Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Nadhani Magufuli anajiamini ana uwezo wa kuendesha kila kitu bila ya msaada wowote kutoka nje. Kiukweli hili tuliona kwa watu kama akina Mugabe na watanganyika jifunzeni miaka 5 ya mwisho ya Salmin Amour kule Zanzibar. Kama mzanzibari naunga mkono hoja ya kuondosha fedha za misaada zote kwa serekali zote mbili kwa miaka 5 ijayo.
 
mkuu uko serious sana,utaugua kisukari taratibu.

kwanza wazungu hawajawahi kuwa serious na shida zako wewe mnuka mdomo wa nanjirinji huko,kukaa na kushangiria hureeeee kwamba sasa utawala unakwenda kukomeshwa.unachelewa kupiga mswaki tu,wahi uende.
Watu wanawapa hela hadi za madawa na kusambaza umeme vijijini alafu unasema hawapo serious man shida zetu???? Kajipange upya kilaza wa Lumumba wewe!!
 
Amani iwe nanyi tena wadau!!

Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.


View attachment 1630138

Napenda tu kusema yafuatayo

1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania

2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania

3. Wamehoji hadi kwanini walitoa ahadi ya fedha kiasi cha Euro Mil. 27[ Zaidi ya Bilioni 74] za ku support harakati za kupambana na COVID19. Wamembana afisa wao kuhusu vigezo gani vilitumika kuona Tanzania inastahili kupewa hela hizo wakati Tanzania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa nchi iko covid free kutokana na sala.

4. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa Serikali.

Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu.
===

Bunge la Umoja wa Ulaya limetakiwa kutoa maelezo ya kwanini Jumuiya hiyo ilitoa msaada wa kiasi cha euro milioni 27 za kupambana na Covid19 kwa Tanzania, licha ya kufahamu kuwa nchi hiyo imetangaza kuushinda ugonjwa huo.

Akiwasilisha hoja yake, mbunge wa Jumuiya hiyo kutoka Ujerumani, Bw. David McAllister, amesema anataka kufahamu ni namna gani fedha hizo za walipakodi wa bara la Ulaya zimetumika katika nchi ambayo imekataa kutoa takwimu na kufuata miongozo ya WHO.

"Ningependa uwajulishe wajumbe wa kamati yetu juu ya pesa tulizoipatia Tanzania; kulikuwa na vigezo gani vya kutoa pesa hizi, na ni kipi hasa kinachofanywa kwa kutumia pesa hizi", amesema

McAllister alisisitiza kupatiwa majibu ya papo kwa papo, na kama ikishindikana, basi iwe ni ndani ya saa 48.

------

European Union granted 27mil euros of European taxpayers' money to Tanzania to combat the effects of Covid.

Now we have a regime in the country saying that there is no Covid in the country. We've rather bizzare explanations.

So once again, we have a government who's refused to follow guidelines from the WHO; a government that has refused to provide statistics -- and still we are giving them 27mil euros.

I'd like you to inform members of our committee about the money we have given to Tanzania; what were the criteria for giving this money, and especially what is happening with this money.

We'rtalking about European taxpayers' money, and I have difficulties that we grant money to a government which is obviously not/trying to cooperate in a decent manner.

So could please answer my question -- and if you're not able now -- I'd expect you to provide details within 48 hours.


Soma pia >

https://www.jamiiforums.com/threads...4-5-za-michango-ya-covid-19-zimeliwa.1786433/
Sasa mbona wa Eiropeani wanataka kutulazimisha sisi tukubali kuwa Tanzania kuwa na Covid-19? Ukweli mbona unaonyesha dhahiri kuwa sio tu Tanzania bali ni Afrika kwa ujumla hakuna Covid-19. Na kama ipo basi isadi ya qatu wanaokuga kutokana na janga hili ambalo limeikumba dunia ni sawa tu na idadi ya waru wanao kufa kwa magonjwa mengine kama Malaria na HIV?
Ushahidi wangu huu hapa;
 
Watanyooka au tutanyooka pamoja na familia yako,ushabiki mwingine hauna maana hata kidogo,vitu vingine sio vya kushabikia kama tunavyoshabikia mpira wa Simba na Yanga...
Kunamambo husababishwa na watawala,awamu ya tano wameamua kuwa madikteta,wameamua kutesa wananchi,na haya ndio madhara yake,raia mioyo yao imebalilika,wamejawa na vinyongo kwa viongozi waliojipatia madaraka kwa hila.Viongozi ambao wanaamini kila jambo litafanyika kibabe.
Usilalamike kuyasikia haya kwani hili ndio zao la kuandesha nchi kama familia yako.
Watawala wanavuna walichopanda wenyewe.
 
Mitano tena [emoji3][emoji3][emoji3]
Ndio ashapewa, acha tushike adabu. Maana kaanza na kuzima mitandao, aanze sasa kupunguza mishahara ya watumishi wa umma na kuwachelewesha kupanda vyeo na madaraja. Hapo tutakuwa ukurasa mmoja
 
Watakaoisoma namba ni wananchi hao wanasiasa wataendelea kutamba mitaani na maviete
Mkuu nikwambie kitu? Amini usiamini wao ndio wataoteseka kuliko wananchi, kwasababu watalipwa mishahara mizuri kuliko wananchi lakini hawatakuwa na amani mitaani (kuanzia ofisini mpaka majumbani kwao) kwa macho ya wananchi jinsi watakavyokuwa wakiwaangalia kwa maisha magumu mtaani. Yaani riots zitaibuka muda wowote wananchi wakishachoshwa na hali ya maisha
 
Haramu ni haramu tu haiwi halali
CCM wamenajisi uchaguzi wa mwaka huu mpaka aibu
Hawana uhalali wowote mbele ya wananchi!
 
Vijana wa Tanzania acheni blah blah na kuwa keyboard worriers ukombozi hauletwi na hao mabeberu ukombozi unaletwa na nyie wenyewe siku mkitaka kufanya maamuzi ya kweli! Hizi story za ICC sijui misaada hazina mantiki yyte mnategemea kupiganiwa uhuru wenu na wengine? Maajabu haya, mko vizuri sana kwenye kuandika ila action less
 
Mkisha Shiba ugali wa bure huko kwa shemeji zenu, nduki mnakuja kuharisha humu, sio? Kama hao Mabeberu wakiamua kuchukua maamuzi hayo, wewe mla bure itakufaidisha nini?

Kwanza sio Watanzania wote tunaopinga matokeo.
Wenda hata huyo anae kupa kula anayaunga mkono matokeo.
 
vijana wa Tz acheni blah blah na kua keyboard worriers ukombozi hauletwi na hao mabeberu ukombozi unaletwa na nyie wenyewe siku mkitaka kufanya maamuzi ya kweli!hizi story za icc sijui misaada hazina mantiki yyte mnategemea kupiganiwa uhuru wenu na wengine?Maajabu haya,mko vzr sana kwenye kuandika ila action less
Kwa hiyo unashauri watu waingie msituni au una maana gani?
 
Shida iko hapa, vijana wengi hamjui athari za kunyimwa misaada na vikwazo vya biashara kwa uchumi wa Nchi masikini kama yetu.

Mwishoni mwa miaka ya 70 Mwalimu Nyerere alitaifisha mashamba ya chai ya wazungu akakumbana na vikwazo hakuna kuuza chai Uingereza na Marekani ! Mwaka mmoja tu Nchi ilikonda. No mapato no foreign exchange! Na alipo kataa kufuata masharti ya World bank na IMF tulijuta.

Wafuasi wa ujinga na CCM yenu subirini.
Kipindi hicho wazazi wako kule kijijini utawahamishia nchi gani?

Tanzania ikiwekewa vikwazo, tutakaangika sisi wa hali ya kati pamoja na wahali ya chini kabisa, kipindi huyo unae mchukia yeye akiendelea kula bata.
Kwa hiyo unachofurahia ni sumu, huenda ikapita na wewe.
 
Tuvute subira mkuu
Hapa naona EU wanatupatia fake hope lakini ukweli ni kuwa goal tayari limeshatuingia hadi 2025. Upinzani wenyewe na EU hawana evidence the fraud on general election kinachotokea hapa ni kuegemea zaidi kwenye human rights ambapo agenda kuu inaachwa pembeni.
 
Back
Top Bottom