Sasa wewe unaogopa nini?
Chapa kazi bwashee!
Johnthebaptist, hii issue si ya kufanyia mzaha - jambo liwezalo kugharimu watanzania ktk sekta zote visababishi vyake ni vya kibinafsi (kundi dogo sana) linanufaika - tutakosa fedha mapambano dhidi ya Ukimwi, elimu, afya, na utawala
Why watu wapambane kufa kupona ili waongoze hata kwa kutumia nguvu na hila za wazi? Ktk hali ya kawaida binadamu unatumia mbinu zilizofichika ili kushinda uchaguzi - mbinu hizo zinapogundulika basi unakuwa mpore na kutii mamlaka za kikatiba. Mfano kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya CCM huwa tunashiriki na mwisho wa siku anapotokea mshindi basi tunatulia - vivyo hivyo kwenye uchaguzi mkuu tulitegemea watu kutii mamlaka za kikatiba na taasisi zilizopewa dhamana ya kusimamia shughuli za uchaguzi kuwa very transparent kiasi cha kusifiwa na kila mgombea;
Police, Jeshi na Usalama nao walipaswa kujificha sana na kukaa katikakati ya wagombea wote kama katiba isemavyo - sasa leo utamwona kiongozi wa Police akisimama na kuharalisha taasisi hiyo kuwa sehemu ya chama "If A = B, B = C". Hai kusema kwamba "wewe fulani hautashinda" (Kilimanjaro); hizi ni aibu kwa mujibu wa kikatiba.
Nimalizie kwa kusema kwamba:-
Ni aibu kwa taifa kama Tanzania ambalo wakulima wake bado wanahitaji msaada ili waweza kujikwamua kiuchumi, vijana wanahitaji ajira ili waongeze pato, vifo vya binadamu kwa makundi yao vikiongezeka wakati huo sisi tukiona poa kukosa misaada hiyo. Hebu tuache ushamba wa kisiasa, tuache ubinafsi wa kimadaraka, na kujiaminisha kuwa hakuna athari zitokanazo na kuminywa misaada.
Tusitarabike kisiasa, kiuchumi na kijamii ili taifa liendelee na kustawi.
Msakila M Kabende
Kigoma - Tanzania