Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Bwashee mtatapika vya mabeberu safari hii.

Mnapeleka sound zenu za Manzese kwa beberu mtakoma.
 
Mku wao tunawashukuru pesa yao iliongeza udhibiti wa Corona Tz. Kwani kama moto unaunguza nyumba unauacha umalize kuunguza nyumba bila kujitahidi kuuzima ili uje upate ushahidi kamili? Utajitahidi sana moto usiunguze nyumba yote maana sio furaha yako nyumba iungue labda kama umekula njama iungue alafu uje ulipwe na Bima.
 
Wamezuia 1.6T pekee. I believe Serikali ‘tajiri’ ya Magufuli can cope without hiyo amount.

Hiyo amount si hata Bilionea Laiser anaweza kumpa Magufuli?😊
 
Sasa kumbe misaada, hawatubabaishi hao
Ukiwa hujui mambo utaropoka hv,lakin kwa jinsi ilivyo baadhi ya sekta Kuna hauweni kutokana na hawa watu weupe kujtoa kwetu,mfano hii nchi haina uwezo wa kununua ARV,neti Kuna watu wanasaidia,hata kwenye elimu Leo watoto wetu viziwi,vipofu,tahira,bubu wanasoma kwa upendo wa wazungu,yaan hz nchi zetu znategemea mengi sana,ila ukiwa Mtoto huwez jua
 
Matapeli rudisheni hela za wanaume haraka sana. Mmeiba uchaguzi na bado mnaleta shobo kwenye hela za wanaume?
 
Unadhani ndugu zetu Wazungu wana akili maandazi kama sisi?

Wanajua tumewapoteza:
  • former prezo
  • minister
  • members of parliament
  • prominent religious leaders
  • prominent business persons
  • just to mention a few.

Korona haina Tanzania!
 
Kikao chetu cha kwanza cha bunge, wajadili kuikataa misaada kutoka EU, kama ikija na mashariti. Sisi tunataka kujitegemea hivyo watuletee vikwazo vyao na kutunyima misaada, ndipo akilk atachangamka mpaka kuweza kujitegemea. Lakini tukitarajia misaada tu hatuwezi kujiendesha kamwe.
Najua tutapata shida mwanzoni, lakini tutaweza kuibuka washindi. Kuna vitu vingi tumedhubutu na kufanikiwa na hapa tutaweza. Matatizo ni vibaraka wa humu ndani ndo watatusumbua na maneno tu, lakini mwisho nao watanyooka.
 
...Mkuu, nikukumbushe tuu. Katika mambo ambayo tulitakiwa kufanya katika kupambana na Covid-19 mojawapo ilikuwa kufanya upimaji wa halaiki na kutoa report kila siku kwa mamlaka husika. Sasa sie kama nchi (serikali unayoishabikia) iliamua ghafla kuacha kabisa upimaji (ambao haukuwa wa halaiki anyway). Kwa style hiyo tulitensa kinyume na matakwa ya WHO. Pia pesa iliyotolewa kama msaada wa kupambana na Covid-19 mojawapo ya kazi zake ilikuwa kulipa risky/hardship allowance kwa wahudumu wa afya kwenye vituo vya kutolea huduma nchini. Mpaka kesho watoa huduma zile posho wanaziskia tuu
 
Magufuli alitangazia dunia mwezi Juni kuwa Corona imeshindwa Tz kwa nguvu za mungu!

Sasa misaada ya mabeberu ya kupambana na Corona ya nini tena? tena misaada unapokea mwezi September!

Mzee Meko ni mwizi na mpigaji.
Atazitapika tu pesa za mabeberu.
Huo msaada tumeubadilisha kuwa zawadi kutoka kwa Mabeberu kutokana na kushinda Vita ya Covid!😂😂😂😂
 
Mungu wabariki Wazungu
 
Unadhani ndugu zetu Wazungu wana akili maandazi kama sisi?

Wanajua tumewapoteza:
  • former prezo
  • minister
  • members of parliament
  • prominent religious leaders
  • prominent business persons
  • just to mention a few.

Korona haina Tanzania!
Sasa wanahoji nini?!
 
Kuna watu inabidi uwashangae tu,...

Dunia ni mshikamano hata Hizo nchi tajiri bila ushirikiano na nchi maskini basi zitakuwa si chochote

Anaeasema kuwa Tanzania itajimudu, otaendelea bila ushirikiano na Mataifa mwengine basi huyo ana akili za mchwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…