Habari za mida wanajamvi!
Naam, kumepambazuka huko Duniani, wazungu wamesikia kilio cha wanao penda demokrasia Tanzania, kwa umoja wao wameazimia kuwa watainyima Tanzania misaada inayo fikia Tshs trilioni 1.64 kwasababu haifuati ustaarabu wa kidunia wa multipartism yaani demokrasia ya vyama vingi.
Kilicho nifurahisha zaidi ni kwamba , wanasema kama Tanzania ikiendelea kukaidi basi itawekewa vikwazo vya kiuchumi ISIFANYE BIASHARA NA NCHI YEYOTE YA ULAYA. HAPO SASA!!
Nini maana yake? Ni kwamba hatuta uza chai kwao, wala kahawa haitauzwa kwao, maua na mbogamboga kamwe hatutauza kwao. Hatutauza dhahabu, hatutauza korosho wala minofu ya samaki. Yaani hatutauza chochote kwao.
Baada ya muda mfupi tu fedha yetu itashuka thamani usipime. Yaani dollar moja yaweza kuwa Tshs 5000/= kisa? Mtu mmoja hataki uchaguzi uwe huru , wa haki, credible na transparent!
Wazungu nimewavulia kofia! Nimetabasamu kwa mara ya kwanza tangu October 28. Ahsanteni wazungu .bye