Serikali ya Sweden imezuia pesa pale REA zilizokuwa zitumike kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu. Sababu, serikali imelikoroga na wamiliki wa vituo binafsi vya kuzalishia umemeHatutapona marekani last time ulipofutwa uchaguzi Zanzibar walionda msaada kwenye REA,sijui sahivi watafuta lipi
Ndio raha ya kuwapa wahutu nchi. Mtu haja wahi kuongoza kijiji mna mpa nchi. Ccm bwanaWaondoe tu misaada, tuisome number wote sio wacha he wanaokula mema ya nchi.
Inaweza ikawa kweli ila sidhani kama wanaweza kusitisha misaada sababu ya ugaidi. Hilo nalikataa.Wenye hela zao ndio waliojadili na mambo ya ugaidi kusini mwa Tanzania sio mimi.
Usipanic sana. Kunywa Maji mengi alafu lala kupunguza stressDuuh haki za wanawake na watoto waliokuwa wanakosa dawa na vitanda siyo haki ya binadamu ila nguruwe ila ya wao kukosa malighafi free of chaji ndiyo haki za binadamu...kinachoniumiza ni kuona kuna ambao wanashadadia badala ya kutoa mbinu za kukabiliana na hawa vampires
Walichofanya serekali ya CCM ni kufanya ufisadi wa kimataifa,yaani ufisadi across borders.Serekali ya Magufuli inajinasibu kuwa ni serekali inayopambana na ufisadi lakini imefanya ufisadi huu wa kutisha wa nje ya mipaka ya Tanzania na hii haijawahi kutokea tokea tupate uhuru.Masharti yote haya walikuwa wanayajua lakini kwa kuwa nia yao ilikuwa ovu,nia ya kuiba hela nje ya mipaka ya Tanzania basi wakaamua kuchukua hizo hela na kutupilia masharti yao mbali.Kwa mwendo huu serekali hii ya kifisadi wa kimataifa haiwezi kufika mbali.Sijui kuhusu hayo masharti, sikushiriki kwenye hayo makubaliano kama hata yalikuwepo, Umi Mwalimu yupo kama kuna cha kujibu atafanya hivyo, ...
Ibilisi atakuletea ya kwako kabla ya hiyo yao kuja...Are you not ashamed of yourself...Icc is on the way. Stay tuned
Hoja ya msingi sana hii. Unatoaje msosi kwa mtu ambaye anasema HANA NJAA? 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣Hoja yao sio corona. Hoja yao ni inakuwaje watoe hela za msaada wa corona kwa nchi ambayo imesema haina corona na hawatoi takwimu zozote juu ya corona??? Hizo hela zinatumika kwenye nini??
Vile vipimo vilivyoonyesha papai lina Covid 19 hukuvisikia?Well,kama vipimo vilikuwa fake serekali ilipaswa kutangaza kuwa vipimo ni fake na hawataweza kutimiza masharti ya EU pamoja na WHO ya kupima watu kisha wakatae fedha zao.Serekali ilifanya hivyo?Serekali ilikataa fedha zao?Kuanzia leo jua tunaposema kuwa Tanzania tuna kiongozi goigoi hatutanii hata kidogo!
Niletee hapa nilipo itasaidia...Usipanic sana. Kunywa Maji mengi alafu lala kupunguza stress
Sio kwel, kila kitu tuna tumia pesa zetu za ndani.. Subirini hata uchaguzi mtasikia pesa ilitoka wapi..Kumbe Tanzania ilikubali msaada wa Euro Mil 27 za mabeberu za Covid-19 September hii. Sasa wanataka kujua kwa nini Tanzania ilipewa msaada huo wakati wamesema Corona haipo. Na pia wanataka kujua zimetumika vipi? Moja ya masharti ya kupewa pesa hizo ni pamoja na kutoa statics za ugonjwa na kufata maelekezo ya WHO ambapo Tanzania hawafati. Ila swali pia kwa serikali yetu kwa nini wanachukua pesa za mabeberu wanaowapiga vita? Au ndio ule msemo usemao ''Baniani mbaya kiatu chake kizuru'' Basi tutakuwa wanafiki. Na kwa nini hata sisi watanzania hatujatangaziwa kama misaada imetolewa na mabeberu? Zaidi ya serikali kutupa wananchi tu picha ya kwamba tuendelee kuwachukia mabeberu.
