Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyompa silaha muuaji wa Lemax Bar iwajibike

Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyompa silaha muuaji wa Lemax Bar iwajibike

Nakumbuka early 2003/4 kati ya hiyo miaka miwili mjomba'angu (sasa marehemu) baada ya ukwasi kuwa mwingi aliona ajiongezee ulinzi aka-apply naye amiliki silaha njia zote alifanikiwa ila police post ya pale mtaani (Mabibo kipindi hiko) alikuwa na kesi ya kumpiga mkewe na stuli habari yake ikaishia hapo.

Mpaka anafariki hakuwahi kupewa kibali, ni kusema baadhi ya watu kwenye system kukosa maadili ndo kunachangia. Kuna siku tena pale Kariakoo jamaa na ki-IST chake kaguswa kidogo kwenye bumper la nyuma na bus Eicher kashuka na chuma hata dereva wa daladala yenyewe hajasema neno yeye ana mkwaju mkononi kilichosaidia kulikuwa na police karibu wakaja wakaondoka naye.
 
View attachment 1858098
Moja kati ya sherehe zake akiwa hai

Wengi wetu tumeona video na picha zilizosambaa za tukio la Mtu kupigwa risasi akiwa Baa Sinza kwa Remi Dar es salaam usiku wa July 17 2021.

Kwa mujibu wa shuhuda ambae pia ni Rafiki, Kijana aliyepigwa risasi na kufariki anaitwa Gift na alikua amekaa jirani na Alex na alisimama kumtuliza Alex baada ya kuona ameanza kutishia Watu kwa bastola yake, amesema Shuhuda huyu.

“Gift ni Kijana mwenzangu tukifanya kazi Ofisi moja, alikua ana muomba Alex asipige risasi kama vile na kupoteza amani, yani kitendo cha Gift kumsemesha yule Jamaa imekua kama kosa aligeuka akammiminia Gift risasi nyingi kama mbuzi, Gift kuona vile akakimbia lakini akaishiwa nguvu hatua chache tu”

“Tulishindwa kutoa msaada kwa Gift kwa sababu Jamaa mwenye Bastola (Alex) alikua kama amevurugwa Shetani kama amemuingia anageuka anaangalia nani mwingine ampige risasi.

My Take
Nimeambiwa jamaa Alex alipewa kibali cha kutumia bastola miezi kama mitatu iliyopita. Ni dhahiri kwamba kamati haikufanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa kibali. Tukio linaonyesha huyu mtu ana shida kichwani na mwepesi kuvurugwa. Kamati ya Ulinzi iwajibishwe
Ni vigumu sana wanaotoa vibali vya silaha kujua mtu akishapata silaha ataitumia namna gani. Kama huyu jamaa alikuwa hana rekodi yoyote mbaya hiyo kamati unailaumu bure. Wa kulaumiwa ni 1. Watu walio karibu naye. Walitakiwa watoe ripoti polisi hata kwa kificho kuhusu tabia yake baada ya kumiliki silaha. 2. Mwenye Bar/wahusika wa bar aliyokuwa anakunywa. Huyu ndiye anabeba lawama kubwa zaidi kwa sababu alitakiwa aite polisi baada ya jamaa kuanza mawenge
 
Tangazo Tangazo ndugu wananchi mnaombwa kwenda kuchukua mafaili yenu Mirembe kwani pamejaa, mkae nayo nyumbani mtakuwa mkiyabeba pindi mkitaka kwenda hospital.....
View attachment 1858096

Haha …!

Tabu ilianzia hapa
IMG_1382.jpg
 
Lawama zinarudi kwa watoa vibali na watu wa karibu na muuaji....Ukiskia ndugu yako anataka kumiliki silaha ogopa sana hiyo kitu... maana silaha ya moto kiukweli haina chaguo...mwenye silaha ya moto yoyote yule tayari anakuwa ameshaweka dhamira ya kuua.
 
Anaonekana alikua na vitu vyake kichwani kibao na alikua na lengo la kujiua muda mrefu alikua anatafuta sababu tu na alishajitabiria kuwa bastola ndio itakayomuua..kamuua mshikaji mwingine bila sababu ya msingi...
 
