimama kidete kuhakikisha haki inatendeka kwenye vituo vya kupigia kura sio wasimamizi wala NEC ambao wangethubutu kufanya waliofanya.

Wakina Salome Makamba, Pendolino Peneza, Suzan Kiwanga, Nusrat na wengine wengi tu wametupwa ndani au wamenyang'anywa haki yao ya kugombea lakini nyinyi wenye " principles " ambao mko tayari kufia chama mliufyata. Waacheni ambao wameonyesha kwa matendo kuwa ni watetezi wa wananchi na chama chao wapewe nafasi ya kuendelea kufanya. Mkitaka wasifanye hivyo , nyie Great Thinkers, anzeni kuwaonyesha kwa matendo kuwa mko pamoja nao. Kama hamuwezi, nyamazeni.

Amandla...

Sasa solution ya uonevu huo ni ama kupambana ili uondoke, au kama huwezi kupambana acha siasa, unga mkono juhudi, au hamia CCM lakini usilazimishe chama chote kihalalishe haramu.

Unataka waende bungeni kwa mgawo wa viti vinavyotokana na uchaguzi feki?.

Yeyote anayeona safari ya kupigania haki imekuwa ngumu, basi atoke tu kwa heshima, ajikalie pembeni. Bora askari 10 walio committed kuliko 100 wasio na moyo wa mapambano

Viti maalum na ruzuku ni haki yao kama uchaguzi ni halali lakini siyo haki yao kama uchaguzi ni feki uliojaa kila aina ya uonevu, ghilba, makandokando etc.

Huwezi kutoa statement ya kutoutambua uchaguzi, halafu uwe wa kwanza kutaka kunufaika na uchaguzi huo. Huo ni Ujinga au unafiki wa kiwango cha kimataifa!
 
Hujui hata utaratibu
Majina yanatakiwa kufika time,mapema zaidi kabla uchaguzi
Itakachofanya tume no kupiga mahesabu kutokana kura mlizopata,kwa mfano hesabu zikisema mnapata wabunge watano,tume itachukua wa Kwanza Hadi wa tano kwenye listi mliowatumia,itawateua
Kazi itakua kwenu kuwafukuza chama
Kumbuka huwezi kumpoka ubunge kirahisi mwanachama wako
Tulieni tu mjijenge sio lazima mbowe na lema wawe wabunge
Yaani nimeamini CCM ni wehu kabisa , yaani uvuruge uchaguzi , uibe kura , uzuie mawakala , uue , ujeruhi , ubambikie kesi wapinzani , uteke , umwage damu ilu upate ushindi, umshinde mpinzani wako kwa kuwatoa roho ili ubaki peke yako , wewe huyohuyo tena uanze kuwalazimisha uliowazuia kushinda kuwapa ubunge , sijui viti maalum , sijui Zanzibar uwalazimishe kushiriki serikali ? Huu sio wehu? Kila siku nawaambia kuna mtu anaumwa bipolar disorder , kichaa kabisa , sifa yoyote ya mtu mzima ni kuchagua maneno ya kutamka na kutenda CCM ni wehu yaani kumbe wana shida sana na madaraka mpaka wamwage damu za watu .
IMG_20201027_223505.jpg
 
Why ujauliza chopa imelipwa vipi kufanya kazi ya kampen?

Why ujauliza Yale magari yananunuliwa na pesa zipi?

Nyie ccm office mpya ya chama mliojenga kwa ruzuku zenu iko wapi?
Hizo ndio sababu tosha kwamba Watanzania hawawapi kura kwa sababu ya ubinafsi wenu.
 
Akili zako ndio zimeishia hapo
Hauna hoja,

Nenda huko fb ukaongee na watoto wenzako
Na wewe hoja zako ni zipi? Kutajirisha kikundi cha Mbowe, Membe na Zito? Khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Na wewe hoja zako ni zipi? Kutajirisha kikundi cha Mbowe, Membe na Zito? Khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Kama serikali inawatambua Hao watu ww ni Nani Mpaka ujifanye una akili Sana?

Kwani ccm hakuna matajiri?
Wale wakina Rostam, Asas, wale ni maskini?

Huna hoja
 
Back
Top Bottom