Zanzibar 2020 KAMATI Maalum ya CCM imependekeza Majina ya Wagombea 5 wa Urais Zanzibar

Zanzibar 2020 KAMATI Maalum ya CCM imependekeza Majina ya Wagombea 5 wa Urais Zanzibar

Sijaona wa kusimama ulingo wa siasa na Maalim Seif hata mmoja hapo! Yaani hata waamue CCM kuwasimamisha wote watano dhidi ya Seif, watagaragazwa labda watumie Jecha style kama zamani
 
Wamefanya kuwa ni siri, majina hayo yatajuulikana huko huko Dodoma. Kiufupi Zanizibar hawana mamlaka hata yakutangaza hayo majina waliyoyachagua.
Na hilo linathibitisha jinsi walivyo kubali kukaliwa vichwani na sisi watuitao CHOGO
 
Utawala wa kifalme Zanzibar umeanza kunukia kwa mara nyingine.

Dkt mwinyi anaendwa kukatwa Dodoma.. ameekwa hapo kuvuruga mind zisijue mhusika mkuu.. ni kama fake no 9... alivyowekwa membe 2015..
 
Yule General hayumo?

Yupi huyo ?

Juni 18, 2020
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Unguja, Zanzibar
Tanzania

Wasifu wa mtia nia Urais SMZ 2020

Balozi Major General (retired) Issa Suleiman Nassor achukua fomu kutia nia Urais SMZ 2020

Hili ni jina geni katika masikio ya wengi panapohusika siasa za Tanzania, lakini sio geni katika uwanja wa kijeshi. Major General Issa S. Nassor alifikia ngazi ya Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa JWTZ (Head of training and operations of the Tanzania People’s Defence Forces TPDF)

Jenerali Nassor amelitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa miaka mingi kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi nchini Misri kutoka mwaka 2017 hadi 2019. Makao yake yakiwa Cairo, Misri huku pia akiiwakilisha Tanzania katika nchi za Lebanon, Palestine, Libya, Iraq, Syria na Jordan. Major General Issa Suleiman Nassoro aliwahi pia kuhudumu ktk Ubalozi wa Tanzania nchini India kama Defence Attache ubalozini kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wetu nchini Egypt (2017-2019).

Picha toka maktaba:
Oktoba 5, 2017.

Baada ya kuapishwa kwa Balozi wa Misri H.E. Major General Mstaafu Issa Suleiman Nassor, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais John Pombe Joseph Magufuli na Mkuu wa Majeshi General Venace Mabeyo, Ikulu Dar es Salaam 05 October 2017.

Japo si jina kubwa katika siasa, duru visiwani Zanzibar zinamuelezea kama mtu asiye na mafungamano na siasa za makundi.

Naye anatajwa kubebwa na karata ya utiifu wake lakini hana umaarufu katika siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Hatima ya nafasi yake ikiwa ataingia katika kinyang'anyiro itaamuliwa na CCM yenyewe.
 
Yupi huyo ?

Juni 18, 2020
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui...
Huyo General ni mzuri katika mambo ya uongozi kuliko wote waliotia nia ; anajua sana kuongoza ingawa inawezekana hajui siasa. Kiongozi mzuri aliyekuwapo kwa Zanzibar kipindi hiki alikuwa huyo.
 
Kama Jecha hayumo, watakuwa hawajamtendea haki. Uzalendo wake wote ule?

Itakuwa kudhihirisha ule usemi wa shukurani ya punda kweli ni mateke.
PEREIRA SILIMA YUKO KICHAMA ZAIDI NA NEUTRAL HAMA MAKUNDI
 
Rais: Makame M. Mbarawa
Makamu wa Pili wa Rais : Issa Selemani Nassor/ Pereira A. Silima
 
Wakati ni ukuta, mfukuto kati ya chaguo la Wanzabari vs Chaguo la Wabara. Njia nyeupe kwa Maalim Seif.
Hata mgombea wa urais akiwa mwakyembe,Sefu hawezi kuwa Rais Zanzibar
 
Wakati ni ukuta, mfukuto kati ya chaguo la Wanzabari vs Chaguo la Wabara. Njia nyeupe kwa Maalim Seif.
Wasioona mbali,wasiojua kusoma nyakati na wenye chuki na Seif ambapo CCM imesahau ndio watakao tilia shaka muono wako.
Ukweli ni kuwa chama tawala safari hii kimekusudia kuionesha dunia kuwa Tanzania demokrasia inawezekana na wawache kuendelea kuleta shutuma za ukandamizaji.

Seif atakapoingia hatokuwa na visasi na atakuwa na hamu kubwa ya serikali ile iliyovunjwa ya umoja wa kitaifa.Hivyo katika hayo majina matano atakayekuwa mgombea au vyenginevyo atakuwa na timu bora ya kufanya nao kazi isipokuwa mtu mmoja tu hapo hachukuliki.
 
Hata mgombea wa urais akiwa mwakyembe,Sefu hawezi kuwa Rais Zanzibar
Kwa sabab seif anafifisha upinzan visiwan na ndio maana Mara zote akichipua mpinzan wa kweli visiwan anapotea,Bila seif visiwan chama la wana lingekua na hali tete Zaid ya hii tunayoishuhudia sabab siasa za kule Ni za kihafidhina.
 
Jecha Salim Jecha hakukumbukwa kabisa! Kati ya wale akina mama waliojitokeza kwenye mchakato, yaani alikosekana hata mmoja tu wa kuingia kwenye hiyo 5 bora!

Bila shaka mfumo dume na udini vimetamalaki sana Zanzibar.
mfumo dume ndio mfumo sahihi ulimwenguni. Hayo mambo sijui ya kiliberal yafanye kwenye familia yako.
 
Khamis Mussa. Hao wanataaluma watatu ningewarudisha vyuoni kwenye fani zao walizobobea
Pamoja na taaluma zao wamefanya nini? Uadilifu ndio kiwe kigezo sio taaluma. Maana tumeona na taaluma zao wameishia kufisidi nchi. Wametajirika wakiwa serikalini. Huku Zanzibar bora Magufuli awe rais wetu, wangekoma hawa watu
 
Imbhonelakule (Nimekuonea Mbali)
Kundi Lililomsumbua Hayati Nkurunziza
😁😂😅😄😃😃
Maana ya Imbonelakule si "Nimekuonea mbali" Bali "Waona mbali". Kiufupi ili u qualify kuitwa Imbonelakule lazima uwe na kipaji Cha Sixth sense, uwe na uwezo wa kuona/kunusa mambo kabla hayajatokea.
 
Back
Top Bottom