Kuna mmoja Sinza bar ya Dolphin anaitwa Wambura kuna siku miaka kadhaa nyuma alileta taharuki na bastola yake. Alimchapa mshkaji ya mkono.
Kweli Mkuu ilikuwa mida ya jioni tulikuwa tunaangalia mpira, jamaa wakapishana kauli dah jamaa akawekaa, ikamchana mkono, Wambura mkorofi namjua sana, anapenda kutembea na silaha hiyo kiunoni yaani ni mshamba, wakati watu waelewa
tunaziacha kwenye magari..
 
Nakumbuka early 2003/4 kati ya hiyo miaka miwili mjomba'angu (sasa marehemu) baada ya ukwasi kuwa mwingi aliona ajiongezee ulinzi aka-apply naye amiliki silaha njia zote alifanikiwa ila police post ya pale mtaani (Mabibo kipindi hiko) alikuwa na kesi ya kumpiga mkewe na stuli habari yake ikaishia hapo.

Mpaka anafariki hakuwahi kupewa kibali,nikusema baadhi ya watu kwenye system kukosa maadili ndo kunachangia.kuna siku tena pale Kariakoo jamaa na ki-IST chake kaguswa kidogo kwenye bumper la nyuma na bus Eicher kashuka na chuma hata dereva wa daladala yenyewe hajasema neno yeye ana mkwaju mkononi kilichosaidia kulikuwa na police karibu wakaja wakaondoka naye.
Angenyoosha mkono angepata kibali, miaka ya nyuma huko 2000s kuna mtu alikuwa anakaa Kibamba akaombea kibali Tabata ambako hajawahi hata kukaa akapata kibali
 
Kweli Mkuu ilikuwa mida ya jioni tulikuwa tunaangalia mpira, jamaa wakapishana kauli dah jamaa akawekaa, ikamchana mkono, Wambura mkorofi namjua sana, anapenda kutembea na silaha hiyo kiunoni yaani ni mshamba, wakati watu waelewa
tunaziacha kwenye magari..
Duh noma mkuu kumbe nawe ulikuwepo ile siku 😂😂😂. Sinza na Chuga huu ujinga upo sana. Ni mambo ya kikolo sana.
 
Huwa hawapimwi akili bali wanaulizwa tu maswali kama

Wewe siyo mwehu?

Hauna faili milembe?

Tukikupa hautopiga watu ovyo?

Mbu wakiingia kwako usiku nao utawapiga risasi?

Maswali kama hayo ndo wanayoulizwa na mengine mengi. Ukijibu yote unapewa kibali
Kamati ya wapi hii yenye utaratibu rahisi hivi? Guys yeyote mwenye silaha Hata kama ni RPC na yupo na influence of alcohol kaa mbali. Pia
askari yeyote Anaelewa mazingira hatarishi, na wengi hujua mida gani Si ya masihara . Haya mengine mengi huku vijiweni ni kuchangamsha genge
 
View attachment 1858098
Moja kati ya sherehe zake akiwa hai​

Wengi wetu tumeona video na picha zilizosambaa za tukio la Mtu kupigwa risasi akiwa Baa Sinza kwa Remi Dar es salaam usiku wa July 17 2021.

Kwa mujibu wa shuhuda ambae pia ni Rafiki, Kijana aliyepigwa risasi na kufariki anaitwa Gift na alikua amekaa jirani na Alex na alisimama kumtuliza Alex baada ya kuona ameanza kutishia Watu kwa bastola yake, amesema Shuhuda huyu.

“Gift ni Kijana mwenzangu tukifanya kazi Ofisi moja, alikua ana muomba Alex asipige risasi kama vile na kupoteza amani, yani kitendo cha Gift kumsemesha yule Jamaa imekua kama kosa aligeuka akammiminia Gift risasi nyingi kama mbuzi, Gift kuona vile akakimbia lakini akaishiwa nguvu hatua chache tu”

“Tulishindwa kutoa msaada kwa Gift kwa sababu Jamaa mwenye Bastola (Alex) alikua kama amevurugwa Shetani kama amemuingia anageuka anaangalia nani mwingine ampige risasi.

My Take
Nimeambiwa jamaa Alex alipewa kibali cha kutumia bastola miezi kama mitatu iliyopita. Ni dhahiri kwamba kamati haikufanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa kibali. Tukio linaonyesha huyu mtu ana shida kichwani na mwepesi kuvurugwa. Kamati ya Ulinzi iwajibishwe
Poor vetting...
 
Back
Top Bottom