Umoja na mshikamano UPI?
Kama Akishinda Mtanzania aliyegombea kwa Chama Cha Chadema akishinda hatangazwi bali anatangazwa Mtanzania mwngine wa CCM , yaani umoja gani kama hata Mtoto wa maskini Mtanzania mwenzetu akishinda hatangazi bali ni bora atangazwe Mhindi toka Bombay alimradi amepitia CCM , umoja unatakiwa uanzie kwenye Kumpata rais asiye mbaguzi kwa misingi ya itikadi za vyama.
Amni amni amini nakuambia itaichukua miaka hata 10 tena kwa CCM kuunyamazisha na kuuangamuza kabisa upinzani kwa kutumia damu za watu lakini Roho ya ubaguzi haiishi mana ni kati ya ibada za shetani za kumtukuza mwanadamu kwa ahadi za fahari za dunia yakiwemo madege,majumba,mameli ,magari mazuri ya seriakali ya kidunua ,mabarabara yanayopendeza ,wanyama kuzagaa mapaka mijini alimradi binadam maskini waliowengi wao wanaishi kwa jasho lao LA damu huku mabwana wakubwa wakipita na mapesa mengi na fahari za kila aina.
Wakikamilisha zoezi la kuwabagua watu kwa vyama vyao watahamia kwenye Dini. Usione Gwajima akitekua anauandama uislam ,Kikwete na CCM na kujifanya kuwa hana Chama Leo anagombea kupitia CCM yenye Rais aliyepita mikoni mwa CCM ,lengo litatimia endapo upinzani utatoweka. Watawagandamiza watu kwa dini zao mana watafanya matendo yatakayopingwa na imani za dini , wataanzana na dini isiyofanana na imani yao , watashangiliwa kuwa wanaimarisha amani ya nchi na umoja. Wakiwamaliza na kuwatia hofu wa dini Inayopingana nao watahamia kwenye Ukabila kwa kanda ,watawamaliza ,baadae watafanikiwa kuwatia hofu watu wa kanda nyingine ili kanda moja itawale kanda nyingine ndio maana hawataki utawala wa majimbo , watafanikiwa na kuifanya Zanzibar kuwa mikoa miwili tu. Baadae watagundua kuwa kumbe kanda waliyoitumia kuangamiza nyingine nayo ina makabila korofi watawaangamiza wale wanaoonekana Korofi , kwenye makabila mengine ,mwishowe watabaki watawala wa Ukoo mmoja. Hivyo ndivyo Utawala wa Kifalme unavyokuwa ili udumu milele.
Ni jukumu letu watanzania kufuata utawala unaoruelekeza kwenye utawala wa kifamilia au kujenga Demokrasia ambapo hata mtoto yatima anaweza kuonyesha Uwezo wake wa kuongoza na akawashawishi wananchi wa vyama vyote wakampa kura na kumshinda mtoto wa Waziri mkuu na akatangazwa kuongoza watu wote kwa haki na kwa kufuata sheria na katiba.
Kwa sasa ndani ya CCM ya leo wagombea wengi ni watoto au ndugu wa watawala waliopo au waliopita ambao kiukweli kwao suala la uchumi wa kuendesha familia zao sio tatizo hata kidogo tatizo lao ni uwezo wa kuongoza kwa misingi ya katiba na sheria na pia uwezo wa kuleta fikra mpya zinazowagusa wananchi maskini moja kwa moja!! Kwao tatizo ni usafiri wa ndege ,treni za mwendo kasi , maofisi yenye viyoyozi, magari ya kifahari n.k. Tofauti na watoto wa maskini ambao mpaka leo wakiona hata chupa ya maji ya uhai imetupwa wanaiokota na kuona ni chombo kizuri cha kwenda kuhifadhia Mafuta,maziwa n.k. Wakipinga mawazo ya watoto wa matajiri na watawala wanapelekwa Polisi na kubambikizwa kesi ngumu ngumu ili kuwatia hofu mana familia zao hazina hata chakula cha kesho.
Kuna watu wanadhani kujenga utawala wa kidikteta ni jambo la kuwapa watu maisha mazuri au kuwapa tende na halua , hapana udikteta unajengwa kwa nguvu, udikteta unajengwa kwa kuwamiminia watu mvua za mabomu na risasi. Udikteta ni utawala mbaya sana. Ni utawala wa walioshiba kutaka kushiba wao tuu huku wakiwaambia wenye njaa vumiliani tu kwani njaa ya siku moja haiui.
CCM wanajiita wapenda amani ,tuwaulize je, wapo tayari kukaa pembeni na kuifurahia amani nje ya madaraka ??
Kwa nini wao amani ni pale wanapokua madarakani tuu lakini wakitoka amani itoweke?
Nani ataondosha amani kama sio wao ambao hawapo tayari kukaa pembeni na kuongozwa kama walivyoongoza wao??
Hivi nani ambaye hajui kuwa wanaomwaga Damu za watu kule Libya ni wale waliokuwa watawala ? Familia na Ukoo was Gadaff hawakuwahi kamwe kuishi maisha ya kawaida , walikimbia na silaha za serikali kwa kuwa wengi ndio waliokua wamekalia nafasi za juu kwenye vyombo vya dola. Wanadhani wao tu ndio walioumbwa kuwatawala wengine.
Kama Demokrasia ingeleta vita basi ulaya ya Leo ingekuwa ni pori la vita. Lakini vita zote za wenyewe kwa wenyewe zinatokana na mwanya unaotokana na utawala katili wa Kidikteta kutokana na kujaa mikono inayonuka Damu jambo kinalopelekea wale waliopoteza ndugu na marafiki zao kuamua kushirikiana na wageni toka nje kwa ajili ya kulipa viasasi.
Kama kuna Demokrasia ya kweli basi kila MTU anaiona nchi yake kuwa ni mahali salama na penye fursa za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Leo hii Tanzania hasa Zanzibar fursa za kisiasa,kiuchumi na kijamii zipo upande wa CCM tuu. Sasa hapo nani anayeondoa amani na umoja wa watu ,je, ni wageni toka Ulaya au ni viongozi wa CCM wanafanya kazi kwa jeuri ,kiburi na dhulma kwa sababu ya kuwa na uwezo wa kuvituma vyombo vya Dola kufanya chochote wanachotaka??