Kamati ya masaa 72 yaifuta kadi nyekundu ya Derick Mukombozi

Kamati ya masaa 72 yaifuta kadi nyekundu ya Derick Mukombozi

Ligi inazidi kunoga, Kila mtu ashinde anavojua...

Kamati ya Masaa 72 imefuta kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi, katika mchezo dhidi ya Simba SC. Uamuzi huu umefikiwa baada ya kamati kupitia kwa kina ripoti ya mwamuzi na kulinganisha na picha za video za tukio husika.

Baada ya uchunguzi, kamati imebaini kuwa maelezo ya mwamuzi hayalingani na kile kilichoonekana kwenye video, hivyo kadi hiyo imeonekana kuwa batili. Kutokana na uamuzi huu, Mukombozi hana hatia yoyote na atakuwa huru kuendelea kuitumikia Namungo kwenye michezo inayofuata.View attachment 3246118
Ni jambo la kushukuru kuona haki imetendeka.

Ila bado kwa upande wa yule mwamuzi! Natamani kuona anapewa adhabu kali, ikiwezekana afungiwe maisha kuchezesha mechi zote zinazotambuliwa na TFF, ili iwe fundisho kwa waamuzi wengine wenye tabia mbaya kama ya kwake.

Kwa wapenda michezo wote tulishuhudia ule uonevu waliofanyiwa Namungo na yule mwamuzi tangu mchezo unaanza kiasi cha kusababisha wachezaji wa Namungo kumlalamikia mara kwa mara.
 
Ni jbo la kushukuru kuona haki imetendeka.

Ila bado kwa upande wa yule mwamuzi! Natamani kuona anapewa adhabu kali, ikiwezekana afungiwe maisha kuchezesha mechi zote zinazotambuliwa na TFF, ili iwe fundisho kwa waamuzi wengine wenye tabia mbaya kama ya kwake.

Kwa wapenda michezo wote tulishuhudia ule uonevu waliofanyiwa Namungo na yule mwamuzi tangu mchezo unaanza kiasu cha kusababisha wachezaji wa Namungo kumlalamikia yule mwamuzi mara kwa mara.
Hii ni Bongo no one cares... Ataambiwa apunguze tu mengine n ujanja ujanja hao wa kumpa adhabu kwanza ndo walishangilia matokeo
 
Ni ajabu mwamuzi hajachukuliwa hatua yoyote kwenye hiyo taarifa.
Na usije ukashangaa mechi zijazo akapangiwa tena kuchezesha mechi za simba na kuendelea kufanya maamuzi yake ya kipuuzi.

Waamuzi wajinga kama hawa ni kuwaondoa kabisa kwenye orodha ya waamuzi wenye sifa ya kuchezesha mpira wa miguu chini ya TFF.
 
Acha kuongea mambo kwa hasira hivi kakosa kamoja ni kakumfungia mtu maisha kuchezesha mpira?
Ungetaka iwe hivyo ligi hii angepona refa gani?
 
Refa hajaadhibiwa? Au ni kamati nyingine?

Namungo wanakuwa compensated vipi kwa maonevu waliyopata?

Wachafuzi na wachambaji watuombe radhi raia ..
Wamekuwa compensated kwa kadi kufutwa hivyo wataweza kumtumia mchezaji wao muhimu Derick Mukombozi kwenye game zijazo za ligi
 
Msimu huu makolo wamedhamiria kwa nguvu zote waivuruge hii ligi,wamenunua hadi wachambuzi kuficha maovu yao huku washabiki wao wakihamasishana propaganda za mitandaoni huku wakiwa na backup ya kidau katibu wa tff,but awatoshinda huu ujinga wao
Sasa kama mnajua hawatoshinda mnahangaika nini na kulalamika mtandaoni kwa kitu unachojua hawataweza
Kuweni na amani mtetee vikombe vyenu simba hataweza chochote mbele yenu
 
Haya tuone Yanga watalalamikia nini tena maana kadi waliyosema haikuwa halali tayari imeshafutwa
ngara23 Tate Mkuu
Kilichobakia kwa sasa ni kuona tu mwamuzi anachukuliwa hatua kali, kwa kushindwa kwake kuchezesha mpira wa miguu kwa kufuata sheria 17! Ili iwe fundisho kwa waamuzi wengine wote wa aina yake.
 
Kilichobakia kwa sasa ni kuona tu mwamuzi anachukuliwa hatua kali, kwa kushindwa kwake kuchezesha mpira wa miguu kwa kufuata sheria 17! Ili iwe fundisho kwa waamuzi wengine wote wa aina yake.
Kwa kosa moja tu kama hilo labda afungiwe kukosa kuchezesha mechi 3 za ligi au akatwe tu posho ya mchezo husika ili aumie kwa kushindwa kuwa makini
 
Kwa kosa moja tu kama hilo labda afungiwe kukosa kuchezesha mechi 3 za ligi au akatwe tu posho ya mchezo husika ili aumie kwa kushindwa kuwa makini
Hapo juu kuna wadau wametoa na ushahidi wa huyo mwamuzi kufanya maamuzi uenye utata kwenye mechi ya Coastal vs Simba iliyoisha kwa sare ya 2-2! Maana yake siyo mara ya kwanza kufanya maamuzi yenye utata.
 
Hii ligi inashuka thamani kwa ajili ya waamuzi wananjaa sana mpaka wanasahau wajibu wao ni kusimamia haki
 
Msimu huu makolo wamedhamiria kwa nguvu zote waivuruge hii ligi,wamenunua hadi wachambuzi kuficha maovu yao huku washabiki wao wakihamasishana propaganda za mitandaoni huku wakiwa na backup ya kidau katibu wa tff,but awatoshinda huu ujinga wao
Naunga mkono hoja kaka
 
Back
Top Bottom