Kamati ndogo suala la posho yaundwa! Mbowe ndani!

Kamati ndogo suala la posho yaundwa! Mbowe ndani!

mbowe kategeshewa mtego wa panya,namshauri aweke msimamo wa kushusha zaidi hiyo posho hadharani,wenzie wakikomalia laki 7 ajitoe
 
Hivi wewe unamuona mbowe kama nani endeleya kumtukuza mimi kwangu paka tu mlafi wa wanyonge nani amekwmbia anauruma na wa tz kama kweli yeye anauruma angelianza ma ndani ya bunge kukata posho je kwenye bunge lakatiba mtu huyo unaemuwamini ataweza kupinga posho isiongezwe?
 
Pocible ndo nn.
Hebu nenda zako facebook kwa watoto wenzako
 
Hawezi kukubali jamaa mwenyewe naye HANA njaa

acha mahaba ya kingese, muulize mkono na rostam kama hana njaa..........na kwa nn alambe hata hiyo sitting allowance wakati ni sehemu ya majukumu yake ya msingi kama mbunge??!!
 
Kwani Mbowe ndio anaongea posho? Ole wenu mliochagua magamba

hakuna cha magamba wala magwanda, wote lao moja........mbona hatuwasikia hao magwanda wakiipinga hiyo posho?! ukiondoa chuki binafsi, ni zito tu alionesha uzalendo!!
 
Mwenyekiti wa muda wa ‪Bunge La Katiba ‬ameunda kamati ndogo ya wajumbe 6 kuchunguza suala la malalamiko ya posho juu ya bunge hilo la katiba.
Wajumbe wanaounda kamati ya kuchunguza posho ni Lukuvi, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Mohamed Aboud, Asha Makame na Jenista mhagama.
Eee kumekucha, hiyo ni kamati ya ngedere kuchunguza tuhuma za nyani kuiba mahindi.
 
Nafikiri wanatupotezea tu kodi yetu.Hatuhitaji hata hiyo katiba ya wanasiasa.Tubaki na ile ile ya zamani.Hao wabunge warudi tu kwao hawana maana hata kidogo.
 
Na. Robert Lengeju
Morogoro Vijijini.

Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalumula katika, Pande Ameir Kificho ameunda tume maalumu ili kuchunguza, kujadili na baadaye kutoa maoni na ushauri kwa Serikali, kama posho ya shilingi milioni Tisa kwa mwezi inatosha au haitoshi. Kamati hii bila shaka itapewa bajeti yake, si ajabu nikasikia hata wamesafiri kwenda Namibia kuona kule wabunge wa Bunge maalumu la katiba walilipwa kiasi kiasi gani. Huu mzaha na matusi ya nguoni kwa mtanzania anayeishi chini ya dola moja!


Taasisi kadhaa ikiwepo Jukwaa la katika, tahariri za magazeti, taasisi za kiraia na wananchi kwa ujumla wametoa kauli zinazoonyesha wamekasirishwa na tama ya watanzania wenzao, ambao juzi walikuwa wanaishi wote chini ya dola, na leo kwa "cheo cha ubunge" ghafla laki tatu haziwatoshi!Naungana na watanzania wote wenye mapenzi mema kulaani kwa kiwango cha juu mno mwenendo huu ulioanza kuonyeshwa mapema mno na hawa tunaoatarajia watuletee katiba mpya.


Nimeshtushwa sana kusikia majina ya walioteuliwa kuingia kwenye hiyo tume haramu. Naiita tume haramu kwa sababu kisheria, mjadala wowote ambao mada yake ni uhalifu, ni mjadala haramu. Wajumbe wa kamati hii haramu ni Freeman Mbowe, William Lukuvi, Jenester Mhagama, Paul Kimiti,Asha Baka Makame na Mohamed Aboud. Sikusahau kuwataja kwa kuanza na Mheshimiwa, nimeondoa makusudi sifa hiyo kwani kwa kukubali kwao kuwa wajumbe wa kamati haramu mimi nimewaondolea sifa hiyo na wakieendelea na mjadala wanaendelea kuporoposha hadhi yao mbele ya jamii. Hapa ndipo ninapowakumbuka wanasiasa wa Kaliba ya Dr.Wilbroad Peter Slaa, Mh.James Mbatia, Mh. ZittoKabwe na Mh. Deo Filikunjombe. Nina uhakika, yeyote kati ya hawa angeteuliwa katika kamati ya namna hii wangekataa uteuzi huo.


Hoja yangu ni hapa ni hii, kwamba suala hilo halihitaji mjadala wala tume. Wale wanaaaona hiyo pesa haitoshi waache hiyo kazi, wapewe watu wengine. Wako huku mtaani watu wenye weledi na uchungu na nchi hii, ambao wanaweza kufanya hiyo kazi kwa kuhakikishiwa usfiri, chakula na malazi pekee, na wengine kwa kujitolea kabisa. Hii nchi imeshateswa na kujeruhiwa mno na sanaa hizo zinazoitwa ‘tume'. Hivi kuna haja ya kuunda tume kwa mfano, ya kujadili kama wabunge waruhusiwe kuvuta bangi bungeni? Kuna haja ya kuunda tume ya kujadili kama wabunge waingie bungeni bila nguo? Ikiundwa kamati ya namna hiyo nawe ukakubali uteuzi wake tukuweke kundi gani? Ni kwali tunahitaji mjadala kujua bangi inafaa au haifai?


Tumewapeleka bungeni kujadili rasimu na kutuletea pendekezo la katiba bora, na juzi ilikuwa siku ya kutunga kanuni za hilo bunge, ninyi mnaacha kutunga kanun, kazi tuliyowatuma, mnaunga kamati za kuongezana posho? Mungu awalaani. Juzi tu tulikuwa wote katika harakati za kudai vitanda viongezwe kule Amana kwakuwa wajawazito 12 wanachangia kitanda kimoja na wengine wakilala chini, leo nyie laki tatu ni vijisent?


Hivi hamjui hapo Dodoma kuna walimu wanalipwa 170,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na 5,500 kwa siku? Hamjui kuwa nchi hii ina machinga wanaozunguka mkoa mzima na kuambulia kuuza chupi ya 700 kwa siku? Hamjui kuwa kuna wenye akili timamu lakini wameamua kuokota makopo yanayowapatia ujira wa 1,000 kwa siku? Hivi mmetembelea soko la Dodoma muone wamama wanaouza bamia, hoho na sukumawiki ambao pato lao kwa siku ni shilingi 2000 huku wakiendesha familia? Hebua acheni unyang'anyi huo……..


MBOWE NA WENZAKO VUNJENI HIYO KAMATI KABLA NGUVU YA UMMA HAIJAWARUDIA WENYEWE! HAMNA MAMLAKA YA KUJADILI NAMNA YA KUWANYONYA WANANCHI!
 
Naomba kufahamu mlipaji wa posho na marupurupu mengine kwa wajumbe (wabunge) hawa wa bunge maalumu la katiba. Nilivokuwa nafahamu mie ni Ikulu kwa maana ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye mlipaji sasa serikali ya Mapindizi ya Zanzibar imepata wapi mamlaka ya kuidhinisha nyongeza ya posho kwa wajumbe/wabunge toka Zanzibar?

Hebu soma hii

"Sakata la posho na fedha za kujikimu kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, limezua kizaazaa ndani na nje ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya baadhi ya wajumbe wa Tanzania Bara kulalamikia posho ya Sh. 300,000 kuwa ni ndogo. Kizaazaa hicho kiliibuka baada ya wajumbe wa Tanzania Bara kupata taarifa kuwa wenzao wa Baraza la Wawakilishi, wanalipwa kiasi sha Sh. 420,000 kwa siku.

