Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuketi kikao maalum Jumamosi (20/03/2021). Yatangaza siku 21 za maombolezo

Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuketi kikao maalum Jumamosi (20/03/2021). Yatangaza siku 21 za maombolezo

Wajumbe wa kamati kuu ni akina nani? Tukumbushane.
Kwa mujibu wa ibara ya 108 ya katiba ya ccm wafuatao ni wajumbe wa kamati kuu
Mangula
Shein
Samia
Mwinyi
Majaliwa
Makamu wa pili Zanzibar
Ngugai
Spika baraza la wawikilishi
Mwenyekiti na katibu wa wabunge wa ccm
Mwenyekiti na katibu wa wabunge wa ccm baraza la wawikilishi
Wenyeviti wa jumuiya za chama, uwt, uvccm na wazazi
Katibu mkuu na secretary yake.
Pinda
Makongoro

Kama kuna niliye msahau mtanisamehe.

Sasa utata ni nani ataongoza hicho kikao !!??
Mangula au Shein!!
Busara inasema the most senior ambaye ni Mzee Philip Mangula.

Katibu je !!??
Sikuona barua ya bashiru kujiuzulu, hata na hivyo tuna manaibu katibu bara na Zanzibar hivyo senior one atamsaidia mwenyekiti.

Kidumu chama tawala
 
Kamati kuu ya CCM itakutana kwa dharura tarehe 20/03/2021 siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mwenyekiti ndugu Magufuli.

CCM imetangaza siku 21 za maombolezo sawia na tangazo la serikali.

Source Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!
Tangazo la serikali kuhusu siku za maombolezo ya kitaifa limerekebishwa?
 
Taasisi haiwezi kutekeleza, yawezekana maombolezo yalianza muda sio kila kitu ujue!.
Death certificate ya JPM ni 17th March 2021, waombolezaji ni wananchi wewe na mm, katiba inasema siku 21.... haya basi achana na ya Samia, Polepole kashasahihisha milingoti ya kijani itapepea nusu sambasamba na ile Taifa kwa muda wote wa siku 21... unapingana na nn!!!
 
Poleni CCM kwa msiba wa Mwenyekiti wenu, na aliyekuwa Rais wa JMT hayati John P. Magufuli.

Mwenyezi awape utulivu na hekima; na kwa kumwogopa mutangulize, at last, maslahi ya Taifa kwenye vikao vyenu vijavyo wakati huu wa msiba. Mna wajibu mzito sana, mkiendelea kushupaza shingo zenu na kuweka u-CCM mbele basi mtalipa gharama zake ninyi na vizazi vyenu.

Narudia, nawaomba sana muwe na hofu ya Mungu na moyo wa upendo katika vikao vyenu - hasa kumpata Makamu wa Rais, kujaza nafasi ya Katibu wenu mkuu na mambo ya siasa za nchi yetu.

Haki inalifuatia Taifa letu kwa karibu na hakuna anayeweza kukimbia wajibu wake.
 
Death certificate ya JPM ni 17th March 2021, waombolezaji ni wananchi wewe na mm, katiba inasema siku 21.... haya basi achana na ya Samia, Polepole kashasahihisha milingoti ya kijani itapepea nusu sambasamba na ile Taifa kwa muda wote wa siku 21... unapingana na nn!!!
Msome tena, hujamwelewa. Kimsingi anakuonyesha kitu fulani .....usiangalie kidole angalia unachoonyeshwa
 
Kwa mujibu wa ibara ya 108 ya katiba ya ccm wafuatao ni wajumbe wa kamati kuu
Mangula
Shein
Samia
Mwinyi
Majaliwa
Makamu wa pili Zanzibar
Ngugai
Spika baraza la wawikilishi
Mwenyekiti na katibu wa wabunge wa ccm
Mwenyekiti na katibu wa wabunge wa ccm baraza la wawikilishi
Wenyeviti wa jumuiya za chama, uwt, uvccm na wazazi
Katibu mkuu na secretary yake.
Pinda
Makongoro

Kama kuna niliye msahau mtanisamehe.

Sasa utata ni nani ataongoza hicho kikao !!??
Mangula au Shein!!
Busara inasema the most senior ambaye ni Mzee Philip Mangula.

Katibu je !!??
Sikuona barua ya bashiru kujiuzulu, hata na hivyo tuna manaibu katibu bara na Zanzibar hivyo senior one atamsaidia mwenyekiti.

Kidumu chama tawala
Asante sana kwa kunijuza.....
 
Leo chama cha mapinduzi kimetoa taarifa rasmi ya kifo cha Dkt. John Magufuli ambae amekuwa mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Taarifa hiyo imesomwa na Humphrey Polepole.

========

Polepole: Chama cha mapinduzi, safu yake ya uongozi na wanachama tumepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli, mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakuu wa chama waliopo, mzee Philip Mangula, makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara na mzee Ali Mohammed Shein, makamu wa mwenyekiti wa Tanzania Zanzibar wameshaurianana kukubaliana kwamba kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa iketi kwa kikao maalum siku ya Jumamosi ya tarehe 20 ya mwezi huu Machi mwaka 2021 saa nane mchana katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Aidha taarifa inatolewa kwamba chama kitakuwa katika maombolezo ya siku 21 sambamba na tangazo la serikali, wakati wote huo bendera za chama cha mapinduzi zitapepea nusu mlingoti.

Kutakuwa na kitabu cha salam za rambirambi na maombolezo katika ofisi ya makao makuu ya CCM, 'White House' hapa jijini Dodoma lakini kitakuwepo pia kitabu cha kupokea salam za rambirambi na maombolezo katika ofisi zetu za chama

Uongozi wa chama unawaomba sana wanachama wote wa CCM, watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, watanzania wote kwa ujumla kuwa na moyo mkuu, kuendelea kuwa watulivu, kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kipekee na wa kihistoria kwa Taifa letu wa ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taarifa inatolewa pia kwamba shughuli za chama zile zihusianazo na uchaguzi ndani ya chama zinasimama kwa muda mpaka yatakapotolewa maelekezo mengine.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani ndugu John Pombe Joseph Magufuli, Amen.

Asanteni kwa kunisikiliza

Chama cha majizi ya kura mtakutana huku jizi kuu likiwa halipo!
 
Sukuma land awaamini dunia imevaa bukta.
Wale waganga njaa wa simiyu vipi kulikoni wapemba wamezidi kete.Ndumba za kwenye miti na ndumba za maji chumvi hii vita ni hatari.vuta nikuvute
Hutujui wewe naona.
 
Tupo kwenye maombolezo, ni wapi pameandikwa siku 21? Hayo ni maamuzi yako na Polepole
Ghana Jerry Lawrance alikaa miezi 6 hajazikwa sasa mnataka tusifaidi Makamu atakavyoapishwa na kufyeka Mawaziri kwa Wakuu wa Mikoa?
Fox, do not be lazy read 'The National Leaders Funeral Act', 2006
Death announcementof national leaders Death announcement of the President
8. -(1) Where the President who is in office dies, the Vice President
shall, after receiving official infonnation and confinnation ofthe death,
deliver death announcement in the manner stipulated under section 7.
(2) The Vice President shall, in respect of the late President,
announce a period of21 days for mourning and the flag to fly halfmast.
 
Chanjo wamepewa watu million 17 na walioathirika hawafiki 400!! Below 0.00% kma tu ambavyo hta tukiwapa Insulin watu laki 1 huwezi kosa watu hta buku watakaopata side effects.

Au mwenzetu tuambie ni dawa gani haina side effects kwa walau 1% ya watumiaji wote.
Mkuu mimi hiyo sio fani yangu naona tuu mataifa makubwa yakisitisha na nikiwasikiliza wataalamu wao napata kitu pia SA waliipiga marufuku na nadhani Ramaphosa inamuumiza sana kichwa hiyo dawa maana waliagiza kichwa kichwa baadae Johnson and Johnson na Aspen kudai kuwa wamemaliza tafiti na dawa yao ipo sahihi ile walioagiza haina nguvu kwa hii wave two...huku tunaona wataalamu wa great skill hospital wakiongea logic kabisa hata Kama sio fani yako unapata kitu Mkuu ni hayo tuu...
 
Fox, do not be lazy read 'The National Leaders Funeral Act', 2006
Death announcementof national leaders Death announcement of the President
8. -(1) Where the President who is in office dies, the Vice President
shall, after receiving official infonnation and confinnation ofthe death,
deliver death announcement in the manner stipulated under section 7.
(2) The Vice President shall, in respect of the late President,
announce a period of21 days for mourning and the flag to fly halfmast.
Wanajeshi (JWTZ) Ndio wame sema kuwa Ni siku 14 .hizo 21 Ni za ccm
 
Nashauri Makamu wa Rais awe Mkristo Mkatoliki na Waziri Mkuu awe Mkristo Mprotestanti au Makamu wa Rais awe Mkristo Mprotestanti na Waziri Mkuu awe Mkristo Mkatoliki.

Waziri Mkuu awe Mkenda au Kimei kuendana na kama Makamu wa Rais atakuwa Mprotestanti au Mkatoliki.

Kabudi anaweza kuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu anaweza kuwa Mkenda.

Au Lukuvi anaweza kuwa Makamu wa Rais na Kimei akawa Waziri Mkuu.

Au combination nyingine nzuri za Makamu wa Rais Mkatoliki na Waziri Mkuu Mprotestanti au Makamu wa Rais Mprotestanti na Waziri Mkuu Mkatoliki.

Bunge ndio liwe uwanja mkuu wa kufanya maamuzi haya, kwasababu uwiano wa kidini ndani ya Kamati Kuu ya CCM, hauendani na hali halisi nchini.

Halafu in the future, baada ya Rais Samia kumaliza vipindi vyake vya uongozi, tujaribu kuwa na Rais Mprotestanti, kwasababu Tanzania haijawahi kuwa na Rais Mprotestanti.

Ushauri huu usipofuatwa hakuna tatizo lolote. Maisha yanaendelea kwa amani na utulivu.
 
Back
Top Bottom