Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kuna watu mbumbumbu kama mimi wanafikiri Tanzania inaweza sasa kujitegemea kwa 100% kuanzia bajeti ya mwaka huu bila misaada yoyote toka USA na washirika wake pamoja na EU.

Kwa wale wahenga kidogo watakumbuka hali ya Tanzania ilivyokuwa baada ya vita ya Kagera, sasa ndiko huko huko tunarudia tena.
 
Kama uriziki na mfumo wa Africa nakushauri nenda kaishi Ulaya,huku Africa utauumiza kichwa chako bila sababu,watu weshazowea Maisha yao na wako Happy!!

Sio happy wamekandamizwa hawana wa kuwasemea
 
Leta ushahidi vinginevyo hizi ni porojo tu kama porojo nyingine
Wewe uletewe ushahidi ili iweje wakati Akili zako ni finyu utaishia kusumbua watu wenzako wenye Akili wameshajua ukweli acha watafune pesa za corona huku wewe ukihangaika kusaka ushahidi kishamba shamba
 
Waathirika wakuu ni wananchi na sio vibaraka na wapambe.Labda wawapige total ban kuingia USA and ulaya wabunge wote wa ccm,wakuu wote wa vyombo wao na familia zao marufuku kuingia,kusoma,kutibiwa,nk ulaya hii itasaidia.
Hawawezi toa pesa zao then ziende kukandamizia demokrasia.Maana wao ndio uathirika kwa kuingia gharama kubwa Sana za kuhudumia wakimbizi afrika.
Hakuna mtawala wa kiafrica anayehudumia wakimbizi Hali wao ndo chanzo cha uzalishaji wakimbizi duniani kwa kuwanyima haki wananchi. Haki ikipotea amani upotea.
Kwani wao ndiyo walitupa pesa ya Uchaguzi!? Hadi watupangie wanavyotaka wao!?
 
Wewe uletewe ushahidi ili iweje wakati Akili zako ni finyu utaishia kusumbua watu wenzako wenye Akili wameshajua ukweli acha watafune pesa za corona huku wewe ukihangaika kusaka ushahidi kishamba shamba
Inashangaza baadala ya kuwa wazalendo na kuitetea serikali ya wanyonge mnakaa kushabikia mabeberu
 
Hata Kama hakuna Corona,pesa zimetumika zaidi kwenye Kinga! Na Kama ujuwaavyo Kinga ni bora zaidi kuliko Tiba!!
Ndio maana wamesema pesa zao lazima mzitolee maelezo ya kueleweka maana ni pesa za walipa kodi wa EU.
 
Kwa vyovyote itakavyo Kuwa wachumia tumbo na walio mshauri vibaya Rais ndio tutalala nao mbele. Hatuwezi teseka ilihali Tunajuwa Rais anawashauri
Mkuu mbona kitengo hawakushauri ccm wale ila wasikombe mboga!?Ina maana kitengo wanazidiwa mbinu na mitambo ya Bashiiru?
Ama kitengo nao wana agenda ya siri kumuaibisha,kumdhofisha mfalme!?
 
Mkuu ebu lete mada vizuri, maana watu kama nyie ndio mnasababisha akina Mexime Melo wanasumbuliwa na serikali, sababu ya habari za uongo.
Hivi, ugaini wa msumbiji na kusini mwa tz, kunawezeshaje nchi kutopewa msaada? Kwani tz ndio mfadhiri wa ugaidi unaondelea huko?
Mi nakushauri, point iwe hiyo ya kisiasa tu wala sio ugaidi. Kweli muongo njia yake fupi.
Umemkamata pabaya hapo!!
 
Hakuna Beberu yeyote atakaye mgusa JPM si kwa vikwazo wala adhabu nyingine yoyote. Wote baada ya muda wataendelea kushirikiana na JPM. JPM kwasasa ameibeba Tanzania Mabegani mwake, chini yake Tanzania itaendelea kung'aa na kuwa na nguvu za ushawishi duniani. Ni swala la muda tu wasio elewa wataelewa.
 
Wafute tu hiyo misaada tukose wote. Wasukuma wachache na vibaraka wao wanataka kula peke yao matunda ya nchi ya chama kimoja.
 
Sasa wewe unaogopa nini?

Chapa kazi bwashee!
Johnthebaptist, hii issue si ya kufanyia mzaha - jambo liwezalo kugharimu watanzania ktk sekta zote visababishi vyake ni vya kibinafsi (kundi dogo sana) linanufaika - tutakosa fedha mapambano dhidi ya Ukimwi, elimu, afya, na utawala

Why watu wapambane kufa kupona ili waongoze hata kwa kutumia nguvu na hila za wazi? Ktk hali ya kawaida binadamu unatumia mbinu zilizofichika ili kushinda uchaguzi - mbinu hizo zinapogundulika basi unakuwa mpore na kutii mamlaka za kikatiba. Mfano kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya CCM huwa tunashiriki na mwisho wa siku anapotokea mshindi basi tunatulia - vivyo hivyo kwenye uchaguzi mkuu tulitegemea watu kutii mamlaka za kikatiba na taasisi zilizopewa dhamana ya kusimamia shughuli za uchaguzi kuwa very transparent kiasi cha kusifiwa na kila mgombea;

Police, Jeshi na Usalama nao walipaswa kujificha sana na kukaa katikakati ya wagombea wote kama katiba isemavyo - sasa leo utamwona kiongozi wa Police akisimama na kuharalisha taasisi hiyo kuwa sehemu ya chama "If A = B, B = C". Hai kusema kwamba "wewe fulani hautashinda" (Kilimanjaro); hizi ni aibu kwa mujibu wa kikatiba.

Nimalizie kwa kusema kwamba:-
Ni aibu kwa taifa kama Tanzania ambalo wakulima wake bado wanahitaji msaada ili waweza kujikwamua kiuchumi, vijana wanahitaji ajira ili waongeze pato, vifo vya binadamu kwa makundi yao vikiongezeka wakati huo sisi tukiona poa kukosa misaada hiyo. Hebu tuache ushamba wa kisiasa, tuache ubinafsi wa kimadaraka, na kujiaminisha kuwa hakuna athari zitokanazo na kuminywa misaada.

Tusitarabike kisiasa, kiuchumi na kijamii ili taifa liendelee na kustawi.

Msakila M Kabende
Kigoma - Tanzania
 
KAYAFA wa Tanzania!Unategemea katika hali kama hii mzungu atoe hela yake?
0659010.jpg
 
Back
Top Bottom