Kamati ya Bunge Maalum la Katiba hatimae imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000!

Mie nadhani wangeongezea walemavu ambao wana wasaidizi tu.....wengine no plzzzz....
 
Posho Bunge Maalumu la Katiba kuwa 500,000 kwa siku.

Habari zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Leo kwamba Kamati ya kufuatilia posho za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000 kwa siku imethibitishwa ni kweli.

Natoa wito kwa Wananchi wote kushinikiza kwa Rais pendekezo hili asilikubali. Naunga mkono wazo la mjumbe wa Bunge Maalum ndg Julius S. Mtatiro la kuorodhesha majina ya wote wanaopinga nyongeza ya posho. Nitaweka sahihi kwenye petition yake hiyo mapema kesho asubuhi.

Wagombea uenyekiti nao wanaahidi kupandisha posho. Nawaonya wasithubutu kutoa ahadi hiyo kwani sio mamlaka yao. Mgombea mwenye sera ya posho hatapata kura yangu na nitashawishi wajumbe wengine wasimpe kura.

#NatakaKatibaSitakiPosho

Chanzo: Zitto Kabwe (FB Wall)

Zitto unatumia nguvu nyingi sana kutetea umaarufu wako ulioporomoka.
 
Mkuu kukaa kimya ni bora, ZZK ni shujaa kwa sasa Tz....kwenye hili amesimama upande wa haki chuki zako ulizopandikizwa na viongozi wanaomuona kuwa ni tishio ziweke pembeni la si hivyo utaonekana kioja.
Hv huwa mnafikiria kwa kutumia viungo gani ktk mwili..!? Ushujaa wake uko wapi wakati anasaini mahudhurio? Ukisaini mahudhurio,maana yake umeidhinisha posho yako itumike. Na kutosaini mahudhurio ni kosa kwa kanuni za bunge. Tupe maelezo toka aanze kukataa posho,zile pesa huwa zinapelekwa wapi? Au kwa akili yako zinarudishwa hazina!? Unalishwa sumu ya kijinga wewe unashabikia! Pia umesema ile kamati imejaa wasomi ndo maana wamemzidi ujanja mbowe. Kumbe kuwa msomi ni kuwahadaa wasiosoma ili uwaibie!? Km jibu ni ndiyo,kuna haja gani ya kuwa na wasomi wezi? Ndo maana tumefika hapa kwa kuongozwa na wachumia tumbo..!!
 
Hivi hawa si ndo walikuwa wanajiita wanaharakati walikuwa wanalalamikia matumizi mabaya ya serikali katika pesa...,kweli kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Mbona habari hii ni kinyume na habari za magazeti ya leo? Nani muongo? Magazeti ama aliyeitoa na lengo lilikuwa nini?
 
mhhhh kama hii ni kweli ina maana wajumbe wale 6 walioteuliwa na Mwenyekiti wa muda wameungana so hata mzee wetu Mbowe nawe unataka uongezewe na wale memba wako wa kamati wakina Kimiti na wengineo?Jaman mmeenda kuomba muongezewe posho au kwa ajili ya katiba?nakumbuka Warioba jibu alilolitoa ni kua kama mtu hawez ajitoe au aandike barua kwa Raisi,tuachane ujinga wa kuchezea hela za watanzania mana hiyo laki tano ni hela kubwa sana hata hiyo laki 3 nayo ni kubwa sana na msituone watanzania ni wasio na uelewa labda mmoja lakini sio wote.

Mnaboa na ujinga wa kuchezea hela za nchi

Thats true hata hivyo wafahamu ya kwamba pesa wanayopewa watu wanapewa kwa mwezi mzima ndo mshahara. Halafu ninacho jifunza hapa ni kwamba hata wale ambao nilikuwa nahisi watakuwa wakombozi wangu wamekuwa kim,ya nikinyonywa na kukamuliwa kodi yangu mwananchi and i believe none can liberate we tanzanian neither ruling nor opposition party.
 
Dodoma. Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba, Mwananchi limebaini.

Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.

Taarifa hizo zilidai kuwa wajumbe hao wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia viwango vya posho vinavyolipwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na Mashirika ya Umma.

Pia kamati hiyo ilichambua viwango vya posho walivyolipwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viwango vya posho ya kujikimu vya Sh80, 000 kwa siku wanavyolipwa watumishi wa Serikali.

"Hili jambo linahitaji busara sana na kutazama mazingira ya nchi pia, kwa hiyo wajumbe wale baada ya kuoanisha viwango vya posho vya taasisi mbalimbali wameona Sh300,000 zinatosha," alisema mmoja wa wajumbe ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Mjumbe mwingine, ambaye pia hakutaka kutajwa, alisema kuwa watakaa leo kukamilisha taarifa ya utafiti wao, kabla ya kuikabidhi kwa Mwenyekiti Kificho.

Alisema pamoja na umuhimu wa kazi za mbunge, lakini isingekuwa rahisi kuongeza posho katika mazingira ya sasa, ambapo wananchi wanalia hali ngumu ya maisha.

Wajumbe hao walioteuliwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho ni William Lukuvi, Mohamed Abood Mohamed, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Jenister Mhagama na Asha Bakari.

Awali, taarifa kutoka ndani ya Bunge zilidokeza kuwa wajumbe hao walikuwa wakutane jana saa 9:00 alasiri ili kuandaa ripoti itakayopelekwa kwa Kificho ikiwa imebeba ushauri kuwa kiwango cha sasa cha posho kinatosha.

Sh300,000 wanazolipwa wajumbe wa Bunge Maalamu la Katiba zinajumuisha Sh80,000 kwa siku ambayo ni posho ya kujikimu na Sh220,000 kwa siku kama posho maalumu ya kuhudhuria kikao.

Posho maalumu ya Sh220,000 inajumuisha posho ya dereva inayopaswa iwe kati ya Sh40,000 na Sh45,000 kwa siku, usafiri wa ndani (mafuta ama teksi), mawasiliano na matumizi mengine binafsi.

Ofisi ya Bunge Maalumu
 
Zitto unatumia nguvu nyingi sana kutetea umaarufu wako ulioporomoka.

Zitto anatumia fursa aliyonayo kuyasemea yale anayoyaamini. Amekuwa akisema hivo siku zote. Hata alipokuwa bado na nguvu Chadema alizipinga posho kwa vitendo kwa kutochukua posho. Hiyo haibadiliki. Labda mwenzetu ungefurahi sana kama angeunga mkono hoja ya kupandisha posho hadi laki 5? Tuwe ni watu wa kutumia akili zetu vizuri siyo kupinga tu simply because you hate him.
Ushauri wangu kwa wanasiasa wapenda nchi tutafute platform mpya ya kulitetea taifa letu. Atokee mtu wa kutumobilise na kuanzisha Tahariri square yetu pale bungeni Dodoma na kupiga kambi pale na kuhakikisha hawa mafisadi hawatoki mle ndani na laki 5! Kwa nini Watanzania tunakuwa wanyonge sana? Chadema na Ccm na Cuf lao ni moja yanapokuja mambo ya ulaji. Wanaiua nchi!
 
Yafaa Zitto apigwe BAN hata huko fb!kwa kuweka habari za kizushi huku akishindwa kutoa ufafanuzi juu ya pesa za ccm zilizokua zinatumwa germany na kurudi kwake kwa western union
 
Hv huwa mnafikiria kwa kutumia viungo gani ktk mwili..!? Ushujaa wake uko wapi wakati anasaini mahudhurio? Ukisaini mahudhurio,maana yake umeidhinisha posho yako itumike. Na kutosaini mahudhurio ni kosa kwa kanuni za bunge. Tupe maelezo toka aanze kukataa posho,zile pesa huwa zinapelekwa wapi? Au kwa akili yako zinarudishwa hazina!? Unalishwa sumu ya kijinga wewe unashabikia! Pia umesema ile kamati imejaa wasomi ndo maana wamemzidi ujanja mbowe. Kumbe kuwa msomi ni kuwahadaa wasiosoma ili uwaibie!? Km jibu ni ndiyo,kuna haja gani ya kuwa na wasomi wezi? Ndo maana tumefika hapa kwa kuongozwa na wachumia tumbo..!!
Unatumia nguvu nyingi sana kufikisha ujumbe ambao hata ufahamu nao hauna. Kwa hiyo kwa imani yako na ufahamu wako ukisign ndiyo umechukua posho? Be serious!
 
Yafaa Zitto apigwe BAN hata huko fb!kwa kuweka habari za kizushi huku akishindwa kutoa ufafanuzi juu ya pesa za ccm zilizokua zinatumwa germany na kurudi kwake kwa western union

Kweli wewe bongolala
 
Posho Bunge Maalumu la Katiba kuwa 500,000 kwa siku.

Habari zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Leo kwamba Kamati ya kufuatilia posho za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000 kwa siku imethibitishwa ni kweli.

Natoa wito kwa Wananchi wote kushinikiza kwa Rais pendekezo hili asilikubali. Naunga mkono wazo la mjumbe wa Bunge Maalum ndg Julius S. Mtatiro la kuorodhesha majina ya wote wanaopinga nyongeza ya posho. Nitaweka sahihi kwenye petition yake hiyo mapema kesho asubuhi.

Wagombea uenyekiti nao wanaahidi kupandisha posho. Nawaonya wasithubutu kutoa ahadi hiyo kwani sio mamlaka yao. Mgombea mwenye sera ya posho hatapata kura yangu na nitashawishi wajumbe wengine wasimpe kura.

#NatakaKatibaSitakiPosho

Chanzo: Zitto Kabwe (FB Wall)

:A S 13:Sawa kabisa
 
zzkabwe ni janga lataifa;mwongo+masifa=kifo cha kisiasa...hata nahvyo posho laki3 nikubwa.wengne bukuten kwasiku shda..
 
Zitto anatumia fursa aliyonayo kuyasemea yale anayoyaamini. Amekuwa akisema hivo siku zote. Hata alipokuwa bado na nguvu Chadema alizipinga posho kwa vitendo kwa kutochukua posho. Hiyo haibadiliki. Labda mwenzetu ungefurahi sana kama angeunga mkono hoja ya kupandisha posho hadi laki 5? Tuwe ni watu wa kutumia akili zetu vizuri siyo kupinga tu simply because you hate him.
Ushauri wangu kwa wanasiasa wapenda nchi tutafute platform mpya ya kulitetea taifa letu. Atokee mtu wa kutumobilise na kuanzisha Tahariri square yetu pale bungeni Dodoma na kupiga kambi pale na kuhakikisha hawa mafisadi hawatoki mle ndani na laki 5! Kwa nini Watanzania tunakuwa wanyonge sana? Chadema na Ccm na Cuf lao ni moja yanapokuja mambo ya ulaji. Wanaiua nchi!

Na je zile za kupiga Posho ndefu za Mashirika mbona hauzisemi ?
Once a traitor you wil b a traitor forever
 
Back
Top Bottom