Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Nadhani Magufuli anajiamini ana uwezo wa kuendesha kila kitu bila ya msaada wowote kutoka nje. Kiukweli hili tuliona kwa watu kama akina Mugabe na watanganyika jifunzeni miaka 5 ya mwisho ya Salmin Amour kule Zanzibar. Kama mzanzibari naunga mkono hoja ya kuondosha fedha za misaada zote kwa serekali zote mbili kwa miaka 5 ijayo.
 
mkuu uko serious sana,utaugua kisukari taratibu.

kwanza wazungu hawajawahi kuwa serious na shida zako wewe mnuka mdomo wa nanjirinji huko,kukaa na kushangiria hureeeee kwamba sasa utawala unakwenda kukomeshwa.unachelewa kupiga mswaki tu,wahi uende.
Watu wanawapa hela hadi za madawa na kusambaza umeme vijijini alafu unasema hawapo serious man shida zetu???? Kajipange upya kilaza wa Lumumba wewe!!
 
Sasa mbona wa Eiropeani wanataka kutulazimisha sisi tukubali kuwa Tanzania kuwa na Covid-19? Ukweli mbona unaonyesha dhahiri kuwa sio tu Tanzania bali ni Afrika kwa ujumla hakuna Covid-19. Na kama ipo basi isadi ya qatu wanaokuga kutokana na janga hili ambalo limeikumba dunia ni sawa tu na idadi ya waru wanao kufa kwa magonjwa mengine kama Malaria na HIV?
Ushahidi wangu huu hapa;
 
Watanyooka au tutanyooka pamoja na familia yako,ushabiki mwingine hauna maana hata kidogo,vitu vingine sio vya kushabikia kama tunavyoshabikia mpira wa Simba na Yanga...
Kunamambo husababishwa na watawala,awamu ya tano wameamua kuwa madikteta,wameamua kutesa wananchi,na haya ndio madhara yake,raia mioyo yao imebalilika,wamejawa na vinyongo kwa viongozi waliojipatia madaraka kwa hila.Viongozi ambao wanaamini kila jambo litafanyika kibabe.
Usilalamike kuyasikia haya kwani hili ndio zao la kuandesha nchi kama familia yako.
Watawala wanavuna walichopanda wenyewe.
 
Mitano tena [emoji3][emoji3][emoji3]
Ndio ashapewa, acha tushike adabu. Maana kaanza na kuzima mitandao, aanze sasa kupunguza mishahara ya watumishi wa umma na kuwachelewesha kupanda vyeo na madaraja. Hapo tutakuwa ukurasa mmoja
 
Watakaoisoma namba ni wananchi hao wanasiasa wataendelea kutamba mitaani na maviete
Mkuu nikwambie kitu? Amini usiamini wao ndio wataoteseka kuliko wananchi, kwasababu watalipwa mishahara mizuri kuliko wananchi lakini hawatakuwa na amani mitaani (kuanzia ofisini mpaka majumbani kwao) kwa macho ya wananchi jinsi watakavyokuwa wakiwaangalia kwa maisha magumu mtaani. Yaani riots zitaibuka muda wowote wananchi wakishachoshwa na hali ya maisha
 
Haramu ni haramu tu haiwi halali
CCM wamenajisi uchaguzi wa mwaka huu mpaka aibu
Hawana uhalali wowote mbele ya wananchi!
 
Vijana wa Tanzania acheni blah blah na kuwa keyboard worriers ukombozi hauletwi na hao mabeberu ukombozi unaletwa na nyie wenyewe siku mkitaka kufanya maamuzi ya kweli! Hizi story za ICC sijui misaada hazina mantiki yyte mnategemea kupiganiwa uhuru wenu na wengine? Maajabu haya, mko vizuri sana kwenye kuandika ila action less
 
Mkisha Shiba ugali wa bure huko kwa shemeji zenu, nduki mnakuja kuharisha humu, sio? Kama hao Mabeberu wakiamua kuchukua maamuzi hayo, wewe mla bure itakufaidisha nini?

Kwanza sio Watanzania wote tunaopinga matokeo.
Wenda hata huyo anae kupa kula anayaunga mkono matokeo.
 
Kwa hiyo unashauri watu waingie msituni au una maana gani?
 
Sina lolote mimi au hao mnawaowaita mabeberu!?
Huna lolote! Sisi tusiotegemea mabeberu hatuna hata habari tunajua tutadunda tu. Na miradi yetu itaendelea kama kawaida tu.
 
Kipindi hicho wazazi wako kule kijijini utawahamishia nchi gani?

Tanzania ikiwekewa vikwazo, tutakaangika sisi wa hali ya kati pamoja na wahali ya chini kabisa, kipindi huyo unae mchukia yeye akiendelea kula bata.
Kwa hiyo unachofurahia ni sumu, huenda ikapita na wewe.
 
Tuvute subira mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…