#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Hao waambiwe hata Chanjo za kifaduro, Kifua kikuu, Homa ya ini, surua na polio zinatoka hukohuko kwa wazungu

Kana hawazitaki waambie watengeneze zao!

*************************************

Baada ya kusema hayo, hata mimi nataka tusikurupuke kwenye kupokea hizo chanjo, Hebu tukae kwanza kama miaka mitano tusikilizie, tukiona hazijawadhuru waliochanja basi hapo ndo tuamue kuchanja au la, tusikurupuke!
Fafanua kidogo mkuu? Sio kwamba kuna vigogo wanataka kupiga pesa kupitia chanjo?
 
Kwa mujibu wa DPC Gerson Msigwa Kamati maalumu iliyoundwa na Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani kufanya tathmini ya ugonjwa wa corona ( Covid-19) itawasilisha taarifa yake leo alasiri mbele ya Rais Ikulu Jijini Dar es salaam

----
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​
Upuuzi tu kujifanya kama hakuna kazi yoyote imefanyika kuhusu corona.
 
Ukisoma ripoti nzima hakuna jipya na ni yale yale tunayoyasikia mataifa ya nje.Inaonekana hawakutumia ujuzi na akili zao wala kusikiliza maoni ya wananchi bali wamekopi na kubandika.

Hivi kamati haijasikia kwamba chanjo nyingi zina madhara na mataifa kadha wa kadha wanazirejesha kwao.

Na hawajasikia kuwa taifa lillochanjwa kwa zaidi ya asilimia 60 corona ndio kwanza inaongezeka.

Na kwamba sasa corona huko ilipo haichagui tena umri,mbona wao bado wanagwa makundi ya watoto na wazee.
 
Ndo wameandika hayo mavitabu yote au wamekopi tu maandishi ya wengine na kuyakusanya na kuyaweka yaonekane kama mavitabu?

Halafu sidhani kama Samia atayasoma [emoji1787].

Sidhani kama ni mtu wa kusoma mavitabu kama hayo.

Yeye ni mitandao tu [emoji1787][emoji1787].
Endelea kudhani dhani tu. Ipo siku utadhani kuwa nawe ni mwanamke!
 
Koona ipoo..jameni..kwisha Tanzania ..tutaanza kujazwa hofu na masharti ya ajabu ajabu ya kulazimishana kuvaa barakoa...Uwii jiwee tutakumis kwa misimamo wako aisee
Hii misimamo ndo imemgharimu!
 
Hao tayari walishanunuliwa na mabeberu...hata majina yao yalikuwa Siri...

Ambao hamjanunuliwa utakuwa wewe na hili jamaa Mjingamimi.

Wapumzike kwa amani wahanga wote walio kuwa wametelezewa hili gonjwa.

Inasikitisha kuwa maisha yaliachwa kupotea ambayo kwa hakika hayakupaswa kupotea.

Hivi kina Prof Mchembe na Makubi na waziri Gwajima bado wako ofisini?
 
Back
Top Bottom