Angalia hapa chini VIDEO Rais wa Bunge la EU anavyolaani utawala wa awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kuwakandamiza watetea haki, wapinzani na kutolinda demokrasia. Hivyo amesema Umoja wa Ulaya utabadilisha siasa yake kuhusu Tanzania ili isipewe misaada moja kwa moja kwa serikali.
Swali langu ni moja tu,kama vipimo vilikuwa ni fake na vinazuia kutii masharti ya EU pamoja na WHO kwa nini wachukue hela za watu ambazo hawawezi kutii masharti yake?Huo siyo wezi?Huo siyo ufisadi?Vile vipimo vilivyoonyesha papai lina Covid 19 hukuvisikia?
tusent twenyewe tubayaaaAU KWA JEURI TUWARUDISHIE TUSENT TWAO WASITUDHALILISHE KWA HAKO KASENT UCHWARA BANA
Maswali ya wana lumumba bana, hadi kichwa kinauma! Haya jibu mwenyewe huenda ikaona faraja ya moyo!Bila kupoteza Muda naomba kwenda kwenye mada moja kwa moja,
Leo nilitenga muda wa kusikiliza kile kilichokuwa kinajadaliwa na Hawa Viumbe wa "EU" (External affairs), Kama tulivyo taarifiwa juzi katika vyombo vya habari vya kwao huko na baadhi ya nyuzi hapa JF.
Ila Nimesikitika Sana kuwa nilichotarajia kukisia kutoka kwao na nilichosikia ni Kama "Vatican na Saud Arabia" (quit different).
In summary; Hiki ndo nilitarajia kukisikia kutoka kwa hawa Nguri wa Hoja duniani;.
1.Uchaguzi wa 28Oct202.
Nilitajia kusikia maswali kama; Kwanini CCM imeishinda kwa asilimia kubwa vile kuliko vyama vingine?
Je baada ya Matokeo Wananchi waliopiga Kura hizo wameridhika na Matokeo Yao au hapana na Kama Ni hapana, Kuna ishara yeyote waliyoionyesha kutokubaliana na walichokichagua( Hapa Wapigiwa kura hawahusiki).
Je baada ya Matokeo wagombea nafasi wa upinzani walioshindwa waliyachukulia je matokeo, Kama Ni ndio sawa na Kama Ni hapana, je Kuna njia zozote za kisheria walizochukua kupinga Matokeo hayo ili kupata haki Yao(ukiondoa ya Matokeo ya urais).
2. Ukandamizwaji wa haki za binadam na Ugaidi;
Nilitarajia kusikia hoja Kama hizi kutoka kwao;
Kwanini msumbuji imeshindwa kuwathibiti Wana mgambo walioweka makazi kwenye nchi yao mpaka Wanasababisha maafa na kukandamizwa kwa haki za binadam nchi jirani Kama Tanzania(Mtwara Kama walivyotaja wao)?. Na Wala siyo kuilaumu Tanzania kisa inapakana na sehemu ambayo magaidi wapo. Nikweli EU hawajui kuwa Msumbuji ni nchi huru na ina mipaka na jeshi lake ambalo haliwezi ingiliwa na jeshi lolote lile pasipo ruhusa?.
3. COVID19.
Nilitegemea kusikia ni, njia gani ilizotumia Tanzania kuondokana na janga la Corona mpaka kufikia hatua ya watu wake kuendelea na maisha yao Kama kawaida bila vifo Wala athari yeyote?
Na wala siyo kulialia kwanini Tanzania haina Corona na tunaipatia pesa, Mara pesa za Corona zimetumikatumika je, Mara Sijui Nini ,
Hapa kwakweli imeonesha wazi kabisa jinsi gani mataifa ya ulaya yalivyo na wivu mkubwa juu ya Tanzania hasa katika suala hili la Covid19.
