Pre GE2025 Kamati ya Bunge yapendekeza isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi

Pre GE2025 Kamati ya Bunge yapendekeza isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe kweli bwege. Ni lini nilikuambia kuwa mimi ni mwanachama wa chama cha mtu yeyote? Chama changu mimi ni ukweli. Hicho ndicho chama changu milele. Mimi siyo chawa au kunguni kama ulivyo wewe. Ndiyo maana akili na fikra zangu, vyote vipo huru.

Tunavyosema tuwe na Tume huru ya uchaguzi, au tuwe na sheria nzuri, hatuangalii CCM watasema nini AU CHADEMA watasema nini.

Lakini ukweli ni kwamba uharibifu wote wa nchi hii mwenye lawama zote ni CCM. Hiki ndicho chama kilichovuruga ustawi na ndoto za Watanzania wengi kwa sababu ndicho kilichoamua kushikilia madaraka kwa njia zote, haramu na halali. Tunataka yeyote anayekuwa kiongozi awe amepatikana kwa njia halali tu.

Siyo majitu mauaji kama Makonda, siku moja, usikie kuwa ni Waziri, kwa kupitia njia haramu na za kihuni.
Naomba unijibu kuwa ulikuwa na ndoto gani ambazo CCM imekuzui kutokutimiza wakati wenzako wakitimiza chini ya serikali hii hii ya CCM Ambayo imekuwa ikiweka mazingira wezeshi kwa kila mtu kutumia fursa kujikwamua kiuchumi.
 
Sina uwezo wa kuunda bunge la majizi.
Basi kaa kwa kutulia uendelee kupeleka mawazo yako na kero zako kwa serikali ya CCM na wabunge waliopo .hili ndilo bunge lako ambalo unatakiwa ukubaliane na ukweli huo.
 
Basi kaa kwa kutulia uendelee kupeleka mawazo yako na kero zako kwa serikali ya CCM na wabunge waliopo .hili ndilo bunge lako ambalo unatakiwa ukubaliane na ukweli huo.

Kero gani zinaweza kutatuliwa na Hawa majizi? Mfano halisi ni umeme.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kamati ya Bunge Utawala, Sheria na Katiba imependekeza kuwa isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi.

Pia kamati imependekeza kuwa badala ya kuitwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iitwe Tume huru ya uchaguzi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

==============


Kamati ilikuwa ina maoni kwamba Sheria isiweke ulazima kwa Mkurugenzi Mtendaji kusimamia Uchaguzi na badala yake, kuwepo na masharti ya Mtumishi wa Umma mwandamizi ama mtu mwingine yoyote mwenye sifa kuteuliwa kuwa Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi.

Serikali iliona kuwa upo umuhimu wa Wakurugenzi Watendaji kutajwa kwenye sheria kwa kuwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya madai na. 138/2019 na Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu kwenye kesi ya madai na ziliamua kuwa Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi haukiuki masharti ya Katiba wala Mkataba wa Afrika wa Watu na Haki za Binadamu mtawalia.

Ibara ya 6(1) inaeleza kuwa kila Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya atakuwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika Jimbo au Kata

Hawakubaliani na Wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma kusimamia uchaguzi kwa kuwa hawawajibiki kwa tume ya uchaguzi bali wanawajibika kwa Rais na Chama Tawala hivyo wanakosa sifa ya kuwa mamlaka ya uchaguzi huru na haki. Vifungu hivyo vifutwe na Tume iajiri watumishi wake wenyewe

Kamati bado ina maoni kuwa hakuna ulazima wa sheria kuweka sharti kwa Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi au wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa kuwa uzoefu unaonyesha wapo Wakurugenzi kwa sababu mbalimbali wanapoteza sifa za kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Nchi kama India hutumia Resident Magistrates wa jimbo husika kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye maeneo husika. Mchakato wa uchaguzi mchakato wa kisheria na ndiyo maana hata huko juu mwenyekiti na makamu wake wa Tume ya uchaguzi ni lazima wawe ni majaji. Hivyo huku chini resident magistrates ndio proper persons. Wasimamizi wa vituo wanaweza kuendelea kuwa waalimu au wanafunzi baada ya kupewa semina.
 
Back
Top Bottom