Zanzibar 2020 KAMATI Maalum ya CCM imependekeza Majina ya Wagombea 5 wa Urais Zanzibar

Zanzibar 2020 KAMATI Maalum ya CCM imependekeza Majina ya Wagombea 5 wa Urais Zanzibar

Joined
Jul 8, 2013
Posts
53
Reaction score
75
Kamati maalumu ya CCM imemaliza mkutano wake huko Zanzibar kwa kupitia majina yote wanachama waliochukua fomu. Tayari majina matano yamepatikana ambayo yatawasilishwa kwenye Kamati Kuu ya CCM itakayoketi wiki kesho pale Dodoma.

=====

KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Zanzibar leo imependekeza majina matano ya Makada wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kati ya Makada 31.

Akizungumza baada ya kumalizika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi, amesema kamati hiyo ni sehemu muhimu ya maandalizi na uchujaji wa majina ya wagombea watano wanaotakiwa kuwasilishwa katika Kamati Kuu kwa ajili ya kujadiliwa tena na kumtafuta mgombea mzuri mwenye sifa 12 zikiwemo hekima,kuaminika, kuthamini muungano na Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Mabodi amesema baada ya Kamati kuu kujadili kwa kina majina hayo matano itapendekeza majina matatu na kuyapeleka Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambayo itachagua jina la mtu mmoja ambaye atapeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar ambapo baada ya hatua hiyo mgombea huyo atapelekwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kwa ajili ya kuthibitishwa na kupata baraka za Wajumbe wote wa kamati kuu na kuendelea na michakato mingine.

Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu ulianza Juni 15 hadi 30, mwaka huu ambapo jumla ya makada 32 walijitokeza kuchukua fomu hiyo ambao ni Mbwana Bakari Juma, Ali Abeid Karume, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Mussa, Hussein Ali Mwinyi, Shamsi Vuai Nahodha, Mohamed Jafar Jumanne Mohamed Hijja Mohamed,Issa Suleiman Nassor.

Wengine ni Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, Mwatum Mussa Sultan, Haji Rashid Pandu, Abdulhalim Mohamed Ali, Jecha Salum Jecha, Dk. Khalid Salum Mohamed, Rashid Ali Juma, Khamis Mussa Omar, Mmanga Mjengo Mjawiri, Hamad Yussuf Masauni Mohamed Aboud Mohamed, Bakari Rashid Bakar, Mgeni Hassan Juma, Ayoub Mohamed Mahmoud, Hashim Salum Hashim, Fatma Kombo Masoud, Hasna Attai Masoud, Maalim Hamad Idd Hamad Idd, Pereira Ame Silima, Shaame Mcha, Mussa Aboud Jumbe na Moudline Cyrus Castico.
 
Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kimefanyika leo na wagombea watano wamepitisha kuwania nafasi ya Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020

Watano hao ni Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Prof. Makame Mbarawa, Dkt. Khalid Salum Mohammed, Khamis Mussa Omar na Pereira Silima

Kikao hicho kiliongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Juma Abdalla Juma
 
Mwenyekiti Taifa kutoka Dodoma safari hii hakuingilia mchakato wa wanaCCM Zanzibar ?
 
Mbona wanajulikana tu hao tatu bora hata kabla ya kutangazwa
 
Hakuna kama jecha!
masoudkipanya_CBuWuTVjcwz.jpg
 
Back
Top Bottom