My take; Tanzania ni nchi yangu na Nina ipenda Sana na Sina shaka na Kiongozi wangu mkuu Yani "JIWE" juu ya kudili na Mabeberu naamini nachokiwaza mimi kuanzia Sasa na kuendelea ndo anachokiwaza Rais wangu. Hizi hoja za Leo niza kupuuza na kukaa kimya kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea maana inaonekana watu wenyewe wamejadili huku mioyo yao ikiwa imejaa chuki binafsi na wivu juu ya Tanzania pamoja na kulialia pasipo kuwa na "deep Intelligences".
Na nilichokugundua Tangu tupate Rais jiwe kwelikweli Tanzania imekuwa femous sana ndani na nje ya Mataifa ya Ulaya. Na wanavyotenga muda wao kutujadili namna hiyo kwetu ni faida kubwa Sanaa maana Kupitia wao ndo wana tangaza na soko letu la utalii na kuwafanya watu wengi zaidi kuja Tanzania kujionea uteule wake.
Mfano; Suala la kututangaza juzi Kati kwenye media zao kuwa "Tanzania ndo nchi pekee dunian ambayo haina maambuzi ya Corona kwa takribani wiki46" na leo walivyosema kwenye mkutano wao kuwa, "tunawapa je Msaada Tanzania angali hawana Corona". Hii itaongeza idadi ya watu wengi Sana wa ulaya waliochoka na lockdown kuja kula maisha kwenye Peace land ya Tanzania huku soko letu la utalii likipanda siku Hadi siku.
#Mungu Mlinde Jiwe, Mungu tulinde Watz wote, Mungu ilinde nchi yangu.
#I love my country [emoji1241].
Tufanyaje ili wizi usiendelee kuwepo?Wizi ulikuwepo au la kushabikia vikwazo kwenye nchi yako ni ukurutu wa mawazo.
Kuwa na maabara ni suala moja, na kutoa takwimu ni suala jingine. Kwa mujibu wa masharti ya pesa za EU, ukishazipata lazima utoe takwimu kwa WHO ambayo sehemu kubwa iko funded na EU baada ya USA kujitoa kuisaidia. Je tuna publish takwimu hata mkama maambukizi ya corona ni 0?Kuna Maabara ya COVID Mabibo iko full nondo kila kitu, hivyo sidhani kama ni ngumu kwa Serikali kuelezea jinsi ilivyotumia fedha kama ni kweli ilipokea msaada kwaajili ya kudili na COVID, ...
Sisi tunalima , tunakula viazi, ugali, maharage, na wali. Shauri yao wanaotembea na ma V8. WayajijuuuuIla mkuu wakipiga pini hakuna rangi tutaacha kuona sisi wananchi, ni vyema wakiweza wangedili na hali hii bila kuumiza uchumi wa nchi. Tutaumia sisi huku walengwa wanakula maisha
Kwa hiyo wewe unategemea nini kitatikea baada ya vikauli uchwara hivyo?Suburini wasaka uteuzi waanze kujitokeza kuwajibu EU pasipo kuwa na hoja za msingi zaidi ya propaganda.
Lakini ni ukiukwaji wa kiwango cha kutisha kwa nchi iliyokuwa sii kufikia mbali bali kuanza safari ya demokrasia kama Tanzania ghafla bin vuu hakuna tena kitu kama uchaguzi wa raia kumchagua kiongozi.Amani iwe nanyi tena wadau!!
Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.
Napenda tu kusema yafuatayo
1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania
2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania
3. Wamehoji hadi kwanini walitoa hela za ku support harakati za Covid na wamembana afisa wao kuwa walitumia vigezo gani kutoa hela hizo wakati Tanzania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa wako covid free
4. Wamemuamuru afisa wao anayejishughulisha na Tanzania kutoa maelezo ya uhakika juu na kwa nini walitoa hela kwa Tanzania na kwanini hawajafuatilia hizo hela zimetumika kwenye nini?
5. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa Serikali.
Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu.