Kamati ya Bunge itakayomuhoji Gwajima ijiandae kukutana na majibu yatakayowaacha wakiangaliana

Kamati ya Bunge itakayomuhoji Gwajima ijiandae kukutana na majibu yatakayowaacha wakiangaliana

Kwa msomaji wa Biblia au mtu yoyote aliesikia habari za Yesu, bila shaka atakuwa amesikia habari au visa vya Yesu kutoa majibu kwa wafuasi wake, majibu yaliyokuwa yakiwafanya watu kubaki wanashangaana kama sio kutawanyika au kubaki midomo wazi na wakati mwingine kujiona wajinga.

Rejea kisa cha mwanamke aliefumaniwa na watu kutaka kumpiga mawe, habari ya kaisali na ile ya wafuasi wake kumtafuta Yesu na majibu aliyowapo.Hayo yakiwa kwa uchache tu.

Kwa wasiofahamu habari za Yesu, kisa kimojawapo ni hiki hapa chini:

Yohane 8 | BHN Bibilia | YouVersion

Japo simkubali sana Askofu Gwajima, lakini naamini atawashangaza wajumbe wa hiyo kamati kwani ni wazi Gwajima hana kosa na zaidi Gwajima hayuko Bungeni kwasababu ana shida na hela ya ubunge.

I wish mahojiano yangekuwa live.

Hata hivyo, kwa majibu watayopewa, watahadithiana na tutayajua.

Tusubiri.

Kuna watu mindsets zao zimeganda kwenye zama za “...zidumu fikra za mwenyekiti wa chama...”
 
Gwajima anapinga msimamo wa serikali halali,ni UAMUZI wa serikali kuwa covid 19 ipo na watanzania wapate vaccine jab ila kwa HIARI yao,sasa wewe kutumia nyumba za ibada na kutamka kuwa waumini wako hawatachanja vaccine ni kupingana na government's of the day,na kama Mr.Gwajima hapendi chanjo hiyo ni haki yake pia alikua na haki ya kuipeleka serikali mahakamani kupinga hizi chanjo.Nchi ina Rais mmoja na ndiye anayetoa directions nchi iende wapi,hukubaliani nayo nenda mahakamani.msimamo wangu binafsi watanzania wenzangu go out there and get a jab,pls do that mimi tayari nimepata jab.
Vipi, ikitokea Rais mjinga Kama kibwetere!??
Akatufungia ndani Ili atuchomee moto ndani?!
Tuendelee kutii tu!!! Hizo directions za kiongozi wetu.

Mh!?
 
Kama Pascal Mayalla mwenyewe ana_like tu humu komenti unategemea nani atatoa majibu yenye weledi?.

Kila mtu anasubili kuanzisha mada baada ya kamati kumlarua huyo gwajiboy.
Mkuu TODAYS , mimi sio tuu hutoa likes kwa kila thread ninayofungua na kwa kila post ninayosoma, ila pia ni mchangiaji mzuri, mfano kwenye uzi huu, nimeelezea experience yangu, kuhojiwa na Kamati ya Bunge.
P
 
Hakuna wa kujibu hoja za Askofu Gwajima. Hata wakikesha na madesa bado ni ngumu kusimama na mtu anayesimamia anachoamini.
Watamualika harakaharaka Mzee aliyetolewa jalalani..anamudu majibubya hovyohovyo na kejeli
 
Tupe uzoefu unavyoona Gwajima kesho anachomoka au hachomoki.Predict
Hachomoki, ila majibu sio kesho, kesho atahojiwa tuu, halafu matokeo ni keshokutwa, atapewa adhabu.

Ila kitu cha mwisho Gwajiboy atakachofanya ni hiki
Hivyo mwisho wa siku, Gwajiboy atachanjwa na misukule yake, watafuatia.
P
 
..Gwajima amesema ukichanjwa unakuwa na nguvu ya sumaku pale sindani ilipoingia. Hivi hakuna Mtanzania anayeweza kum-challenge?

..Pia amesema ukichanjwa pale sindani ilipoingia panaweza kuwasha balbu. Je, hakuna Mtanzania anayeweza kumjibu kwa ushahidi?

..Vilevile amewatuhumu viongozi kuwa wamehongwa ili wa-promote chanjo, na kwamba wamechanjwa chanjo "feki." Hilo nalo hakuna Mtanzania wa kumjibu?
Hajawahi kusema haya!
 
Hachomoki, ila majibu sio kesho, kesho atahojiwa tuu, halafu matokeo ni keshokutwa, atapewa adhabu.

Ila kitu cha mwisho Gwajiboy atakachofanya ni hiki
Hivyo mwisho wa siku, Gwajiboy atachanjwa na misukule yake, watafuatia.
P
Gwajima angefanya Kama Polepole nadhani kusingekuwa na Mgogoro wowote unaofukuta.Polepole yupo kimya hataki malumbano na viongozi nadhani kamati haimhusu.
 
Kwa msomaji wa Biblia au mtu yoyote aliesikia habari za Yesu, bila shaka atakuwa amesikia habari au visa vya Yesu kutoa majibu kwa wafuasi wake, majibu yaliyokuwa yakiwafanya watu kubaki wanashangaana kama sio kutawanyika au kubaki midomo wazi na wakati mwingine kujiona wajinga.

Rejea kisa cha mwanamke aliefumaniwa na watu kutaka kumpiga mawe, habari ya kaisali na ile ya wafuasi wake kumtafuta Yesu na majibu aliyowapo.Hayo yakiwa kwa uchache tu.

Kwa wasiofahamu habari za Yesu, kisa kimojawapo ni hiki hapa chini:

Yohane 8 | BHN Bibilia | YouVersion

Japo simkubali sana Askofu Gwajima, lakini naamini atawashangaza wajumbe wa hiyo kamati kwani ni wazi Gwajima hana kosa na zaidi Gwajima hayuko Bungeni kwasababu ana shida na hela ya ubunge.

I wish mahojiano yangekuwa live.

Hata hivyo, kwa majibu watayopewa, watahadithiana na tutayajua.

Tusubiri.
Wanaenda kumsihi apunguze moto, wakimtishia ataivua nguo serikali kanisani!
 
Labda waamue kumbeba. Tangu aanze mjadala dhidi ya covid ameongea vitu vingi vya uongo.
Hata maswali anayojifanya kumbana nanyo waziri yalishajibika muda.
Hivi karibuni ameanza kulegeza ulimi na kujifanya hapingi lakini alitakiwa kuyakana yale maneno kwenye hotuba yake ya mwanzo kuwa viongozi wamevuta mshiko.
Yapo yutube hivyo atawajibika kutoa ushahidi.
Akitumia clip za Mollel atakwama kwani ni kipindi kile Rais hajaunda kamti iliyokuja na majibu kuwa chanjo ni salama.
Kamati ikisikiliza clip zake zote ina mambo mengi anayotakiwa kuyatolea ushahidi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Tena ingependeza kama hayo mahojiano yangerushwa live kwenye vituo vya habari vyote nchi ili tujue yupi ni mkweli yupi ni mfata upepo.
Ila hawawezi maana inaweza kuwa ni zaidi ya mahojiano.
Kwanini iwe hivyo kwa Gwajima pekee? Wote waliohojiwa kabla walihojiwa kwa utaratibu huo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom