Pre GE2025 Kamati ya Bunge yapendekeza isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi

Pre GE2025 Kamati ya Bunge yapendekeza isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.hii ni kutokana na kuwa na sera nzuri zinazogusa maisha ya watu,pamoja na utekelezaji bora wa ilani yake ambao umekuwa ukibeba na kusheheni mambo na vitu vinavyogusa mahitaji ya watu na wakati. Tofauti na vyama vya upinzani kama CHADEMA havina hata uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi
Sasa kama ni hivyo kinachowaogopesha ni nini? Katiba bora itakayoweka misingi mizuri ya nchi hata kwa miaka 10 tu mnaogopa isiwepo,tume ya maana ya uchaguzi ndo hii mnayojikanyaga nayo kila siku kwa miswada ya kuunga unga wakati vitu viko wazi wala haviitaji porojo nyingi. Halafu kutwa kujitutumua kua mna sera nzuri. Sera nzuri zipi hizo ambazo zinawafanya mnaogopa katiba bora?.
 
Sasa kama ni hivyo kinachowaogopesha ni nini?.Katiba bora itakayoweka misingi mizuri ya nchi ata kwa miaka 10 tu mnaogopa isiwepo,tume ya maana ya uchaguzi ndo hii mnayojikanyaga nayo kila siku kwa miswada ya kuunga unga wakati vitu viko wazi wala haviitaji porojo nyingi.Alafu kutwa kujitutumua kua mna sera nzuri.Sera nzuri zipi hizo ambazo zinawafanya mnaogopa katiba bora?.
Halafu acheni visingizio vyenu ninyi.hivi mbowe kwa miaka yote alikuwa anapita kwa kutumia tume ipi ya uchaguzi? Hivi upinzani wa nchi hii kwaajili zenu mnafikiri mnaweza kupewa nchi hii kuongoza? Acheni kuota ndoto zenu za mchana.
 
Chadema wanadhani CCM watajiwekea kisu shingoni halafu wajichinje. Never
Chadema sijui kwanini hawaelewi? Sijui kwasababu Mbowe analamba asali ndio maana hawaelewi kuwa “ huwezi kufika peponi bila kufa”!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kamati ya Bunge Utawala, Sheria na Katiba imependekeza kuwa isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi.

Pia kamati imependekeza kuwa badala ya kuitwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iitwe Tume huru ya uchaguzi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

==============================================

Kamati ilikuwa ina maoni kwamba Sheria isiweke ulazima kwa Mkurugenzi Mtendaji kusimamia Uchaguzi na badala yake, kuwepo na masharti ya Mtumishi wa Umma mwandamizi ama mtu mwingine yoyote mwenye sifa kuteuliwa kuwa Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi.

Serikali iliona kuwa upo umuhimu wa Wakurugenzi Watendaji kutajwa kwenye sheria kwa kuwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya madai na. 138/2019 na Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu kwenye kesi ya madai na ziliamua kuwa Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi haukiuki masharti ya Katiba wala Mkataba wa Afrika wa Watu na Haki za Binadamu mtawalia.

Ibara ya 6(1) inaeleza kuwa kila Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya atakuwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika Jimbo au Kata

Hawakubaliani na Wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma kusimamia uchaguzi kwa kuwa hawawajibiki kwa tume ya uchaguzi bali wanawajibika kwa Rais na Chama Tawala hivyo wanakosa sifa ya kuwa mamlaka ya uchaguzi huru na haki. Vifungu hivyo vifutwe na Tume iajiri watumishi wake wenyewe

Kamati bado ina maoni kuwa hakuna ulazima wa sheria kuweka sharti kwa Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi au wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa kuwa uzoefu unaonyesha wapo Wakurugenzi kwa sababu mbalimbali wanapoteza sifa za kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Umeanza kupingana na mpendwa wako Bashite? Huu si ndio ulikua msimamo wako na chama kwa ujumla? imekuajeje tena Mwashaaa
 
Back
Top Bottom