Pre GE2025 Kamati ya Maridhiano ya Taifa yashangaa CHADEMA kufanya Maandamano wakati Taifa lina Misiba mitatu mikubwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kamati ya Amani na Maridhiano inayoongozwa na Sheikh Alhad Musa Salum imesema siyo Haki Chadema Kufanya Maandamano wakati Huu nchi ikiwa Kwenye Misiba mitatu mikubwa

Kamati hiyo imewataka Chadema wafanye utu kwa kuahirisha Maandamano hayo hadi Shughuli za mazishi zikamilike

Mchungaji Mlata amewasihi Sana Chadema wajaribu Kuwa na Utu badala ya kulifarakanisha Taifa

Source Upendo TV

Mlale Unono πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Hiyo kamati ya maridhiano inardhiana na Nani? Na iliundwa na Nani? Hiyo kamati ya maridhiano ingekuwa na utu ingekuwa imeisha arodhesha watu wote walio potea na kuuwawa kipindi cha Magufuli. Hapo wangekuwa na nguvu ya kuongelea utu.
 
Jo, huruma zisizo na msingi wakati mwingine ni dhambiπŸ€”. Hivyo jiepushe nazo🫠
 
Hatulali unono wala nini!Tupo ofisi za CDM tunasubiri gari liwake.
 
Misiba mitatu ya akina Nani
 
Huyo Alhad Salum ndo yule yule ama? Hiyo misiba kataja ni ya kina nani?
 
CHADEMA ni wapuuzi sana! Taifa liko katika majonzi na maombolezo wao wanaandamana!

Akili za kijinga na kitoto toto kama hizo ndo maana wananchi huwadharU!

Maandamano yenu lazima yadode!

Halafu kumbe CHADEMA husomba watu wa kuandamana kutoka sehemu mbalimbali?! Nimeshangaa sana!

Nimeongea na Kiongozi mmoja wa CHADEMA mjini Musoma eti CHADEMA- Maandamano imewambia
Musoma mjini ipeleke waandamanaji 300 Mwanza na wajigharamikie wenyewe safari yao kwani CHADEMA haina Hela. Aibu saaana!!!!
 
Kamati ya amani na maridhiano !!! πŸ™„πŸ™„
Maridhiano ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…