Walidai kuwa baada ya kufika Dodoma, wawakilishi walilalamika kwa Spika wao na kuwasiliana na Serikali ya Zanzinar na kukubali kuwaongezea malipo.
" Source Voice of Zanzibar.
 
Naomba kufahamu mlipaji wa posho na marupurupu mengine kwa wajumbe (wabunge) hawa wa bunge maalumu la katiba. Nilivokuwa nafahamu mie ni Ikulu kwa maana ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye mlipaji sasa serikali ya Mapindizi ya Zanzibar imepata wapi mamlaka ya kuidhinisha nyongeza ya posho kwa wajumbe/wabunge toka Zanzibar? Hebu soma hii "Sakata la posho na fedha za kujikimu kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, limezua kizaazaa ndani na nje ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya baadhi ya wajumbe wa Tanzania Bara kulalamikia posho ya Sh. 300,000 kuwa ni ndogo. Kizaazaa hicho kiliibuka baada ya wajumbe wa Tanzania Bara kupata taarifa kuwa wenzao wa Baraza la Wawakilishi, wanalipwa kiasi sha Sh. 420,000 kwa siku.
Walidai kuwa baada ya kufika Dodoma, wawakilishi walilalamika kwa Spika wao na kuwasiliana na Serikali ya Zanzinar na kukubali kuwaongezea malipo
." Source Voice of Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar naye ana mamlaka kwenye nchi yake. Hivi unajua nani anaidhinisha malipo ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi?

Hapo ni kama nchi mbili zinakutana kujadili, hawa wakiwa na posho toka kwao na pia wanakuja kulamba za kwetu! Wazanzibar bwana Chao Chao Chetu Chao.

 
Wajinga sana kwanza dodoma wamekwenda na champion bus nauli elfu 12000 wamefika muke ndani kukalia kiti chekundu wanajiona bab kubwa swain
 
Muanzisha Mada utoto unakusumbua. Laki 3 ni kiadsi kidogo kwa gharama za dodoma. Ukikua utanielewa
 
Wakuu,

Hiki ndicho tulichokuwa tunakisubiria tokea jana kujua msimamo wa Mwenyekiti wa CHADEMA Kamanda wa Anga Mheshimiwa Freeman Mbowe kuhusu posho.

Kama mtakumbuku kulikuwa na kelele kutoka kwa wabunge wengi wa CCM wakidai kwamba posho za shilingi laki tatu kwa siku ni ndogo, hivyo iongezwe angalau ifike shilingi laki 5.

Jioni hii Mwenyekiti Mbowe amezungumza na wajumbe wa tume pamoja na asasi zilizoteuliwa kujadili katiba, ameonyesha msimamo wake wazi, amesema kwambanamnukuu "Pamoja na kuteuliwa kuwa mjumbe kwenye hii tume, msimamo wangu ni kwamba nyongeza ya posho HAPANA, na ninawataka wabunge waridhike na kiasi kilichopitishwa, maana iko fair kabisa. Nawaomba wajumbe wa bunge hili la katiba kuwa wazalendo zaidi kwa nchi yao, waweze kusaidia kwa upatikanaji wa katiba mpya tunayotaka, na kama wanaona hiki kiwango ni kidogo ni dhahiri tumekosa uzalendo kwa watu wetu" mwisho wa kumnukuu.

Kwakweli katika hili tuna kila sababu ya kumpongeza Mwenyekiti Mbowe kwa ujasiri wake wa kusimamia kile anachokiamini, na hii ndiyo faraja kwa watanzania ambao wamewekeza imani yao kwa CHADEMA, wakiamini katika rasimu hii ya katiba hakuna atakayetoka nje ya CHADEMA kuwatetea, bali wajumbe wanaotokana na CHADEMA kutokana na ukweli uliojengeka kwamba CCM na vibaraka wao, pamoja na taasisi zao ambazo zimetokana na makada wa ccm wataendelea kuitetea chama badala ya maslahi mapana ya taifa.

Nawakilisha,


Habari hii ni kwa hisani ya mtu wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom